Alisema hanitaki sasa nani alaumiwe?

Alisema hanitaki sasa nani alaumiwe?

Omwojo

Member
Joined
Mar 3, 2015
Posts
80
Reaction score
15
Niko kwenye kipindi kigumu sana wana MMU, nahitaji msaada wenu kwa ushauri na mengine.

Iko hivi;

Nilitokea kumpenda binti mmoja ambaye pia alinipenda, mahusiano yetu yalianza kama urafiki ambao ulitokana na familia zetu kuwa karibu (family friend), kwa muda mrefu tulidumu katika urafiki wa kawaida, nilipofika kidato cha nne (nilimtangulia darasa) tulianzisha mahusihano rasmi ya kimapenzi, bahati mbaya baada ya mtihan yeye hakupata ufahulu mzuri, mimi kwa kipindi hicho nilikuwa advance level.

Kutokana na familia yake kutokuwa na uwezo waliamua kumpeleka jeshini (JKT) alpomaliza akakaa two years (mkataba) kipindi chote hicho tulikuwa tunawasiliana ingawa kwa shida kutoka na yeye kutokuwa na simu alafu mimi nilikuwa boarding so mawasiliano yalikuwa likizo ingawa kwa shida sana (wakati mwingine likizo iliisha bila kuwasiliana)

Baada ya mimi kuingia chuo kikuu, yeye alipata mkataba mwingine (baada ya wa awali kumalizika bila kupata ajira) kipindi chote tulishirikiana na kupeana moyo tukikumbushana ahadi na mipango tuliyowekeana, tuligawana bum kutokana na maisha magumu ya Jeshini hasa swala la hela ya matumizi( 50000 kwa mwezi)

Mwaka wa pili wa mkataba akapata nafasi ya kujiunga JWTZ akapiga depo na kumalizia makutopola Dodoma, alinialika kwenye gwaride la kufunga mafunzo kipindi icho nlikuwa Dar es salaam, kutokana na kushindwa kufika (nilikuwa kwenye maandalizi ya UE) nikamuomba mdogo wangu aliyekuwa UDOM akaniwakilishe kule.Baada ya kuhitimu chuo na kuanza kusugua gaga kutafuta kazi na yeye akiwa mwajiriwa wa Jeshi matatizo yalianzia hapo.

Alianza visa vingi vya ajabu, kutopokea simu, text hazijibiwi, hapigi simu mpaka mimi nimtafute kuna kipindi alikuja likizo nyumbani nikaongea nae kwa kirefu kuhusu mahusiano yetu aliahidi kurekebisha kasoro hizo.

Kipindi chote kuna mambo mengi yalinihuzunisha sana, nakumbuka kipindi anaanza kidato cha kwanza aliniandkia barua (mpaka leo ninayo) barua ilisisitiza tuendlee kutunzana ikiwemo kutomtaka kimapenzi mpaka amalize masomo yake, cha kushangaza alipofika form three akaniandikia barua ya kuniomba msamaha kwamba ameshawishiwa na tayari alikuwa kwenye mahusiano na mwalimu na tayari wameshiriki ngono, nliumia sana (alimtoa bikra yule ticha).

Aliniomba msamaha kupitia dada yake nilimsamehe, kipindi ameanza kazi jeshini alikuwa kambi Morogoro alikuja Dar kikazi nikaonana nae tuliongea mengi akapewa ruhusa tukalala nae usiku ule akaniambia kule jeshini alishapata boyfrend ambaye walianza mahusiano baada ya mimi kuonekana simjali, na usiku ule alikuwa anasaliti, niilimwambia sawa kwa sababu now wewe ni mtu mzima unaamua unachokitaka.

Kwa ufupi alibadilika sana baada ya kupata kazi na mimi nikiwa mtaani nasugua gaga, aliwaambia ndugu zake mimi hanipendi tena so wasiniite shemeji, ingawa nilivyomuuliza alikataa na kunihakikishia tuko pamoja, kilichokuwa kinanipa wasiwasi muda wote niko chuo nlijitahidi kumsaidia bum likitoka na hata before kishule shule tuligawana hela nilizokuwa napewa nyumbani but alivyopata kazi kila nikimuomba msaada kidogo alinijibu ana majukumu mengi hivyo hawezi nisaidia nisubiri muda utafika.

