Alikiba zingatia malalamiko ya mashabiki wako

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Saleh Kiba al maarufu kama Alikiba ni miongoni mwa wasanii wakongwe na wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na pengine Afrika
kwa ujumla. Ni mshindi wa tuzo zaidi ya 14 kwa mwaka 2016 ikiwezo tunzo kubwa kabisa za MTV EMA kwa kipengele cha Best African Act.

IMG_20170130_090622.JPG


Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata mwaka jana ikiwemo kupata mkataba mnono wa kampuni kubwa ya muziki duniani yaani Sony
Music na kushinda tuzo zote hizo ndani ya mwaka 2016 ni wazi kabisa kuwa thamani ya Alikiba imepanda maradufu barani Afrika na pengine kila mfuatiliaji wa muziki Afrika angependa zaidi kumfahamu Alikiba, kufahamu
kazi zake, ni wapi ametoka na wapi anakwenda.

Sekeseke lilitokea mwaka jana kwenye show ya Mombasa rocks iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya kati ya Wizkid na Alikiba ni moja kati ya
mambo ambayo yalifanya jina la Alikiba lizungumzwe sana barani Afrika haswa Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo mitandao mbalimbali ya Nigeria iliripoti kuwa Alikiba anatrend sana nchini Nigeria.

Ushindi wa MTV EMA pia ambao awali alipewa Wizkid kabla haujatenguliwa na kupewa Alikiba ni mambo yaliyofanya apate attention zaidi
kwenye soko la muziki barani Afrika. Kutrend ni kitu muhimu sana katika soko la muziki kwa sasa, wasanii wengi duniani kote hata mpaka Marekani wamekuwa wakitengeneza kiki kabla ya kuachia kazi zao mpya ili kupata
attention.

Nafahamu kuwa msanii Alikiba amekuwa sio muumini mzuri sana wa kiki, lakini kiki kama hizi ambazo zinajitengeneza zenyewe
ni dhambi kubwa kuacha kuzitumia kibiashara sababu kuna wanaotamani kutrend hata kwa kutembea uchi lakini hawazipati.

Mapema mwaka huu Alikiba alitangaza ratiba ya World Tour yake itakayoanzia South Africa kisha America na kumalizikia barani Ulaya. Kwa
mujibu wa ratiba kutoka kwenye posters zake alizozipost Instagram Tour yake inaanza February mwaka huu.

Hivyo mpaka ninaandika makala hii zimebaki siku tatu kufikia mwezi February. Kati ya sehemu ngumu sana kupenya kimuziki
barani basi ni Afrika Kusini na hii imetokana na ‘wasauzi’ kuthamini sana muziki wao na haikushangaza licha ya jina kubwa alilojijengea
Diamond Platnumz kwenye kiwanda cha muziki barani Africa aliwahi kaririwa akisema amefanya collaboration na AKA ili kupenyeza muziki wake África Kusini.

Sasa wasiwasi wangu ni je? Alikiba anategemea kujaza viti kwa kuitegemea nyimbo ya Aje pekee? Target yake kwenye hii tour ni kuifanya
iwe ya kidunia au analenga waTanzania pekee wanaoishi kwenye nchi husika? Aliahidi atatoa Aje remix ambayo ni nyimbo aliyoimba na msanii
kutoka Nigeria MI Abaga lakini mpaka zimebaki siku tatu kabla hatujaingia mwezi anaoanza tour hakuna dalili ya hiyo nyimbo?

Binafsi nilidhani ingekuwa sahihi sana kama angeachia nyimbo ambayo amesharekodi mama mkongwe Yvonne Chakachaka kwa lengo la
kuiteka zaidi South Africa kibiashara zaidi ili jina lake liwe kubwa nchini humo hata wakati wa Tour yake angetumia pia na fursa hiyo kufanya
media tour kuitambulisha zaidi hiyo ngoma.

