"Ali Obeid Mengash" mkulima aliyeidondosha "Apache" helikopta kwa gobole

Juma Wage

Member
Sep 8, 2023
60
201
Majasusi waliokuwa wakitazama taarifa ya Habari katika chumba cha Hoteli, waligonganisha glasi na kushangilia "Ndiyo" alisema mmoja wao.

"Alifanya hivyo!" "Alifanya hivyo!" walikuwa wakimtazama shujaa wa siku hiyo.

Mkulima mzee mkazi wa Karbala aliyeiangusha helikopta ya kimarekani aina ya "Apache" kwa kutumia bunduki yake ya kuwindia kwale.

ilikuwa ni kama vile Matangazo ya CNN yanapoanza kuonesha matukio yaliyojiri Iraq.

Runinga ya Taifa ya Iraq ilipambwa kwa maandishi meupe yaliyozunguka skrini nyeusi "VITA YA HESABU YA MWISHO."

Habari ya siku hiyo kutoka eneo la vita, ilianza kwa picha ya helikopta ya kisasa iliyoanguka huku mziki wa epic kama "background" ukihanikiza masikio kutamani muendelezo wake na sauti ikisema "Ifuatayo ni mifano zaidi ya mambo machungu yaliyovunwa na wavamizi wa Amerika ambayo tunakuletea bila kuhaririwa, ni hadithi ya shujaa wa Iraq."

Watazamaji waliona helikopta iliyoanguka ikiwa na mizinga ya Makombora ya moto, helmeti mbili na ngao 1 ya "Calvary."

ALI OBEID MENGASH, Mkulima aliyevalia kanzu ndefu ya kijivu na kilemba chenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na nyeupe, alikuwa akihojiwa na ripota wa Iraq aliyevalia Sare za kijeshi.

"Mimi na ndugu zangu tuliipiga risasi ilipokuwa juu" alieleza.

Mtangazaji huyo alidhihaki "Wamarekani waliitangazia dunia kwamba Apache ilikuwa na teknolojia ya kisasa isiyoruhusu risasi kupenya lakini shujaa ameiangusha kwa gobole la kuwindia kwale."

Taarifa za Marubani waliokuwa wakiendesha helikopta hiyo hazikutajwa kwa wakati huo, japo walizionesha kwa wakati Mwingine.

Ndimi Juma Wage
Dodoma.

IMG-20230919-WA0002.jpg
 
Kwanza huyo mkulima hajashika gobole hapo hiyo ni derivative ya AK-47.
Pili Apache si rahisi kudondoshwa na risasi za rifle, medium machine gun yenyewe ni vigumu.
Helicopter iko vulnerable kwenye rotors kuliko sehemu nyingine sababu ziko na reinforcement ya armour. Sasa rotors za Apache zinahimili 20mm round.
Hata vita ya Ukraine hii gunships hazidondoshwi na risasi za rifles bali MANPADS
 
Hii habari ilikuwepo kipindi Cha Vita vya Iraq, marekani wakawa na kazi ya kukanusha kwamba haikutunguliwa kwa AK 47,Kama ulikua timamu na mfuatiliaji wa habari za Vita hiyo kipindi hicho 2003
Hutokea kama coincidence wakati Mwingine.

Unaweza Kuta rubani alifungua kioo then Bw. Mengash akabahatisha kumtumgua rubani na kupelekea helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.
 
Hutokea kama coincidence wakati Mwingine.

Unaweza Kuta rubani alifungua kioo then Bw. Mengash akabahatisha kumtumgua rubani na kupelekea helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.

Kikubwa ni kwamba helikopta ya Mashambulizi isiyopitisha risasi iliangushwa kwa risasi.
 
Back
Top Bottom