Jana pale Landmark Mh Mbowe alizindua album ya nyimbo zilizotungwa na kuimbwa na Lilian Wsira yenye nyimbo sita. Nyimbo hizo zinahamasisha Watanzania wajiunge na harakati za ukombozi, kwamba CCM muda wake wa kuaga umefika, akina mama waamke sasa wakomboe taifa nk. Nilinunua album yangu na kwa kweli nyimbo hizo zinahamasisha sana na watu wengi ukumbini walifurahi sana. Nadhani pale aliuza si chini ya milioni 8. Aliahidi kupeleka ujumbe wa ukombozi Tz nzima. Kama unataka nakala yake nenda duka la Chadema Makao Makuu au wasiliana nadhani namba yake ni 0719 604156. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeees Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr