MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,181
- 5,429
Hakika ukiingia ktk siasa ujue unalo, ujue hata familia yako iko hatarini, ujue utaishi kama wanyama pori waliwao mwituni.
Upinzani Tanzania wameleta chachu ya hali ya juu nchini ndani na nje ya bunge. Hoja zao zenye tija zimepelekea hadi leo bunge lisioneshwe mubashara kwa hofu tu watapata kiki kwa raia.
Watu wengi wanajua hawa wapinzani ndiyo waanzilishi wa mabadiliko bungeni la hasha. Yupo mtu ndani ya ccm aliwahi fanya jambo ambalo hadi leo halijavunjwa bungeni.
Huyu si mwingine ni mh. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya a.k.a Ilombwe.Alijiita jina hilo la utani kwa kuwa hilo ni jiwe linalotumika kupasulia mawe mengine yaani ni gumu hakuna mfano. Kwanini nimemtaja huyu na si mwingine?.
Huyu jamaa akiwa mbunge ndani ya ccm alishuhudia ufisadi wa kufa mtu ukifanywa na mawaziri kwa manufaa yao na hakuna mbunge aliyehoji hayo kwa hofu ya ama kuuawa au kufukuzwa chama au kutopitishwa jina wakati wa kugombea ubunge.

Wakati huo waziri wa viwanda na biashara alikuwa Mh. Idd simba.Kulikuwa na uhaba wa sukari nchini yy waziri alipitisha vibali vya kuingiza sukari nchini kwa wafanyabiashara wachache ambao yeye alikuwa na maslahi kwao wengine walinyimwa. Ikumbukwe huyo waziri pia alijimilikisha UDA kinyemela.
Mh. Mzindakaya akaonya kwenye vikao vya ndani akapuuzwa. Alichokifanya alienda bungeni akalipua mbele ya bunge na kudai tume iundwe haraka kuchunguza maana wabunge wengi ndani ya ccm walimsakama wakidai ni muongo na mzushi.
Zaidi walimtaka aache ili suala hilo limalizwe ndani ya vikao vya chama naye akagoma. Wengine walienda mbali zaidi kumtishia hata kufa lakini akasema atasimamia ukweli wao wakafanye yao yeye yuko tayari kwa lolote.
Iliundwa tume na bado ndani ya misukosuko hiyo alitekwa na watu walioonekana majambazi naye akawawahi kawaua wote eneo la senjele mkoani mbeya. Ajabu kesi ya kuwaua hao majambazi ikapamba moto ili afungwe kumbe waathirika wa suala alilosimamia walikuwa nyuma.
Mwisho wa siku tume ikahitimisha waziri akabainika fisadi na akatemeshwa uwaziri na hakutengamaa kiuchumi hadi kesho.
Leo kuoneana aibu ndani ya ccm kumetufikisha hapa tulipo. Hatuna watu sampuli ya Mh. Mzindakaya bungeni ndani ya ccm wengi waoga ukimuona kapiga kelele jua kafikwa. Anayenitutumua basi anauza hoja kwa wapinzani. Wengi wameishia kulialia tu.
Mh. Nape ameonekana jasiri leo baada ya kufikwa yeye lakini jana walipofikwa wa mtaa wa saba alishangilia na kutoa kebehi na dharau. Laiti angesimama kama Ilombwe angekuwa maarufu kuliko alivyo Lema, Sugu, Lisu, Mbowe ama Kafulila au Zito.
Nachukua nafasi hii kukupongeza Mh. mzindakaya kwa kusimamia ukweli japo kuna mapungufu yako ukiwa mbunge ila kwa hili moja tu lililohatarisha maisha yako hakika bado halijavunjwa na mtu ndani ya viunga vya bunge letu tukufu.
Nashauri wabunge muache unafiki muuseme ukweli bila kujali ni mwanachama mwenzangu au ni bosi wangu vyovyote iwavyo mtaiokoa hii nchi. Leo mkuu wa nchi kachemka kwa bashite.