Bahati nzuri mwaka jana nikapata kazi, sikutaka kumwambia sijui alipata wapi habari akaanza kunimiminia text za pongezi, mwezi uliopita alipata likizo nilimuomba sana apite kwangu alishtuka aliponiona nimebadirika, umbile, status na hata alipofika ndani kwangu aliendelea kushangaa.

Tangu hapo kila siku ananipigia, akinituhumu mimi ndo chanzo cha penzi letu kuyumba so anaomba tukae tuweke mambo sawa coz hataki kuolewa na mwanajeshi mwenzio ambae yuko nae now.

Najiuliza kweli nastahili lawama hizi je, nifanye nini?
 
Duh hilo ni jaribu ila kweli kabisa bila pesa dunia hii, hutapata penzi la kweli labda Mbinguni.

Achana nae bhana. Yaani anasema kabisa amegegedwa halafu na wewe unasema hewalaaaa. Wanaume hatuko hivyo
 
Akufaaye Kwa Dhiki Ndie Rafiki
Akili Kichwani Mwako ......Siku Ukipita Kwenye Magumu Tena Mvurugano Utaanza Upya
 
Jamani hili nalo la kujiuliza na kukusumbua kichwa kweli????
 
huyo sikushauri uendelee nae maana ikitokea umepigwa BAN kazini ujue ndo ataondoka huyo money maker,so kuwa makini na maamuzi yako ujue hata inzi akiacha upumbavu anaweza kutengeneza asali......
 
Sasa ushauri wa nini wakati jambo liko wazi huyo binti amekufanya zoba na ataendelea hivyo for the rest of your life. Tafuta binti mwingine ili next time akija anakutana na wifi mlangoni.
 
Pamoja na kwamba amekuwa si mwaminifu,ila kuwa mwanajeshi tu ni sababu tosha ya kuachana naye
 
Kipindi unaendelea kuchukua maamuzi jihadhari na mwanajesh walienae
 
Huyo piga chini , ukimchukua ujue kuwa lazma mjeda atakuwa anakula mzigo kama kawa, japo ww utakuwa ndo mume wake, afu kuwa huyo hana upendo wa dhati. Ulipokuwa na dhiki alikupotezea, umezipata kaja kwa sababu ya maisha mazuri huna dhiki tena. Ikitokea mbeleni mambo yakazingua atakuona takataka tu. Atatafuta penye pesa. Tafuta mwingine uanze nae ila kuwa makini japo women wengi wapo hivyo Unaweza ukabahatisha ambaye anauvumilivu walau kidogo.

Kwa ufupi huyo hakupend amependa status uliyonayo kwa sasa.
 
nahisi bado hujawa mwanaume...wanaume hatuko hivyo..uko kwenye uvulana...bado akili yako iko ndotoni..... huhitaji akili ya mtu mwingine katika hili......tena yuko morogoro wewe dsm.......hajakuficha ufirauni wake wote...kila kitu kakwambia.....haya endelea kumpenda tuuu.....au hujui kutongoza braza.....????
 
Utapata shida ukiishi nae cku uchumi wako ukiyumba Yuko kimasilahi zaidi mchaga nn ??samahan lakin
 
Tatizo ni kwamba unampenda sana na huna sauti mbele yake na ameshalijua hilo ndo mana ana ku treat kama zoba, manake niwajuavyo wanaume wewe nakuona wa ajabu tena wa ajabu sana jamani duuuh, yani wenzio wameanza kukugegedea toka sekondari mpaka leo bado upo tu tena cha kusikitisha zaidi unaomba na ushauri, ina maana tukikwambia uendelee nae tena umuoe na wewe utaona ni sahihi kabisa? plz grow a pair na be a man. LEAVE HER, huyo dada si tu kwamba hakufai wewe ila hafai kuwa mke wa mwanaume yoyote aliekamili
 
Endelea naye ili utujazie server humu M.M.U
 
pipa chini mbwa huyo, anakufanya reserve, WASICHANA WAMEJAA WENGI UTAPATA MWENYE MAPENZI YA KWELI
 
Huyo sio wa kujishauri hata mara moja,achana nae,inapaswa uwe na mke mwenye msimamo ktk maisha haya na huyo anaonekana hana msimamo na anatamaa,
 
jamaa una moyo sana mwl. kafungua upo tu, mjeda anamchezesha kwata upoo tu tena anakuthibitishia kana kwamba wewe huna libolo fc.
 
ukifunga nae ndoa huyo ujue utatudi tena humu JF kuomba ushauri kuwa nimemfumania mke wangu. JIONGEZE
 
Back
Top Bottom