Aliponiona tu ameanza kulia, maamuzi yana gharama zake!

TheMnyonge

JF-Expert Member
Mar 25, 2022
739
1,870
Bila kupoteza muda niende kwenye mada!
Mwaka 2016/2017 nilikutana na binti akiwa anafanya biashara yake Fulani maeneo fulani ndani ya jiji...

Wakati huo nilikuwa napigika kuandika dissertation though sikumwambia kuwa nasoma masters, alijua nipo undergraduate (ndivyo alivyohisi, maana hakuwa kuniuliza)

Basi nikamwambia hisia zangu (by then nilikuwa serious kabisa kutaka kumuoa), akanijibu kwa kejeli mno..."Utaniwezea wapi mimi na boom lako, kwa level zangu utaishia kulala njaa na kutembea kwa miguu kwenda chuo, na bado sita-feel kama upo..."
Nikamuuliza kwani unauza? Nikashushiwa mitusi hiyo kwa sauti ya juu, mbele za watu, (kitu nisichokipenda katika mahusiano ni kuzozana hasa mbele za watu) nikaondoka nikiwa down sana!

Siku moja nikaona ameweka picha ya jamaa namfamu (anamsaidia mama mmoja kwenye mambo ya catering) nikashtuka kidogo, ila sikusema neno... kumbe bhana kajamaa ndo kanatoka na yule binti na kamemwambia ile biashara ya catering ni yake, sometimes anapita na gari ya ofisi kwa yule binti then binti akaamini kweli ni ya kwake!

Kajamaa kalimwambia binti kwamba biashara imekuwa ngumu hivyo anataka kuanza video shooting pia ila hana capital kutokana na biashara kuwa mbaya, binti akachukua ka akiba kake Mil.4, akaenda kwenye kikoba chao akachukua mil.2.5 akampatia jamaa ili anunue vitu gani sijui vya kufanyia kazi (kwa wakati huo binti alikuwa mjamzito tayari)

Jamaa baada ya kupata ile pesa akatoweka jijini, akaenda mkoani huku binti akijua jamaa yupo bize na kazi, jana nilienda maeneo ya mabibo kuonana na jamaa yangu wa kitambo naye karudi shule kuongeza darasa kidogo, sasa nimepaki tu ka premio changu nashuka namuona yule binti wa zamani akanijia kwa bashasha hivi, tukasalimiana na kupiga story kidogo nikamuaga kuwa nakwenda kumuona rafiki yangu...akanisisitiza sana nimcheck kabla ya kuondoka...nikamtajia namba akanibeep nikaondoka!

Baada ya story kidogo na jamaa tukaagana, narudi sehemu nimeacha kausafiri namkuta bado yupo pale, ila nikagundua kama hayupo sawa, kabla sijaingi kwenye gari akaniambia anaomba tuzungumze kidogo, nikamtaka twende home (nikajua hii dalili ya kula kimaskhara kabisa) hajakataa nikiwa njiani akili ikaniambia home hapana, nikaingia hotel moja maeneo ya Mwenge, Nikamuuliza hapa utakuwa comfortable? Akasema ndiyo japo angependa home zaidi nikamwambia home itakuwa siku nyingine!

Tumeingia room, ghafla akanikumbatia anataka kiss,nikashtuka kidogo na kumtaka akae kwanza mara naona machozi yanamtoka, mood yote ikakata nikataka kujua kulikoni,ndo kunipa mkasa mzima huku akilia kwa maumivu anayopitia, jamaa alipoondoka na kumuacha akiwa mjamzito hakuwahi kumtafuta tena, na hata alipoenda kwenye ofisi alizomuaminisha na kwake aliambiwa jamaa alikuwa kibarua na aliondoka bila taarifa, hawajui alipo!

Binti analea mtoto peke yake, na biashara yake ilikufa kwa miaka 2 na sasa ndo ameanza japo kwa kujikongoja tu, akaniambia ...jamaa yake pia kumbe alikuwa amempa mimba msichana mwingine alipokuwa akifanya kibarua(catering), na huko mkoani amezalisha binti wawili...amebaini hayo alipokuwa akifuatilia jamaa amsaidie malezi ya mtoto!

Baada ya kusimulia yote sikutaka tena kula kimashkara, nikamwambia namrudisha kwanza then tutapanga siku nyingine ya kuongea kwa kirefu, ghafla kanikumbia anataka tusex (huku machozi yakimtoka na vikwikwi muda wote, nafsi yangu ikagoma kabisa, nikampatia 50k, ya kuboost siku!

Akanitaka walau tufanye kidogo nikakataa kabisa kwa sababu nafsi yangu haikuwa tayari...tukatoka, nikamrudisha mabibo, nikageuza zangu!
Nimewaza mbali sana, wakati fulani wanawake wanatengeneza taswira fulani kuubwa vichwani mwao, na kutamani mambo makubwa mwisho wa siku wanaangukia mashimoni, usimdharau MTU kwa kumkadiria, huwezi kujua kesho yako, na kama haumpendi MTU sio lazima umtukane na kumpayukia, kuna namna unaweza kumwambia akakuelewa tu!
 
Nimekunbuka Neema , wangu miaka ya late 90, alishawahi nitamkia , "t blj, .. nakusaidia tu penzi hili kwa kuwa we ni jirani yangu, lakini huna hadhi wala pesa ya kuwa na mimi" wakati huo mi ndo nishapemda haswa ., she was cute kwa kweli na zigo la kutosha , that day ,I felt,, emmotional, mentaly beaten down, and physically not up to par . Nikaamua tu kinyonge ngoja niwaachie hao wenye nguvu zao waendelee naye .

Nimekuja kukutana na huyu dada mwaka jana nikiwa katika mishe zangu huko biharamuro , asee maisha hayatabiriki , ana watoto watatu baba tofauti na mmoja mlemavu wote analea peke yake .
 
Nimekunbuka Neema , wangu miaka ya late 90, alishawahi nitamkia , "t blj, .. nakusaidia tu penzi hili kwa kuwa we ni jirani yangu, lakini huna hadhi wala pesa ya kuwa na mimi" wakati huo mi ndo nishapemda haswa . I felt,, emmotional, mentaly beaten down, and physically not up to par . Nikaamua tu kinyonge ngoja niwaachie hao wenye nguvu zao waendelee naye .

Nimekuja kukutana na huyu dada mwaka jana nikiwa katika mishe zangu huko biharamuro , asee maisha hayatabiriki , ana watoto watatu baba tofauti na mmoja mlemavu wote analea peke yake .
Umsaidie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom