Aliyemuua mke wake kikatili Kagera atiwa mbaroni

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,400
Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumtia mbaroni Sendon Andrew mkazi wa kijiji cha Byamtemba kilichopo katika kata ya Nsunga iliyoko wilayani Misenyi mkoani Kagera aliyekimbilia nchi jirani ya Uganda kwa tuhuma ya kumuua kikatili mke wake Rosemery Desdery kwa kumpigwa fimbo na mateke katika seheme mbalimbali za mwili wake.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera mrakibu mwandamizi wa jeshi hilo Abel Mtagwa ambaye pia ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa huo,amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya mauaji hayo kwenye eneo la Sebure ya nyumba yao alimburuza marehemu hadi kwenye chumba chao cha kulala na kumfunika na blanketi na wakati akitoroka aliwambia watoto wao kuwa amemuacha mama yao amelala na anaondoka atarudi kesho yake.

Kaimu kamanda huyo akitoa wito kwa wananchi amesema jeshi hilo halitawavumilia mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya mauaji kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Chanzo: ITV
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom