Alichokisema Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Ndg Polepole kwenye mkutano na wandishi

Mondoros

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
629
472
WhatsApp Image 2017-01-24 at 1.51.02 PM.jpeg

Leo Ndg Humphrey Polepole amezungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano, Lumumba. Amejikita zaidi katika kuelezea mwendelezo wa CCM kuimarika zaidi na kukubalika na wananchi zaidi huku upinzani ukiendelea kudhoofika kwa kasi kubwa zaidi.

Katika uchaguzi mdogo uliofanyika trh 22/10/2017 ambapo ulihusu jimbo moja la Dimani-Zanzibar na kata 20 Tanzania bara, katika viti vyote hivyo CCM imeshinda jimbo la Dimani na kata 19 kati ya kata zote 20.

Hii ni ishara tosha kuendelea kukubalika kwa Chama tawala huku wananchi wakiupuuza upinzani na porojo zao zote. Zifuatazo ni nukuu za Ndg H Polepole;

"Ndg wanahabari ni desturi yetu kuwashirikisha lolote pale ambapo tuna jambo ili wananchi wapate kupitia kwenu"

"Tunasema asante sana wananchi kwa kuendelea kuiamini CCM"

"Tulikua na chaguzi ndogo kwa nafasi za ubunge&udiwani, tulifanya kampeni nzuri zaidi ktk mambo ya maendeleo"

"Tuliendelea kuwaambia watu juu ya maswala na uelekeo wa Ccm na serikali yake kuijenga Tanzania"

"Licha na hujuma na kubeza sana kulikofanywa na vyama visivyo vya Ccm,bado wananchi mmetupa ushindi mkubwa Ccm"

"Kwa upande wa jimbo la Dimani tumeshinda kwa 78.74% dhidi ya vyama vingine, Ahsante Dimani"

"CUF imepata anguko kubwa sana Dimani hasa ukiangalia takwimu za 2015 na za 2016. Kwetu Ccm tumeinuka sana"

"CCM imeshinda kata 19 kati ya 20, Ahsanteni sana watanzania kwa imani hii kubwa"

"Shughuli za maendeleo tunazozifanya zitatupeleka katika uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2020"

"Siri ya ushindi huu ni MAGEUZI MAKUBWA YANAYOFANYIKA NDANI YA CCM kwa kauli moja"

"Watanzania tuendelee kuiunga Ccm wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kujerea ktk misingi yabkuasisiwa CCM"

"Siri nyingine ya ushindi ni KAZI NZURI YA RAIS WA JMT, amefanya kazi kubwa ya kutekeleza matakwa ya wananchi"

"Dhamira ya serikali ya kupiga vita RUSHWA, UFISADI, UBADHILIFU na kuwa na uwakilishi madhubuti"

"Tunaendelea kuikumbusha serikali iendelee kusimamia 10% ya mapato ya Serikali za Mitaa kwaajili ya vijana na wanawake"

"Viwanda vitakuja pale ambapo tutavilinda viwanda vya ndani kwa kutumia vyetu"

"Nchi iendelee inahitaji serikali inayojituma na tumeona serikali ikijitahidi zaidi na zaidi"

"Ccm na viongozi wote watenge muda kuwasikilza wananchi wao, hili tunalisisitiza sana"

"Kuelekea 2020 Ccm tunauona mwanga Mkubwa sana kupitia uchaguzi mdogo na kazi nzuri za serikali yetu"

"Mwisho, mwelekeo wetu ni Mageuzi makubwa katika Ccm ili kiweze kutenda ipasavyo"

"Mwaka huu ni wa Uchaguzi wa ndani basi wanachama tuwalipe wananchi kwa uongozi adilifu, wakujituma"

CCM kama chama chenye Dira na Dhamira ya kweli kuwatumikia watanzania tutaendelea kuhakikisha kuwa Chenyewe pamoja na Seikali yake itajikita katika kuwasikiliza nwananchi na kutatua kero zao kwa wakati na kwa haraka zaidi. Watanzania sasa waone sababu ya wao kujiunga na chama hiki pamoja na kukiunga mkono, CCM ni Chama bora zaidi kuwahi kutokea na hakuna chenye kukifikia kwa ubora, mfumo na taratibu za undeshaji.

[HASHTAG]#UVCCM[/HASHTAG]
 
Nina uhakika kabisa hata Polepole anajua kwamba hii mistari 4 ni porojo.

Natamani nipate nafasi ya kumuuliza kuhusu mil 50 kila kijiji.
 
Mijadala kama hii inawafanya baadhi ya wana CHADEMA wafe kwa pressure
aise kila saa kushnda humu jf ni mda gani unatumikia wananchi?ndyo mana hvyo vyenu kwnye rasimu ya warioba vilifutwa,hakuna cha maana mnalofanya zaidi kuwakandamiza upinzan
 
Hongera CCM kwa ushindi huo. Ushindi ni jambo la kufurahia na kuna kila sababu ya kufurahia ushindi huu.Hii ki ukweli ilikuwa pima joto na tumeona Watanzania wanataka nini.

Binafsi naamini katika upinzani imara ambao utafanya chama kilichokuwa madarakani kiwe na umakini lakini kwa ujumla asilimia kubwa ya Watanzania hawajawa tayari kujenga upinzani imara.

Kwa hivyo upinzani usiumie sana ila ikukbali kuwa Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko ya maana.

Hongera CCM na hongera Polepole.
 
Mbona hajasema KATA walizokuwa wanazitetea ni ngapi na walizoongeza ni ngapi...... Maana kama ni mpira basi ni bilabila..... Tena wao ndo wametia aibu kbs.... Polic wao, tume yao kila kitu chao.....
 
Back
Top Bottom