Nampenda sana Ali Saleh Kiba kutokana na mziki wake mzuri,sauti yake na hasa utunzi wake makini katika tungo zake mbalimbali mfano mzuri ni huu wimbo wake wa mwana unaotamba kwa sasa.
Video yake aliyoiachia jana ni nzuri sana,nimeipenda.
Ushauri wangu kwa Kiba,yeye ni msanii mkubwa sana,anatakiwa abadilike afanye mambo makubwa kama lilivyo jina lake.Asifanye mziki kwa mazoea kisa ana kipaji kikubwa.Aijue thamani yake sasa maana nakumbuka aliwahi kusema kua amekua surprised kwa mashabiki wake kumuulizia hadi walitaka kufanya maandamano japo alikaa kimya kwa zaidi ya miaka miwili!
Pia Kiba fans wenzangu huu ndio wakati wa kumsapoti Kiba,yeye kaonesha juhudi na sisi hatuna budi kumsapoti katika mziki wake ili naye apate mafanikio kulingana na kipaji chake kikubwa ambacho kiukweli hakiendani na mafanikio yake kimuziki.
Hahaaaaa,si unajua ukikaa karibu na uaridi nawe lazima unukie?
Ndo hivi sasa na mie nanukia....lol
Unakaribishwa pia kutoa mawazo yako,ila napenda kuuliza Dangote yule tajiri wa Naija au yupi?Hapa DANGOTE ndo hariiiii
Unakaribishwa pia kutoa mawazo yako,ila napenda kuuliza Dangote yule tajiri wa Naija au yupi?
Mhhh,hapo kwenye PM....sielewi hivi?
Haya bwana. 😕😕
Sielewi ni roho kwatuuuuu yaani kwa siku naangalia Mara 6 huu wimbo ni mauno madancer ni shegedeehh sipati picha kweli ujana giza na nuru
Umenikumbusha ngoja niende na mimi maana leo nimeshaangalia mara 5 tu.
Basi sasa sijui lipi ni lipi!!Mmmnh! Si ingeondolewa kwenye youtube kwanza? Ngoja tuone, tutajua tu!
Ova
Mtoa mada try to help me understand,nimeona kwenye blog fulani ya Mange anasema USA video ya mwana haina imekuwa blocked kwa issue za copyright,hii imekaaje??