Sao Hill ni eneo kubwa la ardhi lenye misitu ya kupandwa (pines, milingoti na miwati - tangu enzi za Mwalimu) pamoja na viwanda vya kuchana mbao na pia nguzo za umeme vikiwa ndani ya hilo eneo!
Linapatikana Mkoani Iringa, katika Wilaya ya Mufindi mbele kidogo tu baada ya kupita Mji Maarufu wa Mafinga ukitokea Iringa Mjini kwenye barabara kuu ya Tanzania - Zambia (TANZAM)