Alfred Tibaigana: Asiyemtaka Rais Magufuli Imekula Kwake.

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
14.jpg

Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana amesema mwaka jana Watanzania wengi nchini kote walikuwa wakimuomba Mungu kila mmoja kwa dini yake ili waweze kupata rais mzalendo, makini na mtu mwenye kutanguliza mbele kabisa maslahi ya Umma na kumpata.

Napenda rais ajae awe mkali kidogo ili kuondoa hizi Kasoro zinazosababisha baadhi ya watu "kujifanyia mambo watakavyo kama vile hakuna serikali" alinukuliwa na moja kati ya vyombo vya habari mwaka jana, wakati akitoa maoni yake , nani anafaa kuwa rais wa awamu ya Tano.

Hata hivyo kamwe, Tibaigana hakuwa mtanzania peke yake aliyekuwa na mawazo na matakwa hayo, badala yake huo ndiyo ulikuwa msimamo na mahitaji ya idadi kubwa ya Watanzania, wakiwamo viongozi waandamizi wa kidini, serikali yenyewe, wanasiasa na makundi mbalimbali ya kiserikali. Katika orodha hiyo yumo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Musa Assad ambaye kwa upande wake naye alitoa kauli inayofanana na hiyo mapema mwaka huu kwa kusema "Kilichokuwa kinahitajika kwa nchi hii ilikuwa ni kupata "tone" ya kiongozi ili watendaji serikalini na hasa wa ngazi za juu washtuke na kuona kumbe serikali ipo"
Kama kwamba hiyo haitoshi , hata taasisi za fedha za kimataifa mpaka viongozi wakiwemo wa mataifa makubwa kabisa duniani kila mmoja kwa namna yake, wamekiri waziwazi umakini na utendaji wa kazi wa kiongozi huyo wa sasa wa nchi hii. Miongoni mwa taasisi hizo na mataifa hayo ni pamoja na:
1. Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika(ADB) alitoa kauli ya kumuunga mkono Magufuli wakati akitoa mamilioni ya fedha katika Ikulu ya Chamwino kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya Mendeleo inayosimamiwa na Serikali.
2. Serikali ya Korea Kusini wakati ikitoa jumla ya shilingi bilioni 650 ili kugaramia miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, nishati na kilimo.
3. Serikali ya Marekani kwa kupitia shirika lake la (USAID) imetoa kiasi cha shilingi bilioni 895 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo ambayo ni pamoja na kilimo, afya, umeme na utawala bora kwa kipindi cha kuanzia mwaka huu hadi 2020.

Kutokana na hali hiyo , Tibaigana na Watanzania wengine wenye nia njema na nchi yao ndipo wanaposema kuwa asiyempenda Dk. John Pombe Magufuli kutokana na kazi yake nzuri katika ujenzi wa taifa, kudhibiti ubadhilifu wa fedha na mali za Umma, uzembe kazini, ufisadi na kadhalika sasa "IMEKULA KWAO"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom