Alinikataa sasa ananihitaji

Alinikataa sasa ananihitaji

kwetumasoko

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
866
Reaction score
517
Wakuu wana forum hii,

Habarini za leo,

Kuna msichana mmoja nilimpenda sana na ni muda mrefu nilikuwa nikimfuatillia ili tuwe wapenzi na hatimaye tuoane ili tujenge familia lakini cha ajabu aliniambia kuwa yeye ana mpenzi na kamwe hawezi kumwacha kwa sababu ndiye atakayemuoa na anampenda sana. Nikaona isiwe shida nami nikawa nimekata tamaa.

Sasa ni miaka minne imepita, naona anaanza kunifuatilia na kujaribu kuwa karibu nami, ingawa mpaka sasa bado sijaoa.

Naombeni ushauri juu ya huyu binti!
 
labla mambo magumu huko anaamua ajirudi mdogo mdogo
 
Kama roho yako ipo kwake na uko single why not,huenda ndio wakati wako sasa wakufanya maamuzi..
 
Sikiliza sauti ya ndani yako inakwambia nn maana hiyo ndiyo kweli yenyewe.
 
Msaidie mwenzio, kufikisha 30years bila mupenzi ni mtihani wa la nne.
 
Hapa utashauriwa mpaka na watoto wa chini ya miaka 18. Hapo mtaani kwenu hakuna watu wenye hekima?
 
Angalia kwanza kama huko alikotoka hawajatengua urithi (0713)...
Never test the depth of a river by both feet
 
Sasa mimi sielewi kilichomkuta huku wakati alisema anampenda na ndiye wake
Jamani si mulize kulikoni kama unataka kujua,au kwani mtu akisema nakupenda ndio mkimalizana hamtafuti ustarabu mwengine? sikia unaweza kutolewa Mahari na usiolewe sasa sioni ajabu kwa huyo walikua wanatoana Stress...
 
Back
Top Bottom