Alama ya Pundamilia iliyopo Sao Hill, ni kwa matumizi gani?

ila hiyo road from mafinga kwenda makambako isingekua na matuta watu wangekua wanakunjuka balaa yaani
 
😂😂😂😂😂 mlema mada kuna kituu kaa unatakusema lakini unasisita sita .

Kwanza nianze jinsi nilivyoielewa mada yako , mleta mada unahisi kuwa watu wa TANROAD ( au mkandarasi aliyeusika na uwekaji wa alama za barabara ) hakuwa sahihi kuiweka hyo alama hapo .

Kwanini kwasababu hapo ni darajani ukiangalia kushoto na kulia hakuna mwendelezo wa njia yoyote ambayo itamuwezesha mtumiaji wa barabara anayetokea kushoto kwenda kulia kulia au kulia kwenda kushoto sababu ya kizingiti cha mto maana mtu una kuwa upo katikati ya daraja .

Jibu langu .
Kwa upande wangu mimi wapo sahihi tu kuiweka hapo , kwanini ? Kwasababu barabara yoyote ile lazima iwe na upana maalumu ambao ndyo standard hapa nchini kwetu , na ndani ya huo upana lazima kuwepo na mistari itakayoenesha watembea kwa mikuu wanapita wapi ?, na magari ya kushoto yatapitawapi vile vile yakulia yapite wapi ? Huku katikati kukiwa na mstari maalumu unaomsaidia dereva kuweza kujua wapi aovertake na wapi asiovertake kutokana na namna mstari huo utakavyochorwa .

Tirudi sasa kwenye picha .

Kwenye picha nadhani unaiona hiyo mistari ya njano ( dash yellow lines ) kushoto na kulia mwabarabara mistari hiyo huonesha mpaka ambao gari zinazotumia barabara husika hazitakiwi kuuvika na kwakuwa ni dash n siyo full ( mstari mnene wa njano ulionyooka ( non dash yellow line ) gari itaruhusiwa kwenda kushoto au kulia mwa barabara kama tu itaitaji kupark au kaa inahitarafu furahi au kama dereva inaitaji kupumzika kidogo .

Baada ya huo mstari kuna nafasi ndogo kwaajili ya watembea kwa miguu iliyo katikati ya mstari mweupe pamoja na mstari wa njano .

Sasa basi walioweka hyo pundamilia walifikiria kuwa mtembea kwa miguu anaweza tokea upande wa kushoto au kulia msituni akaja akaingia barabarani na kuanza kutembea katikati ya mstari wa rangi nyeupe na njano ( ambalo ndyo eneo specially kwa ajili ya watembea kwa miguu ) mbaka hapo darajani na kupita kwenye hiyo zebra .


Sijui kaa niweza kukujibu na kama itakuwa bado nadhani wengine watakuja kutupa msaada zaidi.
 
Sao Hill ni eneo kubwa la ardhi lenye misitu ya kupandwa (pines, milingoti na miwati - tangu enzi za Mwalimu) pamoja na viwanda vya kuchana mbao na pia nguzo za umeme vikiwa ndani ya hilo eneo!

Linapatikana Mkoani Iringa, katika Wilaya ya Mufindi mbele kidogo tu baada ya kupita Mji Maarufu wa Mafinga ukitokea Iringa Mjini kwenye barabara kuu ya Tanzania - Zambia (TANZAM)
Aisee ni bonge la greenish treasury
 
Sao hill kumbe kuna wanyama pundamilia naungana na wewe kama hakuna wanyama pundamilia kivuko cha pundamilia cha nini? Kinabidi kiwekwe barabara za mbugani kama mbuga ya Ruaha au mikumi au Serengeti

Mimi nikiwa naendesha gari hasa mijini nikipita na gari eneo la kivuko cha pundamilia huwa napita spidi ya kufa mtu sisimami sababu najua mjini hakuna wanyama pundamilia kwa hiyo binadamu akitokea eneo hilo nikimgonga sitasimama na hata akinipeleka mahakamani nitamshinda kuwa kile ni kivuko cha pundamilia yeye ni pundamilia? Kilichomfanya apite pale ni nini? Wakati yeye sio mnyama pundamilia
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom