SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
Amefariki Jumatatu iliyopita. Leo zimetolewa heshima za mwisho nyumbani kwake,Mwisenge, Musoma. Kesho mazishi yanafanyika kijijini Seka, Majita, Musoma.
CV:
Amemaliza University of D'Salaam mwaka 1974. Amepata PhD yake jijini Hanover, Ujerumani, mwaka 1981.
Akiwa masomoni alirudi October 1980 kugombea ubunge kwenye jimbo la Musoma Mjini. Akashindwa na Herman Kirigini. Akarudi kuendelea na masomo yake.
Mwaka 1984 aliteuliwa kuwa mkuu wa chuo cha Reli, Tabora.
Novemba 1985 aligombea tena ubunge safari hii kwa jimbo la Musoma vijijini, akashinda. Hoja kubwa ilikuwa ni kwamba katika thesis yake ya PhD aliandika matatizo yanayohusu wilaya ya Musoma vijijini.
Tatizo aliloliona lilikuwa ni elimu katika wilaya hiyo, hivyo akajikita na elimu.
Kufikia mwaka 1987 akawa amefaulu kuanzisha Shule ye Sekondari ya Nyegina. Hakufanya kama viongozi wengine ambao wakianzisha shule wanaweka watoto wa wengine wao wanasoma shule zingine.
Yeye shule hizo akaweka watoto wake wasome. Watoto wake wawili wamesoma Nyegina Sekondari.
Mwaka 1990 akagombea na akashinda kwa mara ya pili hadi 1995.
Baada ya 1995 akateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Serengeti na baadaye Mugumu. Kuna Wilaya moja alipelekwa mkoa wa Arusha nimeisahau mnaokumbuka kumbusheni.
Baada ya hapo hakuteuliwa tena nafasi za kisiasa bali akakaa kwenye projects kadhaa huko Iringa na kwingine.
Ni mmoja wa watu ambao walikuwa na uadilifu wa hali ya juu lakini inashangaza mitandao kutomjua kabisa na kifo chake kinakaribia wiki sasa.
Mungu aiweke roho yake mahali pema.