Aliyeng’atwa ulimi kushtakiwa

Aliyeng’atwa ulimi kushtakiwa

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Majeruhi wa kung’atwa ulimi, Saidi Mnyambi (26), amefunguliwa shtaka la kujaribu kubaka.

Mnyambi ambaye aling’atwa ulimi hadi kukatika na mwanamke kwenye tukio la ngono, ‘kibao’ kimemgeukia na yuko chini ya ulinzi wa polisi wodi namba nne alikolazwa kwa takriban wiki moja akituhumiwa kwa jaribio la ubakaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba amesema wanamshikilia Mnyambi baada ya awali kumkamata Mwajabu Jumanne (36) kwa tuhuma za kujeruhi kwa kung’ata ulimi.

“Tumelazimika kuwashikilia wote wawili kutokana na kila mmoja kumtuhumu mwenzake. Baada ya uchunguzi wa kina tutafikia maamuzi stahiki,” amesema.


Chanzo: Mwananchi
 
36-26! Huyo dogo inaelekea anapenda sana 'mimama'!🙂🙂
 
Bora kaishia kunyofolewa ulimi kuliko angenyofolewa kifanyio
Kifanyio cha nini sasa wakati anashindwa kuongea. Atamsomeshaje demu? Au atatumia zile mbinu za kale za kuandika barua!!!
 
Win-win situation siioni hapo.
It is too bias aiseh
 
kwa hali hii bora kupimiana kwenye vikombe kuliko kung'atana!!
 
Hata mi nilihisi kua jamaa alitaka mzigo kwa nguvu kwa sababu jirani kalewa ndio akang'atwa ulimi

Ngoja tuone serikali itaamua nini ?
 
Mi tangu mwanzoni nilihisi kuwa huyu nyumbu ni mbakaji tu.
 
Ni mjinga kiasi gani huyo hah haha alazimishe kubaka huku akiwa anang'ang'ania kunyonya denda? Hapo kuna walakini
 
Back
Top Bottom