Aliye injinia kukamatwa na rushwa wabunge Arusha ni EL

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
SAKATA LA WABUNGE NA RUSHWA ARUSHA

Hizi ni habari kutoka kwa wafuasi wa wabubge hao na wanasema Waziri Mkuu awapendi kwa future politics mkoani Arusha, pia waligundua na kutokwenda kumsaidia katika harambee iliyo fanyika Hotel Impala kuchangia CCM,

Mmoja wa mpambe wa mkuu huyo amekiri ni kweli kwasababu alimuingili EL katika jimbo lake la monduli na kuwa na nafasi kubwa ya kushinda ndipo jimbo lilipo gawanya kuwa na jimbo la longodo akaomwambwa kwenda huko na akashinda kwa kishindo.

hapo ndipo chuki zilipo anzaia kwa hiyo EL anampango wa kuwamaliza kiasiasa

mwenye habari zaidi aziweke hapa
 
Nasikia sababu kubwa ni kuwa jamaa ni nguzo za mzee Sumaye. Na kwa kuwa hakuna anayejua mahesabu yake kisiasa kwa siku zijazo, wameamua kumtumia salamu kwa kupitia hao Kondoo wa sadaka. Ni alama za nyakati tu hizo...
 
Nadhani ndio anachomaanisha,just read him between the lines,pili logic na common sense vinasuggest hivyo,ebu tutazame:pCCB ndo walienda kuwakamata wabunge hao,kwa mfumo wa utendaji wa bwana Hosea ni kuwa mpaka kuwe na ushahidi,sasa IPTL,radar et al haijawahi kuchunguzwa kabisaa,pia kwa sasa tunashuhudia Buzwagi ambapo mpaka mkataba umevuja Hosea yuko kimya...sasa katika hali ya kawaida iliwezekana vipi Hosea kuwakamata wale wabunge given the fact that ni wa CCM na kuwa siku zote rushwa hutolewa kwa kificho,pia ni kwa muda gani walifanya uchunguzi mpaka kuwakamata watu hao?unless aseme kuwa waliwawekea surveillance ya CCTV...
 
Ibambasi,
Rushwa inayodaiwa ni ile laki nne alizokutwa nazo mfukoni Bw.Porokwa (Mwenyekiti wa UVCCM). Wabunge hawakukamatwa na vidhibiti mifukoni, isipokuwa wamehusishwa na hizo 400,000 pamoja na gari alilokuwa akilitumia mtuhumiwa Porokwa, kwani lilikuwa mali ya mmoja kati ya wabunge hao wawili.
 
Ibambasi,
Rushwa inayodaiwa ni ile laki nne alizokutwa nazo mfukoni Bw.Porokwa (Mwenyekiti wa UVCCM). Wabunge hawakukamatwa na vidhibiti mifukoni, isipokuwa wamehusishwa na hizo 400,000 pamoja na gari alilokuwa akilitumia mtuhumiwa Porokwa, kwani lilikuwa mali ya mmoja kati ya wabunge hao wawili.

Mkuu kwa hapo napata shida kumuelewa Hosea,unless aniambie kikomo cha mtu kutembea na pesa mfukoni,pili ni kwa vipi utathibitisha zilikuwa hela za kutolea rushwa?
lakini hata hivyo mbon kesi yenyewe ghafla imepoteza mwelekeo,au ni kwa ajili ya Buzwagi na list of shame?
 
Ndiyo maana wamepewa meno na sasa anakula bila ya uoga si nsiyo haya ama kuna zaidi ya hapa ?
 
wana jambo kuna mambo mengine tunakwenda vyema lakini mengine ynaweza kutuweka katika kuonekana watungaji,siyo kweli kwamba muheshimiwa Michael Laizer Lekule ndiye aliyesababisha jimbo kugawanywa la Monduli na kuongeza la Longido bali ni mtu ananyeitwa kapteni Ole Moloimet ambaye mpaka leo ni adui mkubwa wa EL,huyo mheshimiwa Lekule wala hakuwa na nia ya kugombea bali alipandikizwa na EL ili kwenda kumwangusha Moloimet,kama mtangumbuka mpaka mwaka 2005 Moloimet alikuwa DC wa kiteto,sasa yupo kwao Longido,Kisiasa jinsi navyoufahamu mkoa wa Arusha si Elisa Mollel wala Lekule wanaotisha wote hawana uwezo zaidi ya mmoja kuwa na fedha nyingi,kuna befu ambalo waulizeni hao wapambe watawaeleza vizuri hasa kwa Mollel,lakini pia Mollel tattizo lake siyo msafi
 
kuhusu wabunge kutokutwa na fedha navyosikia tatizo kubwa ni viongozi wapya,jamaa walianza kazi ya kutafuta wajumbe mjini Arusha wakatoka wakaenda baa nyingine karibu na pale walipokamatiwa wakagawa mshiko,miongoni mwa waliokuwemo kwenye msafara wao ni kijana wa TAKUKURU aliyevaa sharti la kijana na kujitambulisha ni mjumbe kutoka kata moja bahati mbaya hawakumtambua lakini pili simu zao ambazo jamaa wanazishikiria zina ujumbe SMS kwenda kwenye simu ambazo baadhi ya wale waliokamatwa zikiwa na ushahidi wa mgawo
 
SAKATA LA WABUNGE NA RUSHWA ARUSHA

ndipo jimbo lilipo gawanya kuwa na jimbo la longodo akaomwambwa kwenda huko na akashinda kwa kishindo.

hapo ndipo chuki zilipo anzaia kwa hiyo EL anampango wa kuwamaliza kiasiasa

mwenye habari zaidi aziweke hapa

Ni longido...
Hivi keyboard ina matatizo gani?
 
Uzuri wa siasa ndio huu, kwani kila kambi inazusha. Ukweli utajulikana baada ya mahakama kulishughulikia hili. Kesi imepangwa kusikilizwa/kutajwa tarehe 5 Oktoba, na sidhani kama uchaguzi utafanyika bila muelekeo wa kesi kufahamika. Cha muhimu kujua hapa ni kwamba PCCB huko nyuma walikuwa hawajapewa mwanya wa kushughulikia mambo yanayohusu Chama Tawala, wakati ni huu, tuondolewe uozo ndani ya CCM.
 
Hili Sakata zima la Rushwa ya Vidagaa lilikuwa na nia ya kupunguza Kasi ya Hoja ya Buzwagi na Uoza mzima wa SISIEMU.

Mimi nijuacho SISIEMU ni kitovu cha Rushwa na kamwe haiwezi jiosha mpaka ioshwe na wananchi kama ioshwavyo dhahabu, kwa Moto na Tindikali.
 
Pamoja na kuwa na hoja na maono tofauti kuhusiana na "SAKATA LA RUSHWA YA WABUNGE WA ARUSHA", ukweli mmoja muhimu ni kwamba EL ANAHUSIKA lakini na hao waliokamatwa pamoja na kuwa mahakama itaamua, nao pia si WASAFI, suala la kama wametoa ama hawajatoa rushwa linaweza kuwa gumu kuthibitisha lakini haina shaka kabisa kwamba walitoa rushwa. LAKINI JE NI WAO PEKEE KATIKA CCM WALIOTOA RUSHWA? Jibu ni HAPANA KWANI HATA HAO WAKUBWA WANAENDELEA KUTOA RUSHWA AKIWAMO EL, ZIARA YAKE MWANZA ALIKUA AKIKUTANA USIKU NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU KUTOKA SHINYANGA, MWANZA, MARA NA KAGERA KUWASHIKISHA.

LAKINI KWANINI BASI WEMEKAMATWA HAO. KUNA THEORY NYINGI LAKINI NILIZOKUTANA NAZO NI KAMA IFUATAVYO:

1---Kwanza wanasema EL alikerwa na kauli kwamba yeye anatoka ukoo wa NDOSI, ni familia ya marehemu Meja Ndosi, kwa hiyo WAMASAI (MOLOIMET, LAIZER, POROKWA etc WAMEWEKA WAZI KWAMBA, EL ni MMERU na si MMASAI, jambo ambalo limemkera sana bwana mkubwa.
2---Pili mbali ya Moloimet, wanasema Mwenyekiti wa Vijana mkoa wa Arusha, Ole Porokwa ndiye kijana anayetajwa kuwa anatakiwa kugombea jimbo la Monduli na mwaka 2000 na 2005 alikataa kujitoa hadi alipotolewa kuwania jimbo hilo. Lakini pia Binafsi nina ushahidi wa POROKWA wa barua yake ya mwaka 2004 abayo alimuandikia Katibu Mkuu wa CCM wakati huo, Philip Mangula, na nakala kumpelekea Mwenyekiti Mkapa, akilalamikia kwamba aliitwa nyumbani kwa LOWASA kusutwa kwanini hamuungi mkono yeye na rafiki yake JK katika harakati zao za urais mwaka unaofuata (2005). Katika barua hiyo niliyoipata mwaka huo (2004) Porokwa alisema kwamba EL alimwambia, "UNAJUA KIJANA wewe na wenzako wa Mara na Dodoma muligharamia na kuchochea vijana pale Dodoma kutusaliti wakati wewe tunatoka kumoja...Mimi nasema Mkapa tumeshakubaliana naye kwamba JK atakua RAIS na mimi nitakua PM, kwa hiyo amua kutuunga mkono ama kuendelea, lakini ujue tutakushughulikia. Mwenzako MAra tumeshaanza kumshughulikia."
 
Kwani EL ana mpango gani hapo baadaye? na vipi mzee Sumaye, bado naye anataka Urais? Lakini huyo Porokwa naye kwa nini alikuwa anatumia gari la Mbunge? Yawezekana pia nao hao wabunge hawako clean. Wacha tusubiri kesi, tutajua mbivu na mbichi.
 
Kwani EL ana mpango gani hapo baadaye? na vipi mzee Sumaye, bado naye anataka Urais? Lakini huyo Porokwa naye kwa nini alikuwa anatumia gari la Mbunge? Yawezekana pia nao hao wabunge hawako clean. Wacha tusubiri kesi, tutajua mbivu na mbichi.

Si Kitiyi, kama umesoma kwa makini nilivyoandika hapo juu ni kwamba hawawezi kuwa safi hata mahakama ikiwasafisha jambo ambalo si ajabu, kama Nyari ametoka seuse wabunge! Hakuna kati yao anayeweza kuwa safi. Hakuna cha ajabu kwa wagombea waliojitokeza 2005 kuibuka upya,kwani wengi wanaamini hawakutendewa haki na Ben na wanamtandao. HOja ya msingi hapa ni kwamba ACHENI SISIEMU WATAFUNANE NA HUO NDIO UTAKUA UKOMBOZI WA WATANZANIA WOTE KWANI SASA WATAOGOPA KUFANYA UHALIFU KWANI WATAMULIKANA WENYEWE NA HAPO NDIPO PA KUPASUA NA KUPATA VIONGOZI BORA NA SI BORA VIONGOZI MRADI WATOE RUSHWA
 
Halisi,
..Leipilal Ole Moloimet safari hii hata U-DC wamemnyima. Yuko wapi sasa hivi?

..Ugomvi wa Ole Moloimet na Lowassa ulianza tangu kabla ya Uchaguzi wa 1995. Moloimet alilalamika kwamba Lowassa alikuwa akigawa mashine za kusaga jimboni kwake--wakati huo akiwa mbunge wa Monduli.

..Habari za "utata wa Umaasai" wa Lowassa zimekuwepo muda mrefu sana. Je ni kweli kwamba Ngoyai Lowassa siyo Mmaasai?

..Elisa Mollel ni kiongozi wa jadi ktk jamii yake ya Wamasai. Je, Lowassa hatakuwa anagombana na Wamaasai kwa kumpiga vita "Mzee wa Jadi" wa Kimaasai?
 
Back
Top Bottom