Aliyetangaza ''afya ya Mugabe imedhoofika'' akamatwa

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
773
Waandishi wawili wa Zimbabwe wamekamatwa kuhusiana na ripoti ya gazeti moja ilioelezea kwamba afya ya rais wa taifa hilo Robert Mugabe 'imedhoofika' alipoelekea nchini Singapore kwa kile afisi ya rais huyo ilisema ni zaira ya kimatibabu.
Muhariri wa gazeti la kibinafsi la NewsDay ,Wisdom Mudzungairi na mwandishi aliyeandika ripoti hiyo Richard Chidza hatahivyo wameachiliwa na ni sharti wajiwasilishe mahakamani.
Wakili wao Obey Shava amesema kuwa wameshtakiwa kwa kuhujumu na kutusi afisi ya rais.
Taarifa hiyo iliosema 'Mugabe yuko katika hali mbaya' ilinukuu duru zikisema kuwa rais huyo alisafirishwa kwa ndege siku ya Jumatano alfajiri. Mugabe alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya mwaka 93 na amekuwa katika mamlaka tangu 1980.
Kulingana na chombo cha habari cha AP, watu wanaopatikana na hatia ya kumtusi Mugabe, uhudumia kifungo ijapokuwa kesi nyengine zimetupiliwa mbali.
 
Kila kitu kina mwisho, inasikitisha tu vile wengine wamekufa bila kuishuhudia ile siku ya anguko
 
Sometime huwa najiuliza kama sio wazungu kututawala na ku create nchi zetu, sijui ingekuwaje? Yaani ubinafsi umetutawala sana, kila kabila ingekuwa ndio nchi.
 
Siku Africa ikiamka kutoka usingizini basi kesho yake Yesu anarudi.

Nami huwa naamini kuwa waafrika tulitakiwa labda tuishi porini kama manyani hivi. Maana kuna mambo tunafanya yanadhihirisha kabisa ujuha wetu. Yaan mtu anakuwa Mungu asitajwe. Aiseee......, kweli laana ilituingia
Hayo maneno yakupate kwako tu sio kwetu, kwani mdomo unaumba! Na iwe kwako Kama matamshi yako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom