Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,322
Kuna mdogo wangu aliingia kwenye mahusiano na bi dada mmoja ambae alikuwa "ameachika". Hakuchi Hakuchi mwisho kunakucha, Penzi lilikolea kiasi cha kuamua kuchukuana jumla. Bwana mdogo akiwa katika hatua za kujiandaa kuchukua jumla mwenzie akabadili Gia angani na kusema nimegairi. Japo iliuma aliinua mikono juu na kumshukuru yeye alie juu.
Bi dada huyu kila yanapomsonga MAGUMU humtafuta bwana mdogo kwa lengo la kushauriana na kupewa msaada inapobidi. Bwana mdogo amekaa na kuitafakari hali hii haipatii tafsiri.
Nimeiona niilete kwenu wana JF tuitafakari pamoja.