Albert alimaanisha nini hapa?

Technian Tanga

JF-Expert Member
May 27, 2015
411
200
"When the solution is simple, God is answering." Hii ni Quotes ya Best kabisa Theoretical physcist A.Eistean ww unaitafisiri vipi
 
Naitafsiri kuwa pamoja na Mungu kukubarikia uintelejensi katika fani flani, hata tufanye vipi ukifa utaoza na huwezi kurudu kuinjoi kile ulichokigundua. Na kwamba vile vitu ambavyo tunaona ni vry hard kwa Mungu kujifanya kwa jicho LA kimungu ni simple task sana, ambalo sisi twaliona ni"solution lonalohitaji simple ansa"
 
"When the solution is simple, God is answering." Hii ni Quotes ya Best kabisa Theoretical physcist A.Eistean ww unaitafisiri vipi

Naomba kwanza ujitahidi kuandika jina la mzee sawa: Albert Einstein!

Halafu:
Tafsiri moja kwa moja "Kama suluhisho ni sahili, ni jibu la Mungu"

Maana yake: kama kuna maelezo sahili, haya ni sahihi, na kwa sababu asili ya uumbaji ni Mungu, basi lile sluhisho sahili ni jibu la Mungu kwa tatizo au swali linaloshughulikiwa na mtaalamu.

Kinyume kama elezo ni tata una uwezekano mkubwa ya kwamba si suluhisho bado. Kwa sababu muundo wa ulimwengu hufuata mantiki jinsi inavyoonekana katika hisabati yake.

Neno lingine la Mzee Albert Einstein ilikuwa: "Mungu hapigi dadu" (I cannot believe that God would choose to play dice with the universe).

Ukipenda kuingia ndani zaidi ujisomee kuhusu shughuli za Kopernikus na Glileo, jinsi walivyotambua tabia ya mfumo wa jua letu iliwapa amelezo sahili kwa mwendo wa sayari iliyoonekana angani tangu miaka maelfu. Wataalamu waliowatangulia walifuata andharia kumbe dunia iko kwenye kitovu cha dunia, halafu jua na sayari nyingine zinaizunguka. Hapa walipaswa kutoa maelezo tata sana kwa mwendo wa sayari jinsi ilivyoonekana angani. Kopernikus alipata wazo kuangalia mfumo tofauti: Jua katikati, na dunia pamoja na sayari kuzunguka jua. Hapa alipata makadirio sahili sana kwa kueleza mwendo wa sayari.

Sijui kama Einstein alikumbuka historia hii hasa lakini ni mfano unaofaa kueleza fikra yake kuhusu suluhisho sahili na jibu la Mungu.
 
Back
Top Bottom