Alaf acheni kudharau wateja wenu

Alaf acheni kudharau wateja wenu

miyamba

Member
Joined
Nov 30, 2019
Posts
10
Reaction score
9
Jamani Alaf wanakua wazuri kabla mteja hajafanya malipo hua wanakua na maneno mazuri sana ya kumbembeleza mteja. Ila ukishalipia unaonekana takataka, Nimefanya malipo tangu tarehe mbili hadi sasa sijapata mzigo wangu wa mabati kila nikifika wananizungusha wanadai mabati yamekatwa tatizo ni mtandao, Nilidhani ni mimi peke yangu ila kila mteja analalamika sana kutojaliwa baada ya kufanya malipo.

Pia kuna madalali wengi sana yaani ukishaingia getini wamejaa kibao wanakung'ang'ania, wanataka wakupeleke ndani mimi nikawaambia sihitaji kuingizwa na mtu yoyote nikaenda ndani nikafanyiwa mahesabu nikalipa tatizo ni kuupata mzigo, juzi wameniambia mabati yako yako tayari tatizo ni mtandao,

Alaf mnatuchosha Sisi wateja wenu badilikeni ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana mmeshindwana kiswahili, kiswahili chako kigumu sana hebu kibrashibrashi kieleweke na unayemlenga ajijue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom