Alianza Ahmed Abiy. Hawa nao Wameona Manufaa ya Umoja wa Taifa Lao. Sisi Tumeona Nini Kwenda Wanakotoka?

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Lugha isiwe hoja ya kutoelewa ujumbe uliowasilishwa.

"uhasimu na uadui wa kisiasa kati yangu na ndugu yangu mkubwa Raila umekwisha leo.
Mimi ndio kijana mkubwa wa Baba yetu Raila Odinga, na hapa mimi niko nyumbani" - Ruto alisema.

Ruto akaendelea:
" Vile Prime Minister amesema, leo tumefika hapa na tumekubaliana ya kuwa ile uhasama ya zamani tumezika...tunaanza ukurasa mpya ya kuunganisha wakenya."

" Mkiona Uhuru na Prime Minister Tinga mwenyewe ako hapa na uone 'hustler' pia ako kati yao, mjue mambo iko sawa. Sisi wote tutatembea safari moja ya kuunganisha wakenya."

Kuisoma habari hiyo: https://www.the-star.co.ke/news/201...nt-with-ruto-ahead-of-Uhuru-arrival-in-kisumu


Ruto aliyasema hayo Dec. 13 2018, katika ziara anayoifanya Rais Uhuru Kenyatta Kisumu.

Sote tunataka maendeleo ya nchi yetu, lakini kama maendeleo mpaka yaje ni lazima tufarakane hayo maendeleo yatakuwa na kasoro kubwa. Kwanza sidhani kuwa maendeleo yatakuwepo.
 
"Sote tunataka maendeleo ya nchi yetu, lakini kama maendeleo mpaka yaje ni lazima tufarakane hayo maendeleo yatakuwa na kasoro kubwa. Kwanza sidhani kuwa maendeleo yatakuwepo."
 
Back
Top Bottom