Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Awali gazeti hili lilipata taarifa kutoka katika vyanzo vyake ndani ya jeshi la polisi kwamba Dadi alikuwa akifuatiliwa na makachero wa polisi baada ya mkewe kumtuhumu ‘kutoka’ na binti yao mwenye umri wa miaka 21.
Habari zilidai kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita alionekana na makachero akiwa na msichana huyo wakiingia katika Hoteli ya Executive iliyoko Kilimani, Unguja.
Imeelezwa kuwa mara baada ya kuingia katika hoteli hiyo, Dadi na msichana huyo ambaye jina lake linahifadhiwa, alivamiwa na kufumaniwa na polisi waliokuwa na mama wa mtoto aliyekuwa naye.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kamanda Mkadam alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kisha akasema mtuhumiwa alikamatwa na askari polisi baada ya mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Sharifa, ambaye ni mama wa binti anayedaiwa kufumaniwa naye Dadi kutoa taarifa polisi.
“Sasa hivi tunafanya upelelezi na utakapokamilika tutampandisha kizimbani,” alisema kamanda huyo na kufafanua kuwa baada ya kukamatwa na polisi Dadi alifikishwa Kituo cha Polisi cha Muembe Madema saa 11 jioni.
Pia alithibitisha kuwa mtoa habari polisi ni mama wa mtoto ambaye ni mke wa mtuhumiwa huyo, alisema Dadi yupo nje kwa dhamana ya watu wawili.