Aliponisaidia tu akafa! Nina mkosi?

Pole sn ndugu yetu, ila hilo la kusema ukweli on what happened lipe kipaumbele.
Hukumuua wewe yule, ni ajali tu ilikua imeshaandikwa na Allah.
Naamini when u say it out, utapata releif zaidi.
Jengine ambalo ningependa kukushauru km walivokushauri wengine hapo juu ni vizuri ukawa unaenda mara kwa mara kwa familia ya swahiba wako hao aliowaacha wafanye km ndugu zako wa damu, hope u will be much happier.
All the best mkuu, be brave kaka
 

Ni kwei kabisa hakumuua yeye na ndio tunako elekea. Jamanii Parapandaaaaaa ....!!!!!!!
 

nakubaliana na wewe
 
Hii ilikuwa ni Saikological effect alipokataa zile Hela ulizompa kuna kitu kinatokea kwenye akili!! na huwa Concentration inapungua sana!! Hivyo umakini unakuwa haupo!! ni kama wewe ulivyoona ajali na kuanza kuduwaa kwa muda!! Hata wewe ungeweza kugongwa kwa kuvuka barabara kwa Dharura!! Mungu Amrehemu!!
 
Dah inasikitisha sana, tafuta muda wewe na mkeo mwende mkasalimie familia ya huyo bwana Mungu atakurehemu sana.
 
Pole kwa yote. jitahidi kuwatembelea wale jamaa zake. R.I.P. mwenye ukarimu kwa mwana jf.
 
Mkuu ujumbe au wosia aliokuachia marehemu unatuhusu wanadamu wote kwa ujumla. Ni ujumbe uliotoka kwa Mungu kweli! Bila ujumbe ule na maelezo yake kwako nahisi asingepata maziko yanayomstahili.
 
naamini itakuwa faraja kubwa iwapo wapendwa wa marehemu
watajua kwamba kitendo cha mwisho cha mpendwa wao kilikuwa
cha kutenda wema na kuonyesha upendo kwa mtu asiyemfahamu.

ukiipata familia ya marehemu waeleze wema wa mpendwa wao.
 
Kuna mengi usiyoyajua kuhusu marehemu.
Huna haja ya kujilaumu kwani siku yake ya kuitwa ilifika na pengine alibakisha tendo moja tu jema ili Mungu amchukue!
Inawezekana wewe ndiye uliyemsaidia zaidi, kwani muda wake ulikuwa umefika na alihitaji kutoa sadaka yake ya mwisho kwa kumsaidia mhitaji!
Amini usiamini, lakini maajabu mengi hutokea duniani.
Si ajabu mtu huyo alishakufa kabla ya wewe kufika hapo na alirudishwa briefly kukuokoa kwenye janga.
Tafuta sinema iitwayo 'the eye!' utaelewa situation yako.
unaweza kudhani ni hadithi tu lakini utajifunza mengi!
 

Hii imekaa ki falsafa zaidi! ila ni mtazamo wenye ukweli pia thanks.
 

Ntaitafuta mkuu, hii dania ina vitu visivyokuwa na majibu rahisi!
 

Hili ndilo nililokuwa nalo mwanzo, na nadhani ushauri wa askari ndivyo ulikuwa anakoelekea....
Lakini kwa ushauri wa waungwana wa humu, nta kwenda... na kuchukua tahadhari zote watu wasinielewe vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…