Albamu ya Kanye west yapakuliwa mara 500,000

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160217091359_kanye_west.jpg

Image caption Kanye West
Albamu mpya ya mwanamuziki Kanye West imepakuliwa kutoka mtandaoni zaidi ya mara 500,000 kulingana na kampuni ya kupakua kanda za video na sauti Torrent Freak.


Msanii huyo alitoa albamu hiyo ya Life of pablo kutoka kwa huduma ya mtiririko wa muziki wa Jay-Z Tidal siku mbili zilizopita.

Maelfu ya raia waliolipa ili kusikiza albamu hiyo walilalama kwamba wameshindwa kupakua albamu hiyo licha ya kuilipia.


160217091419_kanye_west_2.jpg

Image caption Kanye West
Kwa sasa inaongoza miongoni mwa albamu zinazopakuliwa mitandaoni kwa njia ya wizi.

Albamu hiyo imeonekana mara mbili katika mtandao wa usambazaji wa miziki kumi bora iliopakuliwa,licha ya Kanye West kutuma ujumbe katika tweeter akisema kuwa albamu hiyo itapatikana katika Tidal pekee.
 
Back
Top Bottom