Alama ya Taifa :Sisi tuna nini?

aaamuk

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
707
Reaction score
209
Leo nilikuwa natazama habari DW kuhusiana na suicide bombers huko ufaransa. ..nikaona mnara wa Aifel.

Nikaanza kuvuta kumbukumbu nikakumbuka.

Brazil.wanayo
Ujerumani. Wanayo.
Marekani. Wanayo
China. wanayo

Swali nililojiuliza miaka yote hii ya kujitawala sisi tumejenga kitu gani kama alama ya u taifa. JE UNAPENDEKEZA TUJENGE NINI KAMA ALAMA YA TAIFA?
 
Hebu taja kwanza hizo za Brazil, Ujerumani na Marekani. Unajua mnara wa Eiffel ulijengwa lini na kwa lengo gani?

Sijaelewa kama unazungumzia nembo ya taifa au monuments...
 
Nazungumzia monuments ambazo ukiiona tu unajua ni ya nnchi gani
 
anza wewe kupendekeza. jikague kwanza kama kichwani kwako ipo unayodhani tunaweza kuitunia ndo utuukize ss tunawaza nn au tupendekeze yako.
 
Nazungumzia monuments ambazo ukiiona tu unajua ni ya nnchi gani
Hebu nitajie za hizo nchi ulizozitaja. Majirani zetu wanazo? Ni lazima tuwe nazo? Sijui kwa nini lakini nahisi kama vile hukufikiria vizuri ulipoamua kuanzisha hii thread. Hujengi monuments tu for the sake of it. Ndiyo maana nikakuulizia kama unajua historia ya hiyo Eiffel tower, Lady Liberty na Mount Rushmore kule Marekani n.k.
 
Okey...kwa hiyo mpaka sasa hatuna sababu ya kujenga any
 
Okey...kwa hiyo mpaka sasa hatuna sababu ya kujenga any
Sikiliza. Huwezi tu kuamka na kusema ngoja nianze kujenga monument. Ndiyo maana nikakuuliza kama unajua ni kwa nini hiyo Eiffel Tower ilijengwa na iligharimu kiasi gani. Huwezi kuamka tu na kusema ngoja nijenge piramidi kubwa la Kufu (Misri), The Great Wall of China (China), The Coliseum (Greece?), The Pantheon, Mount Rushmore, Lady Liberty etc. Ukijua kwanza sababu kwa nini hizi monuments zilijengwa na ziligharimu kiasi gani ndo utapata jibu. Tatizo lako hujibu maswali unayoulizwa. Ni nchi gani Afrika zina artificial monuments ambazo zinatumika kama vitambulisho vya nchi hizo? Monuments hizo, kama zipo, zilijengwa kwa sababu gani na ziligharimu kiasi gani? Majibu ya maswali haya yatakusaidia kujua kama thread yako hii ina tija ama la. Nadhani Mlima Kilimanjaro na/au Serengeti yetu vinatosha kabisa kututambulisha kimataifa kuliko eti tujenge li monument litakalogharimu mabilioni ya dola bila sababu ya msingi!
 
Mjombaa huku inasemekana dinosaurs waliishi Lindi. ...kwa nini tusijenge sanamu ya Dinosaur kwa mfano. ..


Mtu akiiona hiyo anajua this is Tanzania.

AUSTRALIA wanasymbol yao etc. .nadhani unanielewa sasa
 
Mjombaa huku inasemekana dinosaurs waliishi Lindi. ...kwa nini tusijenge sanamu ya Dinosaur kwa mfano. ..


Mtu akiiona hiyo anajua this is Tanzania.

AUSTRALIA wanasymbol yao etc. .nadhani unanielewa sasa
Sijakuelewa. Nenda Google ukaangalie historia ya hizo monuments unazodai ni vitambulisho vya mataifa yao. Na maswali yangu hapo juu mbona hujibu? Nitajie angalau nchi chache za Africa Mashariki na kwingineko zenye monuments tambulishi. Wewe umeona Eiffel Tower ya watu kwenye tv ukakimbilia kuanzisha thread bila kufikiria vizuri.

Mlima Kilimanjaro na Serengeti vinatosha kabisa tena vinatusaidia mpaka kwenye utalii sema tu tumezubaa!
 
Kama hutaki Mt.Kilimanjaro basi hatuna mpango Wa kujenga how DW tutawaambia watusymbolize kwa askari monument ya samora hahahahahaah
 
Ha ha ha ...tunajua sana kutoa visingizio vya kutofanya kitu..

