Issa SLuu
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 2,303
- 1,801
- Mkazi wa kitongoji cha Nyashana, kijiji cha butinzya,wilaya ya bukombe mkoani geita ,ndg Embassy Muhulira(45),amenusurika kuuwawa baada ya kukatwa mapanga na mwanaume anayedaiwa alikuwa akifanya mapenzi na mke wake vichakani.
Mwabulambo alisema Mahulira ndiye alianza kumshambulia mgoni wake kwa panga, lakini alifanikiwa kukimbia huyo mgoni,na baadae alirudi na panga akaanza kumshambulia na kutokomea kusikojulikana.
Tunaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili tumfikishe mahakamani, ila tinamshikilia mwanamke kwajili ya upelelezi",alisema Mwabulambo.
Akizungumza kwenye hospitali ya wilaya ya bukombe alikolazwa, Mahulira alisema mkewe alikuwa kwenye harusi kitongoji cha jirani cha mbura hadi SAA tano usiku,hivyo akahamua kumfuata mkewe.
Baada yakuona muda umeenda na hajarudi, nilihamua kumfuatilia nikihofia ameogopa kurudi kutokana na kitongoji iko kuwa na vichaka",alisema
Mahulira na kuongeza , "Gafla nilisikia sauti ya mtoto wangu ikilia vichakani,nikamulika tochi nakuona nguo za mke wangu nikamfuata ndipo nilipoanza kushambuliwa".
Mahulira alisema aliweza kumbaini aliyekuwa anafanya mapenzi na mkewe, kwani alikuwa miongoni mwa wanafamilia ilipofanyika harusi.
Kaimu mganga mkuu was wilaya ,Dk Mahano kaji alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri tofauti na alivyopokelewa.
GAZETI MWANCHI: 22/05/16