Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,348
- 23,757
Ndugu zangu Watanzania,
Hiyo ni Kauli ya Mamlaka iliyotolewa Na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Albert Chalamila kuwaasa wale wote watakao kufanya kujitoa akili au kujizima Data na kutaka kuleta vurugu siku ya uchaguzi.
Amesema ya kuwa watashughulikiwa kimyakimya na vyombo vya Dola.
Nami Mwashambwa Lucas nasema ya kuwa watakao jaribu kushiriki ujinga huo washughulikiwe kisawasawa mpaka akili iwakae sawa na wajute kuzaliwa Kwao. Linapokuja suala la kulinda amani na usalama wa Taifa letu ni lazima tuwe wakali na tusicheke na Nyani tukavuna Mabua.
Soma hapo chini 👎
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewatoa hofu wananchi wa jiji hilo kuhusu usalama katika siku ya kupiga kura ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa hakuna atakayepata madhara kwa kushiriki katika zoezi hilo la kikatiba.
Akizungumza Oktoba 17, 2025 jijini Dar es Salaam katika kikao na makundi maalumu ikiwemo mama lishe, baba lishe, machinga, vijana na wadau mbalimbali, Chalamila amesema mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya wapiga kura milioni 4,420,912 waliojiandikisha, na wote watapiga kura kwa amani na utulivu.
“Watu hao Mheshimiwa Waziri Mkuu tunakuthibitishia kuwa wote watakaojitokeza kupiga kura hakuna jambo lolote baya litakalowakuta. Nyanyukeni, mkapige kura, yale makundi machache yanayojinasibu kwenye mitandao achieni vyombo vya dola, watashughulika nao vizuri kabisa bila kelele na ninyi mtapiga kura zenu kwa amani,” amesema Chalamila na kuongeza,
“Wanaojizima data, tutawawasha data ili ‘network’ ishike vizuri, waone kinachoendelea na sisi tunaitwa ‘Wanachotaka, Tunataka’,” amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliohudhuria.
Chalamila amesisitiza kuwa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha kuwa kila mwananchi anatekeleza haki yake ya kikatiba kwa amani bila bughudha yoyote.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.