Aliyemtisha Rais Kikwete.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyemtisha Rais Kikwete....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rungwe, Oct 31, 2011.

 1. rungwe

  rungwe Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  [​IMG]
  Katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alitoa ahadi kedekede za kuwavutia wananchi. Maisha bora kwa kila mtanzania, kukomesha rushwa na kuondoa kero zote zilizokuwa zikiwasumbua watanzania. Mheshimiwa Kikwete aliahidi kutekeleza hayo yote kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.

  Mara tu baada ya kuingia ikulu, mheshimiwa Rais akaanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo. Waziri mkuu wake Mheshimiwa Edward Lowasa mara moja akaitisha mikutano kadhaa ya viongozi wa bodi za mazao ya pamba, korosho, kahawa na kadhalika. Lengo la mikutano hiyo iliyofanyikia katika ukumbi maarufu wa Karimjee lilikuwa kuchambua matatizo yanayo wakabili wakulima, kuandaa mikakati mpya ya kuboresha uzalishaji wa mazao hayo, na kuandaa mbinu za kuwawezesha wakulima ili waweze kuzalisha katika kiwango cha juu zaidi na kuweza kuuza mazao ya biashara nje ya nchi.
  [​IMG]
  Wakati mheshimiwa Lowasa akishughulika na maswala ya wakulima, Rais Kikwete akafanya ziara maalum katika mkoa wa Dar es salaam ili kujua matatizo yanayo likabili jiji hilo ambalo kwa kiasi kikubwa ndio linawakilisha hali ya miji mingine midogo. Katika ziara hiyo Rais alikagua miundo mbinu ya jiji, maeneo ya biashara na maofisi kadhaa ya serikali ili kupata picha halisi ya mahitaji ya wananchi.


  [​IMG]Si hivyo tu, Rais akatembelea magereza ya Keko, Ukonga, na Segelea ambako alikutana na wafungwa na kuzungumza na maafisa wa magereza ili kujua matatizo yanayo wakabili wafungwa na maaskari. Kwa mara ya kwanza katika historia, Rais wa nchi akazungumza mpaka na wafungwa waliohukumiwa kifo na kuwaahidi kuzipitia upya kesi zao ili kuweza kuwasamehe wale ambao wanastahili msamaha. Aidha Rais akaagiza wafungwa hao wapewe chakula kizuri na huduma nyingine bora ambazo binadamu anastahili. Mpaka hapo kila mtanzania akaruka ruka kwa furaha...hatujawahi kupata Rais mwema kama huyu.


  Zikafuatia ziala za ghafla katika hospitali, maofisi ya serikali na sehemu nyinginezo ambazo katika utawala uliotangulia watu walisha sahau kwamba Rais wa nchi anapaswa kufika. Lengo ikiwa ni kuwaamsha wananchi ili wawajibike wakati wote wakijua kuwa Rais anaweza kuja wakati wowote.


  Mwezi Desemba ulipofika, serikali ya Rais Kikwete ikaandaa sherehe kubwa ya uhuru. Sherehe hiyo tofauti kabisa na nyingine zilizo tangulia ilikuwa na lengo la kurudisha moyo wa uzalendo kwa watanzania, ili wananchi waipende na kujivunia nchi yao. Kwa mara nyingine watanzania wakapiga makofi na vigelele kwa kupata Rais anaefaa.

  [​IMG]Ghafla ukasikika uvumi wa ajabu. Kwamba kuna watu waliokuwa wanatoa vitisho kwa Rais Kikwete na kwamba maisha yake yalikuwa hatarini. Baadhi ya raia wakapiga kelele sana na kuwaomba polisi na idara ya usalama wa Taifa kuongeza ulinzi kwa Rais wetu ili mabedui hao wasije wakamdhuru. Hata hivyo, hakuna aliyemgusa Rais na baada ya muda uvumi huo ukatoweka.

  [​IMG]Tatizo ni kwamba, uvumi huo uliondoka na Rais Kikwete wetu tuliyekuwa tukijivunia. Ushujaa, wema na mikakati ya Rais kikwete tuliyokuwa tumeanza kuiona ikayeyuka kama samli katika kikaango. Hali mbaya ya maisha ikavamia nchini kama moto wa petroli. Wezi, mafisadi na wahujumuwa mali za umma wakaanza kutamba waziwazi bila kujali kwamba kuna serikali halali na Rais aliye chaguliwa kwa ridhaa ya wananchi. Mikataba ya aibu ikawa inaendelea kufanyika huku serikali ikiwa kimyaa kana kwamba mafisadi hao ni waajiliwa wa serikali. Mpaka ilipofika uchaguzi wa mwaka 2010, watanzania waka wana jiuliza mara mbili kama kweli anastahili kurudishwa ikulu.


