GE2025 Alex Duma ajitosha Udiwani kata ya Kihesa

GE2025 Alex Duma ajitosha Udiwani kata ya Kihesa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
Mwenyekiti wa umoja wa maafisa usafirishaji (BodaBoda)kanda ya kihesa Ndugu ALEX ELIAS DUMA amejitosa kusaka udiwani kata ya Kihesa manispaa ya Iringa

Alex Duma anakoleza joto la uchaguzi katika kata hiyo ambayo diwani anaye maliza muda wake na aliyekuwa naibu meya July Sawani nae anatetea kiti hicho

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Alex amesema kuwa kata ya kihesa inahitaji maendeleo zaidi na kuwafikia wananchi kwa ukaribu ili kushiriki nao katika utatuzi wa changamoto zilizopo na kuyafikia maendeleo imara kwa pamoja.

Hata hivyo Alex Duma Mwenyekiti wa umoja wa maafisa usafirishaji (BodaBoda)kanda ya kihesa anagombea nafasi hiyo na kuongeza idadi ya vijana wanaotaka kuingia katika ngazi mbalimbali za maamuzi ambapo Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM taifa Comrade Mohamed Kawaida katika nyakati tofauti walinukuliwa wakihamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huu kwa kugombea au kupiga kura.
1751450964246.jpeg
 
Back
Top Bottom