GE2025 Aliyeenguliwa kuwania Urais ADC, Mutamwega Mgaywa amekusudia kukata rufaa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Siku moja baada ya Chama Cha Alliance Democratic For Change (ADC) kumpata mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar, kada wa chama hicho na aliyewahi kuwa Mbunge wa Mwibara mkoani Mara, Mutamwega Mgaywa amekusudia kukata rufaa kwenda Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, kupinga mchakato huo

Msingi wa kuchukua uamuzi huo ni kutaka haki itendeke dhidi ya kitendo anachodai cha kihuni kilichofanywa na uongozi wa chama hicho kumuengua kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kugombea urais wa Tanzania, kwa kunyofoa baadhi ya taarifa zake muhimu zilizojazwa kwa ufasaha na kuwekwa nyingine asizozitambua

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Jumapili Juni 29, 2025, ukiambatana na mkutano mkuu maalumu, wajumbe wa chama hicho walimchagua, Wilson Elias kuwa ndiyo mgombea urais wa chama hicho kwa upande wa Tanzania bara huku mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Hamad Rashid akichaguliwa kugombea urais upande wa visiwani

Mgaywa aliondolewa kwenye ukumbi wa mkutano huo kinguvu kwa kile kilichoelezwa hakuwa sehemu ya wajumbe halali licha ya kuwa ni mtia nia wa nafasi ya kuomba ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho

mara.png
 
Bado hajaelewa tu,anatakiwa aunge mkono NO REFORMS NO ELECTION, Watanzania wanajua vyama vingine nje ya CHADEMA ni Mali ya CCM hivyo uchaguzi bila CHADEMA tafsiri yake ni kwamba CCM inasimama peke yake kwenye uchaguzi na kujipigia kura.NO REFORMS NO ELECTION Hesabu zetu tunazifungia hapo.
 
Back
Top Bottom