Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo ahamia CHADEMA

yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,113
1,102
Katika hali ya kuonyesha CCM hapako shwari leo mkuu wa Wilaya Gabriel Kimolo amevua gamba na kuvaa Gwanda hii leo ni kwenye Kongamano linaloendelea muda huu katika hotel ya Land mark ambapo wangeni rasmi ni Tundu Lisu, Mnyika, Lema, Msigwa, Heche na Kilewo.

Akiongea na watanzania waliojana kwenye kongamano hilo Kimolo amesema CCM inakufa na kuna kila ishara za CCM kufa mfano kuuwa waandishi wa habari, kutesa wana harakati, kutumia nguvu nyingi kuzoofisha upinza hasa CHADEMA pia amewaomba watanzania kujiunga na chadema kwani kwasasa ni tumaini la watanzania na kuna kila ishara kuwa inaenda kuongoza nchi...


Nawasilisha

============
Gabriel Kimolo, alijiuzulu mwezi Mei 2012 (Ref https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/262111-mkuu-wa-wilaya-ya-mbozi-atangaza-kujiuzulu.html ) kufuatia madai kuwa alikuwa akikejeliwa na wafanyabiashara wakimwita Mbwa!
===============
==================



Gabriel Kimoro




 
Yegella
Isije ikawa ni mkuu wa wilaya 1993 - 2004. Hizo zitakuwa ni propaganda mbaya. Kama ni incumbent DC, is very big up.
 
Ni Mkuu wa Wilaya gani?atakuwa amefanya uamuzi mgumu kujitoa sasa,lakini kama Ukuu wa Wilaya alishapigwa chini basi bila shaka ni njaa inauma.

Na hili ndilo tatizo la maisha yote kutegemea siasa, badala ya siasa kuwa kwa ajili ya utumishi, watu wamewekeza kwenye siasa kama ndio njia yao pekee ya kupata chakula,kwa walio wengi,mwisho wake ni mbaya sana.
 
Kimolo alikua mkuu wa wilaya huko mbeya....nadhani hadi mwaka jana.
 
Huyo ndg nahis ni yule aliekuwa MBEYA km ckosei alijiudhulu,,,!
hakujiudhuru alishaambiwa kuwa jina lake halipo kwenye wakuu wa wilaya wapya akaamua kujifanya anajiudhuru kumbe alishatemwa na mizengo kwa uzembe wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…