Aliyekodi watu na kumuua baba yake ahukumiwa kunyongwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,703
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, imemhukumu Seni Lisesi adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kumtia hatiani kuhusika na mauaji ya baba yake mzazi.

Lisesi (33) mkazi wa Kijiji cha Mwadui wilayani Sumbawanga, alidaiwa kuhusika kwenye mauaji ya baba yake Lisesi Magadula (50) ili arithi mali.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne ya Mei 18, 2021 na Jaji wa Mahakama hiyo Dustan Ndunguru baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Njoloyota Mwashubila na Irene Mwabeza.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, inaeleza kuwa Lisesi alitenda kosa la mauaji ya Magadula kwa kushirikiana na kikundi cha watu.

Ilidaiwa kuwa Liseni alikodisha kikundi hicho kwa ajili ya kufanya mauaji hayo mnamo Desemba 4, 2016 nyumbani kwa marehemu huko Kijiji cha Mwadui.

Ilidaiwa na waendesha mashitaka wa Serikali kwamba muuaji akiwa na wenzake walivamia nyumbani kwa Liseni nyakati za usiku wakiwa silaha aina ya mapanga na kumkatakata hadi kufariki huku lengo likiwa ni kurithi mali mbalimbali ikiwemo ng'ombe na mashamba.

Hata hivyo, Polisi katika uchunguzi wao walimtia mbaroni Liseni na kumfikisha katika vyombo vya sheria.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, waendesha mashitaka wa Serikali waliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kushiriki kukatisha uhai wa wazazi wao kwa tamaa za kurithi mali.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Ndunguru alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasi kuacha shaka na amemkuta mtuhumiwa na hatia ya kufanya mauaji ya kukusudia hivyo kwa kutumia kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 na kifungu cha 197 anahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Chanzo: Mwananchi
 
Ndugu mleta mada undeelezea kwa kirefu zaidi ili wasomaji tukuelewe sasa apo hakuna maelezo ya kutosha nani wa wap lini ilikuwaje
 
Back
Top Bottom