Alala na kula Serena kisha kutokomea bila kulipa deni la milioni 21, adakwa na kufikishwa mahakamani

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,508
8,129
Mkazi wa Dar es Salaam, Denis Mfumbulwa mwenye miaka 44 wa Goba Kulangwa amefikishwa mahakama ya mwanzo ya Kariakoo akidaiwa kujipatia malazi na chakula kwenye hoteli ya Serena kitapeli vyenye thamani ya milioni 21.4

Baada ya kupata huduma, mdaiwa alitokomea kusikojulikana. Mfumbulwa alikana mashtaka hayo. Pamoja na dhamana kuwa wazi, mshtakiwa amebaki rumande baada ya kushindwa masharti yake ya kuwa na bondi iliyosainiwa ya milioni 10.

Mwamba naona alijua ataambiwa tu aoshe vyombo kama wafanyavyo mama ntilie

Pia, soma=> Anayedaiwa kulala na kula Serena kisha kutokomea aachiliwa
 
Mkazi wa Dar es Salaam, Denis Mfumbulwa mwenye miaka 44 amefikishwa mahakama ya mwanzo ya Kariakoo akidaiwa kujipatia malazi na chakula kwenye hoteli ya Serena kitapeli vyenye thamani ya milioni 21.4

Baada ya kupata huduma, mdaiwa alitokomea kusikojulikana. Mfumbulwa alikana mashtaka hayo. Pamoja na dhamana kuwa wazi, mshtakiwa amebaki rumande baada ya kushindwa masharti yake ya kuwa dhamana iliyosainiwa ya milioni 10.
Hadi inavuka 10m wanamuangalia tu.
 
Utakuta alikua hajui gharama za hio hotel, alidhani ni zile lodge za mtaani soda Tsh buku. Unakuta alikua na kamilioni ame bet akaona akajipongeze.

Baada ya bill kuja akaona uwezo wa kulipa hana bora kutokomea kusikojulikana, hii inawakuta wengi unafika sehemu unaagiza msosi wakati hufahamu utaratibu wa eneo hilo.
 
Hiyo kesi Ina miezi zaidi ya sita kama sikosei na huyo jamaa alikuwa na wenzake. Walianzia Hyatt wakaenda Rotana, mwisho wakakamatiwa Serena. Alikuwa na wakenya. Kuna watu wamdpiga pesa wakenya wameachiwa
Ila kuna watu wana tabia, tamaa na mambo ya ajabu. Hutakiwi kulazimisha maisha ishi kulingana na uwezo wako.

Kuna mtu na mke wake wazungu watu wazima tu huko uingereza tabia yao ilikuwa kula restaurant nzuri ghali wanaagizia steaks wakishamaliza hawalipi bills wanatoroka hadi za pauni 200 CCTV footage zikawaumbua. Wakatangazwa na kuanikwa kwenye magazeti ya umbea ya uingereza (tabloids) the sun na dailymail. Wameshikwa na kushtakiwa.

Yani ukiwaona muonekano wao kwa nje ni nadhifu huwezi kuwashuku na kuamini hawa.

Black Sniper
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom