Ukitaka kuwaweka kila mtu kwenye historia y ukombozi wa africa basi utaweka adi wanajeshi maafisa police na wanausalama wa taifa ambao wamefanya mengi.kikubwa historia itawasema kwa wakati wao watakopitajika kama hapa nyerer kapewa meza basi ndio lazima tumjue mhusika.lakini huwezi weka wote.tutavuruga maana nzima ..
Troojan,
Linawekwa jina la yeyote yule aliyehusika katika historia ya uhuru wa nchi yetu iwe awavyo.
Ali Msham hakutoa meza peke yake.
Ali Msham aliunga mkono harakati za uhuru kwa kufungua tawi la kwanza la TANU nyumbani
kwake Magomeni Mapipa.
Akiuza kadi na fedha akipeleka mwenyewe kwa
Iddi Faizi Mafongo aliyekuwa Mweka Hazina
wa TANU New Street.
Hapana ubaya kuihifadhi historia hii.
Maofisa wa polisi waliosaidia TANU walikuwapo mmoja wapo alikuwa
Hamza Aziz wakati ule
ofisa wa ngazi ya chini katika Jeshi la Polisi la Waingereza.
Hamza ni mdogo wake
Dossa Aziz.
Huyu TANU walimtumia sana kupata mikakati ya Waingereza kuihujumu TANU.
Alikuwapo
Amri Kweyamba na
Kitwana Kondo katika Special Branch.
Huyu
Amri Kweyamba aliwashughulisha sana wana TANU.
Mara kadhaa alivamia nyumba ya
Ally Sykes Mtaa wa Kipata kutafuta makaratasi ya ''uchochezi,''
ambayo
Ally akiyasambaza kuanzia Dar es Salaam, Morogoro nemda hadi mwisho wa reli Kigoma
na Mwanza.y of
Mimi nimeandika historia hii katika kitabu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes,'' (1998) na
haijavuruga chochote katika historia ya Tanganyika bali imeleta changamoto kubwa kwa wanahistoria
si wa Tanzania tu bali ulimwengu mzima.
Leo kitabu hiki kinasomeshwa kote wanakosomesha, African History na kipo Library of Congress,
Washington.