Aliyekwapua’ Sh. 51.6 milioni NMB matatani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
GODWIN Muganyizi (44), wakili wa kujitegemea hapa nchini pamoja na wenzake watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuitapeli Benki ya NMB, Shilingi 51, 640, 000/-, anaandika Faki Sosi.Katika kesi hiyo, washitakiwa wengine ni Maseke zenge (50), Augustine Paschal Mrema (55) ambaye ni mhasibu na Ahmadi Kambona ambaye ni ofisa wa kampuni ya udalali ya Unyangala Auction Mart.

Akisoma mashtataka yao, Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali mbele ya Amillius Mchaura, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, amesema kosa la kwanza linalowakabili watuhumiwa hao ni kula njama ya kutenda kosa.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao, walitenda kosa hilo siku isiyojulikana na sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kutenda kosa la kughushi hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu Kisutu, tarehe 22 Agosti mwaka 2014 iliyoelekezwa kwa Benki ya NMB tawi la Azikiwe na Jamhuri, ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kughushi amri ya mahakama ya kuitaka benki hiyo kulipa kiasi cha Sh. Milioni hamsini na moja, laki sita na elfu arobaini (51,640,000/-).

Watuhumiwa wote wamekana mashtaka hayo na dhamana yao ilikuwa wazi, wakitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaosaini hundi ya Sh. 10 Milioni kila mmoja, hata hivyo wadhamini wao hawakuwepo mahakamani siku ya leo na hivyo watuhumiwa kurejeshwa rumande.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 13 Oktoba, mwaka huu.
 
Wizi hauna chama,we chunguza Ruzuku ya vyama vyote jinsi inavyotumika utapata jibu..
 
Hata mchepuko wa mkeo ni mwana CCM.
Hahahahah ukiona unaanza kunitukania mke wangu ambaye hahusiki hapa ujue ni kuishiwa hoja, Sioni mantiki ya kumtukana mke wangu unless Kama ulitaka nikuoe Wewe. Nadhani tushambuliane kwa hoja Sio kwa matusi
 
hela walizopiga zote hizo wanakosaje kuweka kinga nje ya milion kumi na tano kwa ajili ya mambo ya mdhamana majinga sana
 
KWA VYOVYOTE HUYO NI CHADEMA TU. LAZIMA WAMEMUIGA RUBANI
Hahahahahaha Hahahhahahaaa hapo sawa, sasa Kuna Kenge mmoja hapo juu anamtaja mke wangu! Sijui alitaka nimuoe yeye! Haha huu mchezo hautaki hasira, hio Pesa waliitumia kwenye kampeni za Kijani tu sio bure, au unasemaje Mpwa??
 
UZURI CHADEMA WANA MABINGWA WA KUCHORA MA DEAL.
 
GODWIN Muganyizi (44), wakili wa kujitegemea hapa nchini pamoja na wenzake watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuitapeli Benki ya NMB, Shilingi 51, 640, 000/-, anaandika Faki Sosi.Katika kesi hiyo, washitakiwa wengine ni Maseke zenge (50), Augustine Paschal Mrema (55) ambaye ni mhasibu na Ahmadi Kambona ambaye ni ofisa wa kampuni ya udalali ya Unyangala Auction Mart.

Akisoma mashtataka yao, Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali mbele ya Amillius Mchaura, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, amesema kosa la kwanza linalowakabili watuhumiwa hao ni kula njama ya kutenda kosa.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao, walitenda kosa hilo siku isiyojulikana na sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kutenda kosa la kughushi hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu Kisutu, tarehe 22 Agosti mwaka 2014 iliyoelekezwa kwa Benki ya NMB tawi la Azikiwe na Jamhuri, ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kughushi amri ya mahakama ya kuitaka benki hiyo kulipa kiasi cha Sh. Milioni hamsini na moja, laki sita na elfu arobaini (51,640,000/-).

Watuhumiwa wote wamekana mashtaka hayo na dhamana yao ilikuwa wazi, wakitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaosaini hundi ya Sh. 10 Milioni kila mmoja, hata hivyo wadhamini wao hawakuwepo mahakamani siku ya leo na hivyo watuhumiwa kurejeshwa rumande.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 13 Oktoba, mwaka huu.

Ukitaka andika habari kuwa na uwakika nazo. Hakuna shitaka la wizi kuhusu wakili Godwin Muganyizi Mahakamani. hapa kilichoko mezani ni NMB wanaleta figisu wasilipe pesa zinazo daiwa na NICAS AUTO CENTER. kwa uelewa wangu mfupi au kama nijuavyo mimi ipo kwenye suala hili ipo judgment na decree ambayo yaweza kukupa picha kamili ni mchezo gani unataka kuchezwa . Kwa kifupi naweza sema hivi Tuache kuwa tunachafua majina ya watu bure mtaani. Mbinu za kimjini kukwepa kulipa hazifai na kuchuafuana majina haufai pia. Ipo siku wakili Godwin Muganyizi atawashitaki na mtaishia kulipa fedha nyingi. Ngoja niwawekee vithibitisho vinavyoonesha kuwa hapakuwepo na haja ya kugushi.Hii issue inaonekana ina agenda ya siri.
 
Attachments

Back
Top Bottom