Alichokionya Mwl.Nyerere kuhusu"Utii"kinaelekea kulipasua Taifa

ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,055
4,243
IMG-20160622-WA0031.jpg



Ili kuleta ufanisi katika utendaji,suala la uwajibikaji wa pamoja ni moja ya jambo la msingi ambalo halinabudi kufuatwa.Tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya tano,Taifa limekuwa likishuhudia aina mpya ya uongozi,uongozi usiohitaji wala kupokea ushauri juu ya mambo yahusuyo Taifa letu.

Badala ya serikali kutumia vyombo vyake katika kuongoza nchi,sasa mihimili yote ya dola imeacha wajibu wao wa msingi badala yake inasubiri maelekezo ya nini cha kufanya toka kwa mkuu wa nchi.

Siku chache zilizipota,tulisikia kile kilichoitwa "mamlaka ya juu ya chama na serikali ya ccm" wakiwapiga marufuku wabunge watokanao na chama chao kutofautiana na hoja za serikali.Kwamba kwa kuwa wao ni wa CCM,hawaruhusiwi kuhoji chochote katika yale yaletwayo bungeni.Hili ni jambo la kusikitisha na halitoi picha nzuri kwa afya ya Taifa letu.Kwamba mbunge wa ccm hata kama serikali inafanya madudu kiasi gani,hapaswi kuikosoa kwa namna yoyote kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kuupoteza ubunge wake.

Kama serikali haitaki ukosoaji wa aina yoyote toka kwa wanaCCM,kulikuwa na sababu gani ya chama kuwa na wabunge zaidi ya 200 bungeni wakati wabunge hao hawaruhusiwi kuhoji chochote kilichotofauti na maslahi ya chama na serikali?

Kuwazuia watu kutofautiana kimawazo,ni kuwafanya watu wazipe likizo taaluma zao na fikra zao.Kuruhusu mijadala mipana bungeni hupelekea kupatikana kwa majibu ya changamoto zinazolikabili Taifa,unapowazuia na kuwanyima watu fursa ya kutoa mawazo tofauti juu ya hoja za serikali,unamaanisha kuwa huhitaji mijadala katika maamuzi ya serikali,kama maamuzi ya serikali hayapaswi kuhojiwa,yanapelekwa bungeni kufanya nini?Kwa nini yasianze utekelezaji mara moja badala ya kuyapeleka bungeni na bunge kupoteza Rasilimali muda na fedha kujadiri mambo ambayo hawaruhusiwi kutofautiana hayo?

Kuuminya uhuru wa fikra yaweza kuwa dalili ya Mwisho ya udikteta wa kimfumo.Kama serikali haitaki kuhojiwa juu ya yale iliyoyaamua,hatuna jina jingine tunaloweza kulipa serikali hiyo zaidi ya jina la serikali ya kidikteta.

Kitendo cha serikali kuzuia mijadala huru ya wawakilishi wa ccm kitapelekea wawakilishi hao kuogopa kuikosoa serikali,badala yake wataanza kujipendekeza kwa kuisifu kinafiki hata katika yale ambayo dhamiri zao zinayaona wazi kuwa si sahihi.

Kuiruhusu hali hii,ni kuua kabisa uwezo wa kufikiri wa watu wetu,watu watalazimika kuweka kando Taaluma zao na kujiunga katika kundi la kuisifu na kuiabudu serikali kwa maana kuikosoa serikali kunaweza kuwa kosa la jinai liwezalo kukugharimu nafasi yako.

Ili kujenga Uhuru wa kifikra,Hayati Baba wa taifa alionya tabia ya watu kuwa na utii wa kijinga,utii unaozuia watu kuhoji mustakabali wa Taifa lao.Wakati viongozi wetu wakijinasibu kuwa wanamuenzi Baba wa Taifa hili,tunawaomba wajipe nafasi ya kupitia baadhi ya maneno na nukuu zake ili wajifunze toka kwake.Kama Mwalimu aliona madhara ya Watanzania kuwa "kondoo" kwa kukubali kuswagwa bila kuhoji,kwa nini leo hii watu hawa wanaojinasibu kumuenzi Mwl.hawataki kuwapa watu Uhuru wa kujadili mustakabali wa Taifa lao?

Ni jambo la hatari kuikabidhi nchi hii mikononi mwa mtu mmoja na wengine wote wakakaa kusubiri maelekezo ya nini cha kufanya toka kwake mithiri ya waumini wamsikilizavyo kiongozi wao katika nyumba za ibada.Serikali ni mkusanyiko wa vyombo na Taasisi mbalimbali,kuvizuia "vyombo viundavyo Serikali" kutumia weledi wa kuundwa kwake,ni kuvifanya vyombo hivyo viache kazi yake ya msingi ya kuisimamia serikali na kuvifanya vijigeuzi kuwa washangiliaji wa matamko ya serikali.

Ili kuleta ufanisi na uwajibikaji wa pamoja,serikali inapaswa kuvipa Uhuru vyombo vyake ili viweze kutumia Taaluma zake na uwepo wake katika kuisaidia serikali yetu kuyafikia Maendeleo tunayoyahitaji.Vinginevyo vitaishia kuitikia pambio za sifa jambo ambalo haliwezi kuwa na tija kwa Maendeleo ya Taifa letu.
 
Back
Top Bottom