Nadhani si Mimi ila asilimia 98 ya mashabiki hawaridhishwi na namna ambayo Alikiba amekuwa slow sana na kutojua namna soko la
mUziki linavyoenda na nini linataka. Ni jana kupitia mtandao wa instagram msanii wa maigizo ambaye pia ni shabiki mkubwa wa msanii Alikiba alipost kipande cha screenshot kikionesha ujumbe aliotumiwa na shabiki mwingine wa Alikiba DM kuwa Ali atapoteza mashabiki wake sababu hawapi raha wanayoitaka, siku zote amekuwa mtu wa kujiamini na kuwasibirisha mashabiki wake ambao ukweli bila wao asingekua hapo halipo leo.

Mwaka mpya umeanza kwa kasi kweli kila mtu
yuko kasi lakini naona Alikiba bado yule yule.



SOURCE: BONGO5
 
Moja ya vitu ambavyo Alikiba anakosea ni kutokuwa na ratiba inayoeleweka.
Hapo hayuko serious kabisa
 
Ali Kiba ana wimbo mmoja tu unaompatia jina Afrika ... "Aje"

Ali Kiba anabebwa na mashabiki zake zaidi kuliko juhudi zake.. hapa ninamaanisha kuwa mashabiki zake wanajuhudi zaidi kuliko Ali Kiba mwenyewe

Yaani, kiukweli huo wimbo wa Aje umempatia sifa zilizopitiliza uzuri wa wimbo..!
 
Ali Kiba ana wimbo mmoja tu unaompatia jina Afrika ... "Aje"

Ali Kiba anabebwa na mashabiki zake zaidi kuliko juhudi zake.. hapa ninamaanisha kuwa mashabiki zake wanajuhudi zaidi kuliko Ali Kiba mwenyewe

Yaani, kiukweli huo wimbo wa Aje umempatia sifa zilizopitiliza uzuri wa wimbo..!
Swali ni je wimbo wa aje ulihit sauzi? Au anaenda kuwaimbia wabongo wanaishi sauzi
 
Ali Kiba bifu na Dai ndiyo linambeba kwa hiyo mashabiki wake wengi wao siyo wote ni wale wanaomchukia Dai ndo maana unaona wamen'gan'gana naye hayo mapungufu yote wanayaona wanajifanya kama hawaoni na wanashidwa kumwambia ukweli.
 
Sony hamuwajui vizuri nyie..unafikiri ukisaini Sony basi unaluwa na uhuru wa kutoa nyimbo unavyotaka?!Davido alikaa muda gani mpaka kaja kutoa nyimbo?!

Nyie subirini hapo mukitegemea maajabu
 
Kuna watu wanasauti nzuri tu, akishilikishwa ataimba vizuri, ila atoe nyimbo yake sasa.. Kwasisi tunaojua music arrangement unabaki unashangaa tu.
 
Ali Kiba ana wimbo mmoja tu unaompatia jina Afrika ... "Aje"

Ali Kiba anabebwa na mashabiki zake zaidi kuliko juhudi zake.. hapa ninamaanisha kuwa mashabiki zake wanajuhudi zaidi kuliko Ali Kiba mwenyewe

Yaani, kiukweli huo wimbo wa Aje umempatia sifa zilizopitiliza uzuri wa wimbo..!
True that,Ali kiba ana maneno mengi kuliko vitendo,though anajisifu he is best lakini ameshindwa ku-proove ubora wake upo api.Mwambieni aache maneno aweke muziki..!!The game has totally changed,anatakiwa a-focus kwenye branding sio blaaa blaaa
 
True that,Ali kiba ana maneno mengi kuliko vitendo,though anajisifu he is best lakini ameshindwa ku-proove ubora wake upo api.Mwambieni aache maneno aweke muziki..!!The game has totally changed,anatakiwa a-focus kwenye branding sio blaaa blaaa
ningependa huu ujumbe uwafikie wahusika..!
tanzania-king-majuto.png
 
Back
Top Bottom