Alipa Kisasi Kwa Kumnyang'anya Bwana Mama Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alipa Kisasi Kwa Kumnyang'anya Bwana Mama Yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 10, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Alipa Kisasi Kwa Kumnyang'anya Bwana Mama Yake


  Tuesday, November 10, 2009 3:20 AM
  Mama mmoja nchini Uingereza ambaye alimwacha mtoto wake kwenye nyumba ya kulelea yatima miaka 22 iliyopita, amebaki akisaga meno baada ya binti yake huyo kulipiza kisasi kwa kumnyang'anya mume wake.
  Elizabeth Murray mwenye umri wa miaka 46, amebaki akilia akisaga meno kwa huzuni baada ya binti yake aliyemkaribisha nyumbani kwake baada ya kumwacha kwenye nyumba ya kulelea yatima miaka 22 iliyopita, kutoroka na baba yake wa kambo.

  Mwaka 1987 Elizabeth alimpeleka mtoto wake wa kike Melissa Anderson kwenye nyumba ya kulelea yatima wakati huo Melissa akiwa na umri wa miaka 3.

  Miezi michache baadae Elizabeth alianza uhusiano wa kimapenzi na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la John na haikupita miaka mingi alizaa naye watoto watatu wa kike ambao hivi sasa wana umri wa miaka 18, 16 na 14.

  Hatimaye mwaka 2006, Elizabeth na John waliamua kuoana na kuvalishana pingu za maisha.

  Ikiwa imepita miaka 22 tangia alipomuacha binti yake kwenye nyumba ya kulelea yatima, Elizabeth aliamua kumchukua Melissa na kuishi nae pamoja na John na watoto wao wengine watatu.

  Haukupita muda mrefu, Melissa na John walianza uhusiano wa siri wa kimapenzi.

  Siku moja Elizabeth aligundua ujumbe wa simu wa kimapenzi toka kwa binti yake kwenda kwa John na alipombana John kama anatembea na mtoto wake wa kambo, John na Melissa walihama nyumba na kwenda kuishi pamoja.

  Elizabeth amebaki nyumbani kwake akilea watoto wake watatu na ameamua kuvunja uhusiano wake na John kwa kufungua kesi ya madai ya talaka.
   
Loading...