Mfano tukiangalia na kujiuliza tumejenga kilomita ngapi za reli toka mkoloni aondoke...mtakuja na takwimu za barabara.. so funny
 
Hayo ma God given feature kila nnchi inayo. ..nilichokuwa nalenga ni our own creation..

Kuna hoja ikatolewa ni Google nijue sababu ya kujengwa hayo ma monuments. .nikauliza je sisi hakuna sababu?

Nikapendekeza sanamu ya Dinousar
 
Ha ha ha ...tunajua sana kutoa visingizio vya kutofanya kitu..

Mfano tukiangalia na kujiuliza tumejenga kilomita ngapi za reli toka mkoloni aondoke...mtakuja na takwimu za barabara.. so funny
Hakuna anayeleta visingizio. Wewe tu hoja yako haina mashiko. Huwezi tu kuanza kujenga monuments bila historical na cultural significance. Mlima Kilimanjaro na Serengeti vimetushinda kuvitangaza mpaka Wakenya wanadai viko kwao hiyo sanamu ya Dinosaur ndiyo tutaweza?

Acha kutangatanga. Hoja yako ndo ina matatizo. Mara ya kumi sasa nakuuliza unitajie nchi za Kiafrika zenye artificial monuments kama utambulisho wa taifa hutaki bali unaruka ruka tu. Safari nyingine kaa ufikirie vizuri kabla hujaanzisha thread na ukiulizwa maswali yenye lengo la kusukuma mjadala mbele jaribu kuyajibu. Hii ni Jamii Forums na siyo Facebook!
 
Hayo ma God given feature kila nnchi inayo. ..nilichokuwa nalenga ni our own creation..

Kuna hoja ikatolewa ni Google nijue sababu ya kujengwa hayo ma monuments. .nikauliza je sisi hakuna sababu?

Nikapendekeza sanamu ya Dinousar
Wewe ndiye mleta mada. The burden of proof is on you sir. Huwezi kuleta mada halafu tena ndo utuulize sisi tutoe sababu.

Soma hoja yangu hapo juu kwa mwendelezo zaidi. By the way kuhusu hiyo sanamu ya dinosaur, unajua kuwa kuna parks kabisa zilijengwa baada ya zile muvi za Jurassic Park za Steven Spielberg? Mojawapo ipo kule Tampa Florida kuna ma dinosaur makubwa mengine mpaka yanatembea utafikiri mazima. Sasa leo hii we ndo uchonge lisanamu la dinosaurs liwe kiwakilisho cha Tanzania? Kama unafikiri ni lazima kufanya hivyo, tunaweza kutumia vitu ambavyo vipo tayari lakini pia utahitaji millions of dollars kufanya kampeni dunia nzima ili waelewe significance ya hiyo monument yako. Haya mambo huwa hayatokei hivi hivi. Mlima Kilimanjaro na Serengeti vimetushinda, hiyo monument yako ndo tutaweza? Ni nchi gani zingine Africa wana hizi artificial monument kama national Identifiers? Nadhani kuna mambo mengine ya muhimu zaidi kuliko hili la kujenga monuments hata bila sababu za msingi!
 

Mkuu mwambie Mount Kilimanjaro is our international Icon.
 
Mkuu mwambie Mount Kilimanjaro is our international Icon.
Hataki natural features kama Mt. Kilimanjaro na Serengeti bali anataka (man made) monuments. Ameona Eiffel Tower ya Wafaransa jana baada ya kupigwa mabomu na magaidi sasa anataka na sisi tujenge artificial monument yetu iwe kitambulisho chetu cha kimataifa. Amependekeza sanamu ya dinosaur!
 
Nimepokea michango mizuri. ..nashukuru Great Thinkers

Sio vibaya tukipishana mtazamo. ..but nnchi za afrika kukosa hizo Iconic monuments kuna kitu cha kujiuliza. ...maana kama ni sababu za kujenga ziko nyingi lakini hakuna anayejali.

Let alone Egypt ambao wamefanya kitu.

Kama ukitazama upande wa pili wa shilingi jiulize nyumba walizojenga babu zetu kama bado zipo...au magofu yake.

Lakini nyumba walizojenga wakoloni Boma mpaka leo zipo au magofu yapo.
 
We are good at mazungumzo na sio matendo mpaka sasa we can not do anything in perfection. ...miji yetu tu inatushinda kuipanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…