  Hapo ndipo tunapojiuliza, kubadilika kwa Rais Kikwete kulitokana na vitisho alivyo vipata au ni 'change of heart?' Kama ni vitisho, ni mtu gani anaethubutu kumtisha Rais? ina maana huyo mtu haogopi majeshi yetu yote ya ulinzi na usalama? ana ubavu kiasi gani huyo mtu? Au anajua siri gani za Rais Kikwete kiasi cha kum- blackmail? Rais Jakaya Kikwete tunaemjua ni mwema, mpole, mkarimu, mwingi wa huruma, Rais anaethubu kuwaonea huruma wafungwa walioua na kuagiza watendewe haki. Ndio maana tunajiuliza ni nani aliye mtisha? Tunaomba anaejua, atupatie jawabu.


  mwana dikala
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  New world order
   
 3. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa huyu mkulu alianza na moto sana sasa ni nani huyo aliyemtisha na kuvuruga maendeleo yetu??
   
 4. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Zilikuwa mbwe mbwe tu za kuingilia MAGOGONI ilipo pepo ya TZ!
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  kikwete choka mbaya
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mbona mkulu yuko juu sana bado ukifanya ulinganifu

  Tatizo TZ matatizo ni mengi na wakamishaji kibao
   
 7. k

  kaluu Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna aliyemtisha tatizo yale yote ilikuwa ni usanii mtupu hana uwezo huo.tumsamehe bure
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ni yeye mwenyewe tu hana lolote huyu........unacheza na nguvu za soda?!!
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  kajitisha mwenyewe kwa kugawia watoto wa mitaani pipi badala ya elimu...
   
 10. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Jamani Huyu jamaa alikuwa anapania kuingia Ikulu kama jambo la sifa tu, hakuwa na mpango na wala hakuwahi kupanga nini anaenda kufanya kule ikulu. Bahati mbaya sana mambo yote na mikakati yote ya kuingia ikulu hakuwa amefanya yeye, kwanza alifanyiwa na Januari Makamba (tembelea website yake, www.januarymakamba.com) na baadae wakaingia mafisadi wakubwa kwa jina la wanamtandao akiwamo Samweli Sita ambaye sasa anajifanya anauchungu na nchi hii.

  Wanamtandao hao hawakuwa na lengo lolote la kuwasaidia wananchi wa Tanzania. Lengo lao kubwa lilikuwa kujinufaisha wao tu. Ili kujenga imani kwa wadanganyika, Kiwete alipo ingia ikulu akaanza zile mbwembwe tulizoshuhudia. Nawaambia watanzania wenzangu, kama kweli ruhani huyu angelikuwa na mipango ya kweli ya kuleta maendeleo asingekuwa anatoa majibu ya kipimbi ati ".....oh, sijui kwa nini Tanzania ni maskini. ......

  Mara oh Ngeleja hawezi kuleta mvua ya kujaza mabwawa ya kuzrisha umeme, ah......mimba za watoto wa shule ni kiherehere chao, ...... nitajenga uwanja wa ndege wa kimataifa Misenyi". kuadadadadeki walah huyo ndio baba wa taifa atakaye kumbukwa na vizazi vingi vijavyo.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  sanaa doti komu.
  Mnachezea m'kwere ehhhh.
   
 12. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  New brooms sweep clean!
   
 13. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hata shetani akizeeka hujifanya malaika,tulijua hafiki mbali huyo,kwani hakuwa na dhamira ya dhati toka kwenye mtima wake,na ndo maana yale yote aliyoyafanya yalikuwa nguvu ya soda.

  Ni mara ngapi tunaona watendaji wake wanakiuka maagizo yake ili hali yeye yupo.!inatia kichefuchefu kuona kauli za kiongozi mkuu wa umma zinadhihakiwa wakati kuna mamlaka husika zipo zimelala usingizi wa pono.

  Sijui tuna kwenda wapi,hatuoni hiyo impact ya semina elekezi zaidi ya vigogo kujilimbikizia mali.tusiseme sana labda ndiyo kauli mbiu yao katika semina elekezi,mali kwanza wananchi baadae

  by sammosses
   
 14. C

  Chakusonje Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aridhani nchi inaongozwa kwa mbwembwe na ubest!! Hakuna aliye mtisha uwezo wake imeishia hapo.
   
 15. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Moto wa pumba haukeshi..NI KWELI KUNA WATU RAIS KIKWETE ANAWAOGOPA, TENA SANA. Ndio waliomfikisha hapo alipo, katu hafurukuti ndo mana inakula kwetu raia.
   
 16. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yule aliyekuwa anakimbilia ikulu mpaka anapiga mieleka siyo huyu wa sasa. Zile mbio zimeishia ukingoni mwa mafisadi, wamemuweka mfukoni na serikali yake sasa anatekeleza wanayo muagiza. Mi ntamkumbuka sana yule aliyekuwa anakimbilia Ikulu mpaka anadodoka kuliko huyu asiyedondoka!
   
 17. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani tusimwonee rais Kikwete. Ki utendaji raisi kikwete hajabadilika hata chembe, isipokuwa ni mtazamo wa wale walio kuwa wafuasi wake ndiyo umebadilika.
   
 18. M

  Maengo JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kaole iko wapi?
   
 19. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,135
  Likes Received: 10,492
  Trophy Points: 280
  Hizo zilikuwa ni nguvu za soda huyo mkweree hana lolota kwisha habari yake anjua kubadilisha wanawake tu. shwaini zake akafie mbele.
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Makundi waliyoyaasisi wakati wanatafuta utawala
   
Loading...