Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,119
- 1,569
Isa 53:7 SUV
[7] Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Yesu alipita katika mateso mengi yasiyo ya haki, alitendewa mambo mabaya isivyo halali, jambo ambalo halikuwa jepesi hata kidogo.
Kinachoshangaza katika mateso yake ya kuonewa, hamkumjibu mtu kwa hasira, wala hakuwa na kisasi na wale waliomtesa, alichugua kuwa mnyenyekevu. Hii inaonyesha vile alikuwa mtii na alivyojitoa kwa ajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu.
Yesu alibeba mateso mengi kimya kimya, hakulaumu au hakulalamikia juu ya hali yake aliyokuwa anapitia, wala hakuwa na muda wa kujitetea. Inaonyesha vile alikuwa mvumilivu na alikubali kupitia hali hiyo kuleta ukombozi kwa mwanadamu.
Yesu alijitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi za wanadamu, alifanyika mkosa ili kutuletea ukombozi kwa damu yake.
Kutolewa mfano wa kondoo, kondoo anapokatwa manyoya huwa katika ukimya, hii inaonyesha wazi utulivu wa Yesu na alivyojitoa pasipo kuwa na malalamiko.
Hii itusaidie kuelewa vile Yesu alijitoa kwetu kutupatanisha na baba yetu wa mbinguni, amelipa gharama kubwa kwa ajili yetu sisi, huna sababu kuendelea kuishi maisha ya dhambi, tubu leo ujipatanishe na Mungu wako.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana