Aladin na taa ya ajabu

Aladin na taa ya ajabu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430

ALADDIN NA TAA YA AJABU --- SEHEMU YA KWANZA (1)​

ALADDIN NA TAA YA AJABU

Hapo zamani kabisa, aliishi mshonaji masikini, ambaye alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Aladdin, ambaye alikuwa ni mzembe na mvivu kabisa, asiyependa kufanya kazi yoyote isipokuwa kucheza mitaani na watoto wenzake wavivu kama yeye.

Tabia hii ya mwanawe, ilimhuzunisha sana mshonaji, mpaka ikapelekea apate ugonjwa ambao ulisababisha kifo chake. Ingawa mama yake Aladdin alifanya kila aliloweza, alilia na kufanya kila aina ya maombi, lakini mwanawe hakubadilika, aliendelea na tabia yake ileile.

Siku moja akiwa anacheza mitaani kama kawaida yake, alikuja mgeni mmoja na kumuuliza umri wake, na kama yeye hakuwa mtoto wa Mustafa mshonaji. Alijibu Aladdin; “Ndiye mimi, lakini baba yangu alishakufa muda mrefu uliopita”. Baada ya kusikia hili, yule mgeni ambaye alikuwa ni mchawi maarufu wa kiafrika, alimkumbatia Aladdin na kumbusu, huku alikwambia; “Mmi ni baba mdogo wako, nilikujua kutokana na kufanana kwako na kaka yangu. Nenda kwa mama yako na umwambie kwamba nakuja”.

Aladdin alikimbia kwenda nyumbani, ambako alimwambia mama yake habari za baba yake mdogo. “Kweli, mwanangu. Baba yako alikuwa na ndugu yake, lakini siku zote nilidhani kuwa alishafariki” alisema Mama yake Aladdin. Hata hivyo aliandaa chakula cha usiku, na kumtaka Aladdin akamtafute baba yake mdogo, ambaye alikuja akiwa na mvinyo na matunda.

Alipofika pale, alianguka chini na kubusu sehemu ambayo Mustafa alikuwa akipenda kukaa, huku akimtaka Mama yake Aladdin asishtuke kwa kutomuona hapo kabla, kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kwa muda wa miaka arobaini. Kisha alimgeukia Aladdin, na kumuuliza alikuwa akifanya biashara gani, ambapo Aladdin aliinamisha kichwa chini, na Mama yake alianza kulia.

Baada ya kujua kwamba Aladdin alikuwa ni mvivu na hajui kufanya biashara yoyote, alitaka kumchukua na kumfungulia duka ili auze bidhaa. Siku iliyofuata, yule baba mdogo alimnunulia Aladdin, nguo mpya nzuri, na alimchukua na kwenda kutembea nae mjini, aklimuonyesha maeneo mbalimbali, ilipofika usiku alimrudisha kwako, ambapo Mama yake alifurahi sana kumuona mwanawe akiwa yupo vizuri.

Siku iliyofuata, yule mchawi alimchukua Aladdin na kumpeleka kwenye bustani nzuri sana iliyokuwa mbali kidogo na mji. Walikaa chini kwenye chemchem, na yule mchawi alitoa keki kutoka kwenye mfuko wake, aliikata kati na kipande kumpatia Aladdin. Waliendelea kusafiri mpaka wakafika milimani. Aladdin alichoka sana na aliomba warudi.

Mchawi hakutaka warudi, hivyo aliendelea kumlaghai Aladdin kwa hadithi tamu tamu ili safari yao iendelee. Mwisho walifika kwenye milima miwili iliyotenganishwa na bonde jembamba.
Mchawi alimwambia Aladdin; “Tutaishia hapa, hatutaendelea na safari, nitakuonyesha kitu kizuri. Kusanya kuni niwashe moto”. Aladdin alikusanya kuni na mchawi aliwasha moto. Baada ya moto kuwaka, yule mchawi alitoa unga mweupe na kuutupia kwenye ule moto huku akitamka maneno ya kichawi. Ardhi ikatikisika kidogo na ikafunguka, lilionekana jiwe kubwa lenye umbo la mraba likiwa na mshikio katikati.

Aladdin alijaribu kukimbia lakini mchawi alimkamata na kumzaba kibao kilichofanya aanguke chini. Aladdin aliongea kwa upole uliojaa woga; “Nimefanya nini Baba mdogo. Mchawi alijibu kwa upole nae; “Usiogope kitu, nitii mimi. Chini ya jiwe hili kuna hazina ambayo ni ya kwako, na hakuna yeyote awezaye kuigusa, hivyo lazima ufaye kama ninavyokuambia”.

Baada ya kusikia neno ‘hazina’, woga ulimuondoka Aladdin, aliishika kwa nguvu pete kama alivyoambiwa, huku akitaja majina ya Baba na Babu yake. Jiwe lilikuja juu na kufunguka, ngazi zilionekana. Mchawi alimwambia Aladdin; “Nenda, chini kabisa ya hizo ngazi utaona mlango upo wazi ambazo utakupeleka kwenye kumbi kubwa tatu. Kunja kanzu yako na upite bila kugusa kitu chochote au utakufa. Hizo kumbi zinaongoza kwenye bustani ya miti ya matunda matamu. Endelea kwenda mpaka ufike kwenye pembe ya varanda ambapo kuna taa ya chemli inayowaka. Mwaga mafura yake na uniletee”.

Mchawi alivua pete yake na kumpa Aladdin, na kumtakia kila la kheri. Aladdin alikutakila kitu kipo kama mchawi alivyosema, alichuma baadhi ya matunda na kuchuka ile taa, alirudi na kufika kwenye mlango wa pango. Mchawi alimpigia kelele kuwa aharakishe; “Fanya haraka unipe taa hiyo”. Aladdin alikataa kumpa ile taa, akitaka mpaka atoke nje ya pango lile.

Mchawi alishikwa zaidi na hasira, akamwaga unga mwingine kwenye moto na kutamka maneno yake ya kichawi, lile jiwe lilirudi na kujifunga kama mwanzo. Mchawi aliondoka kutoka Fursi daima, jambo lile lilimuonyesha Aladdin kuwa yule hakuwa Baba yake mdogo, ila ni mchawi tu ambaye alisoma kwenye vitabu kuhusu taa ya ajabu, ambayo ingemfanya yeye kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani.

Ingawa ni yeye (mchawi) tu ndiye aliyejua taa ilipo, lakini ilikuwa ni lazima aipokee kutoka kwenye mikono ya mtu mwingine. Alimchagua mpumbavu Aladdin kwa jambo hili, akiazimia kupata taa na kumuua Aladdin baada ya hapo.

Kwa muda wa siku mbili, Aladdin aliendelea kubaki gizani, akilia na kujuta. Mwisho alikuwa akisugua mikono kwa maombi, katika kufanya aliisugua ile pete, ambayo mchawi aliisahau kuichukua kutoka kwake. Kwa haraka alitokea Jini mkubwa anayetisha sana, akasema; “Unataka nini kwangu? Mimi ni mtumwa wa pete na nitakutii na kufanya chochote utakacho”.

Bila woga Aladdin alijibu; “Nitoe kwenye hii sehemu!”. Ardhi ikajifungua, na Aladdin alijikuta yupo nje. Baada ya kukaa sawa, alianza kurudi nyumbani kwao. Alipofika, alimwambia Mama yake kilichotokea, alimuonyesha taa na matunda, ambayo kumbe yalikuwa ni madini kuhalisia (sio matunda).

Aladdin aliomba chakula kwa Mama yake. Mama alijibu; “Aah!! Mwanangu, hamna kitu leo. Lakini nimechuma pamba kidogo, nitakwenda kuuza na kununua chakula”. Aladdin alimwambia Mama yake ahifadhi pamba yake, badala yake atakwenda yeye (Aladdin) kuuza ile taa. Kwa kuwa ilikuwa chafu sana,Mama yake alianza kuisugua ili iwe safi na aiuze walau kwa bei ya kuridhisha kidogo.

Wakati akiendelea kuisugua ile taa, ghafla alitokea Jini na kuuliza kitu gani anataka. Mama alizimia, lakini Aladdin aliwahi na kusema; “Niletee chakula”, Jini alileta bakuli, sahani kumi na mbili zilizojaa nyama nzuri, vikombe viwili na chupa mbili za mvinyo, vyombo vyote vilikuwa vya fedha.

Mama alipozinduka alisema; “Vyakula hivi vizuri vimeletwa na nani?”. Aladdin alijibu; “Mama usiulize, wewe kula tu”. Walikula, mpaka ilipofika mchana, Aladdin alimwambia Mama yake kuhusiana na taa. Mama alimuomba Aladdin auze ile taa na asijishughulishe na Majini. Aladdin alisema; “Hapana, lazima tuitumie hii taa na hii pete vilevile, ambayo itakuwa kidoleni kwangu kila siku”.

Walipomaliza kula vyakula vyote vilivyoletwa na Jini, Aladdin aliuza moja ya sahani zake za fedha na nyingine mpaka zikaisha zote. Kisha aliendelea kumuita Jini, ambaye alimpatia sahani nyingine, walikula chakula na sahani kuuza. Waliendelea kuishi vile kwa miaka mingi.

Siku moja Aladdin alisikia amri kutoka kwa Sultani, ikisema kwamba kila mmoja anatakiwa asitoke nyumbani kwake na afunge milango na madirisha wakati Bintisultani akienda na kurudi kutoka kuoga. Aladdin alishikwa na tamaa haswa ya kuuona uso wa Bintisultani, kitu ambacho kilikuwa ni kigumu, kwasababu muda wote aliufunika uso wake kwa nikabu.

Aladdin alikwenda kujificha nyuma ya mlango wa bafu, na alikuwa akichungulia kupitia kitobo kidogo. Bintisaltani alipandisha nikabu yake alipokuwa akiingia, alikuwa ni mrembo sana kiasi kwamba Aladdin alijikuta akimpenda na kuzama palepale. Aladdin alirudi nyumbani kwao akiwa amebadilika sana mpaka Mama yake akaogopa labda huenda mwanae kapata tatizo.

Aladdin alimwambia Mama yake kwamba amempenda Bintisultani sana kiasi kwamba hatoweza kuishi bila yeye na anahitaji kumuowa. Mama yake aliposikia hili, aliangua kicheko kikubwa, lakini Aladdin alimuomba Mama yake aende kwa Sultani akafikishe ombi lake. Mama alichukua kitambaa na kuweka ndani yake yale matunda ya kichawi kutoka bustani ya kichawi, ambayo yaling’aa kama vito vizuri vya rhamani. Mama alibeba vitu vile ili walau amfurahishe Sultani.

Mama alitoka na kuelekea Ikulu, Mshauri mkuu na Wakuu wengine wa serikali waliingia kwenye ukumbi wa mkutano. Wakati huo Mama yake Aladdin naye aliingia ukimbini pale na kusimama sehemu ya mbele akiangalia kiti cha enzi cha Sultani. Hatahivyo, Sultani hakumzingatia (hakumtilia maanani).

Mama aliendelea kwenda pale kila siku kwa muda wa wiki nzima. Pindi mkutano ulipoisha kwenye siku ya sita, Sultani alimuuliza Mshauri wake; “Huwa ninamuona mwanamke fulani kwenye chumba cha mikutano kila siku akiwa amebeba kitu kwenye kitambaa. Nataka umuite, ili nijue anahitaji kitu gani”.

Siku iliyofuata, kwa ishara ya Mshauri mkuu, Mama yake Aladdin alikwenda kwenye kiti cha enzi na kubaki akiwa amepiga magoti huku macho ameinamisha chini mpaka Sultani alipomwambia; “Inuka ewe mwanamke mwema na uniambie unataka nini”. Mama alisita kidogo, hivyo Sultani aliondoa watu wote isipokuwa Mshauri wake, na kumuomba azungumze kwa uhuru, huku akimuahidi kutochukizwa na kusamehe kwa chochote atakachozungumza.

Mama alimueleza Sultani kuhusu suala la mwanawe (Aladdin) kumpenda sana Bintisultani. “Nilimuomba sana amsahau” alisema Mama, “Lakini ilishindikana, alitishia kufanya kitu kibaya kama ningekataa kuja kukuambia kuhusu yeye kutaka kumposa Binti yako. Sultani naomba unisamehe mimi na mwanangu”.

Sultani kwa upole alimuuliza yule Mama kitu gani amebeba kwenye kitambaa, Mama alifungua kitambaa chake na kumuonyesha Sultani vile vito vya thamani kubwa alivyobeba. Sultani alipigwa na butwaa, akamgeukia Mshauri wake na kumwambia; “Ulisema nini? Hivi sihitajiki kumuoza Binti yangu kwa mtu ambaye anamthamini kwa gharama kama hii?”.

Mshauri, ambaye alikuwa akitaka Bintisultani aolewe na mwanaye, alimuomba Sultani aendelee kusubiri kwa miezi mitatu, huku akiwa na tumaini kwamba mwanaye atamletea Sultani zawadi za gharama kubwa kuliko zile. Sultani alikubaliana na jambo lile, na kumwambia Mama Aladdin kwamba ingawa yeye amekubali na jambo la ndoa, lakini Mama Aladdin hatakiwi kuja tena kwa Sultani mpaka ipite miezi mitatu.

Aladdin aliendelea kusubiri kwa karibu miezi mitatu, lakini baada ya miezi miwili kupita, Mama Aladdin alikwenda mjini kununua mafuta, alimkuta kila mtu akifurahi, aliuliza ni kitu gani kinaendelea. “Hujui!! Mtoto wa Mshauri mkuu anamuoa Bintisultani usiku wa leo?” hilo ndio lilikuwa jibu.

Mama Aladdin akiwa kaishiwa pumzi, alirudi nyumbani haraka na kumwambia Aladdin habari zile, alipatwa na mshtuko mkubwa, lakini alitulia na baadae kidogo aliikumbuka taa yake. Aliisugua na Jini alitokea na kusema; “Unataka nini?”. Aladdin alijibu; “Sultani kama unavyomjua, amevunja ahadi yake kwangu, na amamuoza Binti yake kwa mtoto wa Mshauri. Amri yangu ni kwamba, usiku wa leo uwalete hapa bwana na bibiharusi”. “Ninatii, Bwana wangu” alisema Jini.

Aladdin alikwenda chumbani kwake,ambapo usiku ule, Jini alileta kitanda kilichowabeba Bintimfalme na mumewe. Aladdin alimwambia Jini; “Mchukue huyu bwanaharusi mpya umpeleke nje kwenye baridi, kisha urudi asubuhi”. Jini alimchukua mtoto wa Mshauri mkuu na kumpeleka nje huku kitandani akibaki Aladdin na Bintisultani. Aladdin alimwambia Bintisultani; “Usiogope kitu, wewe ni mke wangu, niliyeahidiwa na Baba yako asiyetenda haki, na hautadhurika na chochote”. Bintisultani aliogopa sana na usiku ule ulikuwa ndio usiku mgumu kwenye maisha yake, wakati akiwa amelala pembeni yake tena akikoroma sana.

Muda ulipofika, Jini alirudi akamchukua bwanaharusi kutoka kwenye baridi na kumlaza kitandani, kisha alikirudisha kile kitanda ikulu. Sultani alikwenda kumsalimia Binti yake, mtoto wa Mshauri alijificha, wakati Bintisultani hakuweza kusema neno lolote na alikuwa ni mwenye huzuni sana.

Sultani alipoona hali ile, alimtuma mkewe akazungumze na mwanawe; “Vipi mwanangu hauzungumzi na Baba yako? Nini kimetokea?”. Bintisultani alishusha pumzi nzito na kumwambia Mama yake, wakati wa usiku, kitanda chao kilipelekwa kwenye nyumba ngeni, na kilichotokea huko. Mama yake hakumuamini, lakini alimuomba aichukulie ile kama ni ndoto mbaya tu.

Usiku uliofuata, kitu kile kile kilitokea tena, na asubuhi iliyofuata kwa kitendo cha Bintisultani kukataa kuongea na Sultani, Sutani alitishia kumkata kichwa. Bintisultani kwa kuogopea maisha yake, alisema yaliyotokea yote kwa Sultani, na kumwambia kama ataona ni uongo basi amuulize mtoto wa Mshauri mkuu (ambaye ndiye mume wa Bintisultani).

Sultani alimwambia Mshauri wake amuulize mtoto wake, ambaye alisema ukweli wote, na kuongeza kwamba, ingawa alimpenda sana Bintimfalme, lakini yupo ni bora kwake kufa kuliko kupitisha usiku mwingine wa kutisha na kuomba aachanishwe na Bintimsultani. Ombi la mtoto wa Mshauri mkuu lilikubali na hivyo kuachana na Bintisultani.

Pindi miezi mitatu ilipoisha, Aladdin alimtuma Mama yake kwenda kumkumbusha Sultani kuhusu ahadi yake. Sultani alipoona Mama yake ni masikini sana, alijihisi uzito kutekeleza ahadi yake, alitaka ushauri kutoka kwa Mshauri wake, alimshauri Sultani kuweka mahari kubwa sana ambayo hakuna mtu yeyote atakayeweza kuimudu.

Sultani alimgeukia Mama Aladdin na kumwambia; “Mwanamke mwema, Sultani lazima akumbuke ahadi yake, na mimi nitaikumbuka ya kwangu, lakini mtoto lazima aniletee mabakuli arobaini ya dhahabu yaliyojaa vito vya thamani, yakiwa yamebebwa na watumwa arobaini weusi, wakiwa wamevaa mavazi ya thamani. Mwambie mwanao nasubiri jibu lake”.

Mama Aladdin alirudi nyumbani akihisi tayari wameshindwa. Alifikisha ujumbe kwa Aladdin na kumwambia; “Ametoa muda mrefu wa kusubiri jibu kutoka kwako”. “Sio muda mrefu Mama, kama unavyofikiria” alijibu Aladdin, “Nitafanya jambo kubwa zaidi ya hilo kwa ajili ya Bintimfalme”.

Aladdin alimuita Jini, na ndani ya muda mfupi walifika watumwa themanini na kujaa nyumba nzima mpaka kwenye bustani. Aladdin aliwataka waelekee ikulu, wawili kwa wawili, wakiongozwa na Mama yake. Walikuwa na wamevaa ya gharama sana, wakiwa na vito vya thamani kwenye mikanda yao, huku wakiwa mabakuli ya dhahabu vichwani mwao, watu walikusanyika kwa wingi kuwaangalia.

Waliingia ikulu, na baada ya kupiga magoti mbele ya Sultani, walisimama nusu mduara kuzunguka kiti cha enzi, wakati huo Mama yake Aladdin aliwatambulisha kwa Sultani. Sultani hakusita tena, ila alisema; “Mwanamke mwema, rudi na umwambie mwanao kwamba ninamsubiri kwa mikono mikunjufu kabisa”.

Mama hakupoteza muda kwenda kumwambia Aladdin na kumtaka afanye haraka. Lakini Aladdin kwanza alimuita Jini na kumwambia; “Nahitaji kuoga maji yanayonukia, farasi mzuri kuliko wa Sultani, watumwa ishirini. Pia nahitaji watumwa sita wakiwa na mavazi ya gharama wakumsindikiza Mama yangu, na mwisho nahitaji vipande elfu kumi vya dhahabu vikiwa ndani mikoba kumi”. Vitu vyote hivyo vikatokea palepale.

Aladdin alipanda farasi wake na kupita mitaani, watumwa wake walikuwa wakirusha dhahabu huhu na huko wakati wanakwenda. Wale waliocheza naye utotoni, hawakumjua kabisa, alikuwa amependezac sana. Sultani alipomuona Aladdin akija, alishuka kwenye kiti chake cha enzi ili kumlaki, na kumuongoza mpaka kwenye ukumbi ambako kuliandaliwa sherehe kubwa, huku Sultani akiwa ameazimia kumuoza Binti yake kwa Aladdin siku ileile.

Lakini Aladdin alikataa kuoa siku ile na kusema; “Lazima nijenge Kasri linaloendana na Bintisultani”. Baada ya kusema vile Aladdin aliondoka. Alipofika nyumbani alimwambia Jini; “Nijengee Kasri kubwa lenye kunakshiwa kwa marumaru na mawe mengine ya thamani. Katikati ya Kasri kujengwe kuba, kuta nne za dhahabu na fedha, kila upande liwe na madirisha sita, isipokuwa moja, liachwe likiwa halijamaliziwa matengenezo yake, hayo madirisha yapambwe kwa almasi na yakuti. Lazima kuwe na farasi, wachungaji wake na watumwa”.

Siku iliyofuata, kazi ya kujenga Kasri ilikuwa imeisha na Jini alimchukua Aladdin na kumpeleka kumuonyesha, na kulitandikwa kapeti kutoka kwenye Kasri ya Aladdin mpaka kwa Sultani. Mama Aladdin alivaa vizuri, na kuanza safari ya kuelekea ikulu akiwa na watumwa wake, huku Aladdin akimfuata Mama yake kwa nyuma akiwa juu ya farasi.

Sultani alipeleka wanamuziki wakiwa na matarumbeta na ngoma kwenda kuwapokea. Mama Aladdin alipelekwa kwa Bintisultani, ambaye alimsalimia kwa heshima kubwa sana. Usiku Bintisultani alimuaga baba yake, na kuanza safari kuelekea kwenye Kasri ya Aladdin akiwa na Mama yake huku akifuatwa na watumwa mia. Bintisultani alifarishwa alifurahishwa na muonekano wa Aladdin, ambaye aliwahi kumpokea.

“Bintisultani, ulaumu uzuri wako kwa vitendo vyangu kama nitakuwa nimekuudhi” alisema Aladdin. Bintisultani alimwambia kwamba, kwa kule kumuona tu, basi amekubaliana na baba yake kwa moyo wote juu ya jambo lile la ndoa.
 
ALADDIN NA TAA YA AJABU --- SEHEMU YA PILI (2)​

Baada ya ndoa kupita, Aladdin alimchukua mkewe mpaka ukumbini, ambako kulikuwa na sherehe, walikuwa chakula cha usiku, bada ya hapo walicheza mpaka saa 6 usiku. Siku iliyofuata, Aladdin alimualika Sultani kuona Kasri yake. Waliingia kwenye ukumbi wenye madirisha ishirini na nne, yenye yakuti, almasi na zamaridi.

Sultani alipigwa na butwaa na kusema; “Hii ni moja ya maajabu ya dunia! Kuna kitu kimoja kinanishangaza hapa. Ilikuwa ni bahati mbaya kwamba dirisha moja limeachwa bila kumaliziwa?”. Aladdin alijibu; “Hapana, nilitaka wewe Sultani utie baraka zako kwa kumalizia hii sehemu”.

Sultani alifurahi, alileta Masonara bora pale mjini na kuwaonyesha dirisha ambalo halijamaliziwa, na kuwataka walitengeneze kama yale mengine. “Sultani, hatuna vito vya kutosha kumalizia dirisha hili” alisema msemaji wa Masonara. Sultani alihangaika kutafuta vito na kuvileta, vilitumika vyote vikaisha, lakini bila kutaraji, kwa mwenzi mzima kazi ilikuwa haijafika hata nusu.

Aladdin akiwa anajua kuwa kazi ile imeshindikana, aliwaomba waiache na kuwarudishia vito vyao walivyokuwa tayari wamevitumia, na Jini alimalizia lile dirisha. Sultani alingaa kurudishiwa vito vyake, na hivyo alimtembela Aladdin, ambaye alimuonyesha kuwa tayari dirisha limemaliziwa.

Sultani alimsifu Aladdin, lakini yule Mshauri mwenye alianza kuhisi huenda Aladdin akawa anatumia uchawi. Aladdin alipendwa sana na watu kwa misaada aliyokuwa akitoa. Alipewa cheo na kuwa Jenerali wa majeshi ya Sultani, na alishinda vita vingi sana, lakini alibaki kuwa na moyo uleule kama mwanzo wala hakubadilika, na aliishi kwa amani kwa miaka mingi.

Lakini mbali kabisa Afrika huko, yule mchawi alimkumbuka Aladdin, na kwa kutumia uchawi wake aligundua kuwa Aladdin badala ya kufa ndani ya pango, aliokoka na kumuoa Bintisultani, na alikuwa akiishi kwenye utajiri mkubwa na heshima kubwa. Mchawi alijua kabisa kwamba yule mtoto wa mshonaji masikini aliweza kuyafanya yale yote kwa kutumia ile taa.

Mchawi alisafiri usiku na mchana mpaka akafika kwenye mji wa china, aliapa kumuangamiza Aladdin. Alipokuwa akipita mjini alisikia watu wakiongelea habari za Kasri la ajabu. Mchawi aliamua kumuuliza mtu mmoja; “Naomba unisamehe kwa ujinga wangu, Kasri ipi hiyo mnaizungumzia?”. “Hujawahi kusikia habari za Kasri la Aladdin, ajabu kubwa zaidi la dunia? Nitakupeleka kama utataka kuliona” alisema yule mtu.

Mchawi alimshukuru, na baada ya kuliona lile Kasri, mchawi alijua kabisa kuwa ni kazi ya Jini wa taa, alibaki akiwa amechanganyikiwa kwa hasira. Aliazimia kwanza kuipata ile taa na kumtupa Aladdin kwenye umasikini mzito kabisa. Kwa bahati Aladdin alikuwa ametoka kwenda kuwinda kwa muda wa siku nane, huu ulikuwa ni muda wa kutosha kwa mchawi kufanya mambo yake.

Mchawi alinunua dazeni ya taa za shaba, akaziweka kwenye kikapu, na kuelekea kwenye Kasri huku akipiga kelele kwa kusema; “Nabadilisha taa mpya kwa ya zamani!” huku kundi la watu wakimfuata kwa kumfanyia masikhara. Bintisultani akiwa amekaa kwenye ukumbi wenye madirisha ishirini na nne, alimtuma kijakazi wake akaangalie hizo kelele zilikuwa zinahusu nini, kijakazi alirudi huku akicheka na kumwambia Bintisultani; “Bibi, nani anayezewa kujizuia kucheka kwa kumuona mzee mpuuzi akitoa ofa ya kubadilisha taa mpya kwa ya zamani?”.

Kijakazi mwingine aliposikia suala lile alisema; “Kuna taa moja ya zamani ipo kule imening’inizwa, labda apewe hiyo”. Ile ndio ilikuwa taa ya uchawi, ambayo Aladdin aliiacha pale, kwasababu hakuweza kwenda nayo mawindoni. Bintisultani bila kujua thamani ya taa ile, huku akicheka alimtaka aichukue na kwenda kufanya mabadilishano.

Kijakazi alikwenda na kumwambia yule mchawi; “Nipe taa mpya, chukua hii”. Mchawi aliichukua ile taa na kumtaka yule kijakazi achague mpya aipendayo. Baada ya hapo mchawi alijifanya kuendelea na biashara yake, na kutoka kabisa nje ya mji. Alikaa huko mpaka usiku ulipoingia, aliitoa taa na kuanza kuisugua. Jini alitokea, na mchawi alimpa amri kwamba amchukue yeye pamoja na Kasri ndani yake akiwa Bintisultani mpaka Afrika.

Asubuhi iliyofuata, Sultani alitazama Kasri la Aladdin kupitia dirishani lakini hakuliona, alisugua macho yake vizuri lakini bado hakuliona. Alimuita Mshauri wake na kumuuliza kimetokea kitu gani kwenye Kasri. Mshauri naye alitazama nje na kupigwa na butwaa. Mshauri alisema ule ni uchawi, na Sultani alimuamini, alituma askari thelathini wakamkamate Aladdin na kumleta kwake akiwa kwenye minyororo.

Askari wale walimkuta Aladdin akiwa juu ya farasi akirudi nyumbani, walimkamata, na kumlazimisha atembee kwa miguu akiwafuata. Watu ambao walimpenda sana Aladdin, walimfuata, wakiwa na silaha, kuona kwamba Aladdin hadhuriki na chochote. Alipelekwa mbele ya Sultani, ambaye alitoa amri kwa muuaji amkate kichwa. Muuaji alimpigisha magoti Aladdin, akamfunga macho kwa kitambaa na kuinua panga ili akate kichwa cha Aladdin kwa amri ya Sultani.

Kwa muda ule Mshauri, ambaye aliona kundi kubwa la watu waliokuwa wakilazimisha kuingia ndani na wengine wakiparamia ukuta ili kwenda kumuokoa Aladdin, alimwambia muuaji asubiri kwanza. Watu wakiwa wenye hofu na hasira imewajaa, hali ile ilimtisha Sultani mpaka alitoa amri kwamba Aladdin afunguliwe na kumtaka msamaha mbele ya watu.

Aladdin aliomba kujua amefanya nini. Sultani alisema kwa hasira; “Mchawi muongo wewe!! Njoo hapa”, alimuonyesha kupitia dirishani sehemu ambayo Kasri lake lilikuwepo. Aladdin alipigwa na mshangao mpaka alishindwa kutamka neno lolote. “Iko wapi Kasri yangu na Mwanangu? Kwa hilo la kwanza sihusiki sana, ila mwanangu lazima nimpate, na wewe lazima umtafute au utapoteza kichwa chako” alifoka Sultani.

Aladdin aliomba apatiwe siku arobaini ili amtafute Bintisultani na kama atashindwa basi atarudi ili apatiwe adhabu ya kifo. Ombi lake lilikubaliwa na aliondoka akiwa mwenye huzuni sana. Kwa siku tatu mfululizo alizurura kama mwendawazimu, akimuuliza kila mmoja kilitokea kwenye Kasri yake, lakini wengine walimcheka na wengine walimonea huruma tu.

Aladdin alifika kwenye kingo za mto, alipiga magoti na kuanza kuswali swali yake ya mwisho kabla ya kujitosa mtoni. Wakati akifanya hivyo aliisugua ile pete ya kichawi aliyokuwa ameivaa. Jini aliyemuona kule pangoni alijitokeza na kumuuliza anataka nini. “Okoa maisha yangu Jini, naomba uniletee Kasri yangu” alisema Aladdin kwa unyonge.

Jini alijibu; “Jambo hilo halipo kwenye nguvu zangu. Mimi ni mtumwa wa pete tu, lazima umuombe mtumwa wa taa”. “Hatahivyo, lakini unaweza kunipeleka kwenye Kasri yangu, na kuniweka chini ya dirisha la mke wangu” alisema Aladdin. Mara moja Aladdin alijikuta yupo Afrika, chini ya dirisha la Bintisultani, alilala pale chini kidogo.

Alikuja kuamshwa kwa sauti za ndege, na moyo wake ulikuwa mwepesi. Aliona mikosi au matatizo yote yaliletwa kwa sababu ya upotevu wa taa, na alijiuliza ni nani aliyekuwa ameiba ile taa. Asubuhi ile, Bintisultani aliamka mapema sana tangu achukuliwe na kuletwa Afrika na yule mchawi, hatahivyo Bintisultani alimfanyia vitimbi yule mchawi kiasi kwamba hakutamani waishi pamoja.

Wakati Bintisultani akivaa nguo, mmoja wa vijakazi wake aliangalia nje na kumuona Aladdin, alikimbia kumwambia Bintisultani. Bintisultani alikimbia na kufungua dirisha, alimuita Aladdin kwa sauti kubwa na Aladdin alitazama juu na kumuona mke wake. Bintisultani alimmwambia Aladdin aingie ndani, na furaha ilikuwa kubwa sana kwa wapenzi hawa wawili kuonana tena.

Baada ya kupigana mabusu mawili matatu, Aladdin alimwambia mkewe; “Ninakuomba mke wangu, kwa jina la Mwenyezimungu, kabla hatujaongea kitu chochote, kwa ajili ya usalama wako na wangu, niambie kitu gani kwenye ile taa niliyoiacha pale kenye kona ya ukumbi wa madirisha ishirini na nne nilipokwenda kuwinda”. “Aaah!! Mimi mdiye msababishaji wa tatizo hili” alijibu Bintisultani, na kumueleza kuhusu kubadilishana kwa taa.

Aladdin alisema; “Sasa nimeshajua, inabidi tumshukuru huyu mchawi wa kiafrika kwa jambo hili! Iko wapi taa?”. Bintisultani alisema; “Muda wote huwa nayo yeye. Na anahitaji kunioa, huku akiniambia kwamba tayari wewe ushachinjwa na baba yangu. Siku zote anaongea mabaya kuhusu wewe, lakini kila siku huwa najibu kwa machozi tu. Kama nitaendelea kumkatalia nina shaka huenda akatumia nguvu”.

Aladdin alimliwaza mkewe, kisha akaondoka maramoja. Alibadilishana nguo na mtu wa kwanza kukutana naye mjini, na alinunua unga na kurudi nao kwa mkewe, ambaye alimfungulia mlango na kuingia ndani. “aladdin alimwambia mkewe; “Vaa nguo zako nzuri sana, mpokee mchawi kwa tabasamu, mfanye aamini kuwa umenisahau kabisa mimi. Mualike chakula cha usiku ale nawe, na useme kuwa unatamani kuonja mvinyo wa nchi yake hii. Atatoka kwenda kutafuta mvinyo, wakati akiwa ameondoka nitakwambia cha kufanya”.
Bintisultani alimsikiliza kwa umakini mkubwa mumewe, baadae Aladdin aliondoka na Bintisultani alijiandaa vizuri kama alivyoambiwa. Alivaa mkanda wake na ushungi ulionakshiwa kwa almasi, kisha alijitazama kwenye kioo na kujiona ni mrembo kupita kiasi.

Alimpokea mchawi na kumwambia; “nimeshaamua kwamba, kwa kuwa Aladdin amekufa na machozi yangu hayatomrudisha, sitaomboleza tena, hivyo nimekualika ule chakula cha usiku nami, lakini nimechoka mvinyo wa china, ningependa nionje ladha ya mvinyo wa afrika”. Mchawi haraka aliondoka kwenda kutafuta, na Bintisultani aliweka ule unga aliopewa na Aladdin kwenye kikombe chake.

Mchawi aliporudi, Bintisultani aliomba amiminiwe mvinyo kwenye kikombe chake, kisha wakabadilishana kikombe na mchawi kama alama ya mapenzi. Kabla ya kunywa ule mvinyo, mchawi alianza kusifu urembo wa Bintisultani, lakini Bintisultani alimkatisha kwa kusema; “Acha ninywe kwanza, na utaniambia hiko utakacho baadae”.
Bintisultani alijifanya kama anakunywa vile, wakati huo mchawi alikunywa mvinyo wote na kuanguka chini akiwa kapoteza maisha.

Bintisultani alimfungulia mlango Aladdin na kumkumbatia kwa nguvu, lakini Aladdin alimtoa kwanza na kumuomba amuache kidogo kwasababu ana mambo mengi ya kufanya kwa muda ule. Alikwenda kwa yule mchawi aliyekufa na kuichukua taa, kisha alimtaka Jini airudishe ile Kasri china. Hili lilifanyika, na Bintisultani akiwa chumbani kwake alihisi mitikisiko miwili midogo, na alijikuta kafika china tayari.

Sultani akiwa amekaa kwenye kiti huku akiomboleza kupotea kwa binti yake, alinyanyuka na kutazama nje, alifikicha macho yake kwani ile Kasri ilirudi palepale kama mwanzo! Aliharakisha kwenda, na Aladdin alimpokea ukumbini huku Bintisultani akiwa ubavuni kwake. Aladdin alimwambia Sultani yaliyotokea ns kumuonyesha mwili wa yule mchawi ili apate kuamini.

Sultani alitangaza siku kumi za kusherekea tukio lile, na ilionekana kwamba Aladdin ataishi maisha yake yote kwa amani, lakini haikuwa hivyo. Yule mchawi wa kiafrika alikuwa na ndugu yake, ambaye alikuwa ni mbaya zaidi kuliko kaka yake. Alisafiri mpaka china ili kulipa kisasi kwa kifo cha kaka yake, alikwenda kumtembelea mwanamke mtakatifu aliyeitwa Fatuma, aliona ndiye anafaa kumtumia.

Aliingia ndani ya nyumba ya Bi Fatuma na kuchoma kisu kifuani. Alichukua mavazi ya Fatuma na kuvaa yeye, alijipaka rangi usoni kama Fatuma, kisha akamuua kabisa ili asije kuhadithia yaliyotokea. Kisha yule ndugu wa mchawi alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye Kasri ya Aladdin, na watu wote pale walidhani ni yule mwanamke mtukufu, walimzunguka na kubusu mikono yake huku wakiomba baraka zake.

Alipofika karibu na Kasri, kulikuwa na kelele mpaka Bintisultani alimwambia kijakazi wake achungulie dirishani kujua nini kinaendelea huko nje. Kijakazi alisema ni mwanamke mtukufu, akitibu watu kwa kuwagusa. Jambo lile lilimvutia Bintimfalme, ambaye alikuwa akitmani siku moja Fatuma amtembelee, hivyo aliagiza kijakazi wake amuite. Baada ya kuingia ndani yule mchawi alifanya maombi ya uwongo kwa Bintimfalme kumuombea afya njema.

Alipomaliza yule mchawi maombi yake, Bintisultani alimtaka akae na kumuomba aendelee kuishi pale. Fatuma wa uwongo, ambaye hakumtakia mema Bintisultani, alikubali, lakini alishusha nikabu yake kwa hofu ya kugundulika. Bintisultani alimuonyesha ukumbi, na kumuuliza anafikiria nini.

Alisema Fatuma wa uwongo; “Ni mzuri sana, lakini kwa mawazo yangu naona hapa kunahitajika kitu kimoja tu”, “Kipi hiko” aliuliza Bintisultani. “Kama yai la roki lingening’inizwa katikati ya hii kuba, ingekuwa ni maajabu ya dunia” alijibu yule mchawi. Baada ya hili, Bintisultani hakufiria kitu chochote zaidi ya yai la roki.

Aladdin alipotoka kuwinda alimkuta mkewe mnyonge, aliomba kujua kitu gani kinamsibu mkewe, Bintisultani alisema kwamba uzuri wote mle ndani umeharibiwa kwa kukosekana yai la roki pale katikati ya kuba. Aladdin alisema; “Ni hilo tu! Basi utafurahi muda si mrefu”, alikwenda kuisugua taa na Jini akatokea na kumpa amri ya kuleta yai la roki.

Jini alitoa kelele na sauti ya kutisha mpaka ukumbi ukatikisika. “Mpumbavu, hivi haya yote niliyokufanyia hayatoshi, mpaka unaniamuru nimlete Bwana wangu na nimning’inize katikati ya hii kuba? Wewe, mke wako na hii Kasri mnastahili kuchomwa na kuwa majivu. Lakini ombi hili halijatoka kwako, ila limetoka kwa ndugu wa yule mchawi wa kiafrika ambaye wewe umemuua. Kwa sasa yupo ndani ya kasri yako akijifanya mwanamke mtakatifu - ambaye ameshamuua. Yeye ndiye ambaye ametia wazo hilo kwenye kichwa cha mkeo. Chukua tahadhari, kwasababu anataka kukuua” baada ya kusema hayo, Jini alipotea.

Aladdin alirudi kwa mkewe na kumwambia kuwa kichwa kinamuuma, hivyo aliomba Fatuma mtukufu aje kumponya. Lakini mchawi alipomkaribia tu, Aladdin alitoa kisu chake haraka na kumchoma nacho moyoni. “Umefanya nini tena jamani? Umemuua mwanamke mtakatifu!!” alipiga kelele Bintisultani. “Sio huyo, huyu ni mchawi mshenzi tu” alijibu aladdin.

Aladdin alimwambia mkewe jinsi alivyodanganyika. Baada ya tukio lile Aladdin na mkewe waliishi kwa amani. Aladdin alirithi kiti cha Sultani baada ya Sultani kufariki na aliongoza kwa miaka mingi sana, huku akiacha nyuma yake msururu mrefu wa wafalme.

MWISHO
 
ALADDIN NA TAA YA AJABU --- SEHEMU YA KWANZA (1)​

ALADDIN NA TAA YA AJABU

Hapo zamani kabisa, aliishi mshonaji masikini, ambaye alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Aladdin, ambaye alikuwa ni mzembe na mvivu kabisa, asiyependa kufanya kazi yoyote isipokuwa kucheza mitaani na watoto wenzake wavivu kama yeye.

Tabia hii ya mwanawe, ilimhuzunisha sana mshonaji, mpaka ikapelekea apate ugonjwa ambao ulisababisha kifo chake. Ingawa mama yake Aladdin alifanya kila aliloweza, alilia na kufanya kila aina ya maombi, lakini mwanawe hakubadilika, aliendelea na tabia yake ileile.

Siku moja akiwa anacheza mitaani kama kawaida yake, alikuja mgeni mmoja na kumuuliza umri wake, na kama yeye hakuwa mtoto wa Mustafa mshonaji. Alijibu Aladdin; “Ndiye mimi, lakini baba yangu alishakufa muda mrefu uliopita”. Baada ya kusikia hili, yule mgeni ambaye alikuwa ni mchawi maarufu wa kiafrika, alimkumbatia Aladdin na kumbusu, huku alikwambia; “Mmi ni baba mdogo wako, nilikujua kutokana na kufanana kwako na kaka yangu. Nenda kwa mama yako na umwambie kwamba nakuja”.

Aladdin alikimbia kwenda nyumbani, ambako alimwambia mama yake habari za baba yake mdogo. “Kweli, mwanangu. Baba yako alikuwa na ndugu yake, lakini siku zote nilidhani kuwa alishafariki” alisema Mama yake Aladdin. Hata hivyo aliandaa chakula cha usiku, na kumtaka Aladdin akamtafute baba yake mdogo, ambaye alikuja akiwa na mvinyo na matunda.

Alipofika pale, alianguka chini na kubusu sehemu ambayo Mustafa alikuwa akipenda kukaa, huku akimtaka Mama yake Aladdin asishtuke kwa kutomuona hapo kabla, kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kwa muda wa miaka arobaini. Kisha alimgeukia Aladdin, na kumuuliza alikuwa akifanya biashara gani, ambapo Aladdin aliinamisha kichwa chini, na Mama yake alianza kulia.

Baada ya kujua kwamba Aladdin alikuwa ni mvivu na hajui kufanya biashara yoyote, alitaka kumchukua na kumfungulia duka ili auze bidhaa. Siku iliyofuata, yule baba mdogo alimnunulia Aladdin, nguo mpya nzuri, na alimchukua na kwenda kutembea nae mjini, aklimuonyesha maeneo mbalimbali, ilipofika usiku alimrudisha kwako, ambapo Mama yake alifurahi sana kumuona mwanawe akiwa yupo vizuri.

Siku iliyofuata, yule mchawi alimchukua Aladdin na kumpeleka kwenye bustani nzuri sana iliyokuwa mbali kidogo na mji. Walikaa chini kwenye chemchem, na yule mchawi alitoa keki kutoka kwenye mfuko wake, aliikata kati na kipande kumpatia Aladdin. Waliendelea kusafiri mpaka wakafika milimani. Aladdin alichoka sana na aliomba warudi.

Mchawi hakutaka warudi, hivyo aliendelea kumlaghai Aladdin kwa hadithi tamu tamu ili safari yao iendelee. Mwisho walifika kwenye milima miwili iliyotenganishwa na bonde jembamba.
Mchawi alimwambia Aladdin; “Tutaishia hapa, hatutaendelea na safari, nitakuonyesha kitu kizuri. Kusanya kuni niwashe moto”. Aladdin alikusanya kuni na mchawi aliwasha moto. Baada ya moto kuwaka, yule mchawi alitoa unga mweupe na kuutupia kwenye ule moto huku akitamka maneno ya kichawi. Ardhi ikatikisika kidogo na ikafunguka, lilionekana jiwe kubwa lenye umbo la mraba likiwa na mshikio katikati.

Aladdin alijaribu kukimbia lakini mchawi alimkamata na kumzaba kibao kilichofanya aanguke chini. Aladdin aliongea kwa upole uliojaa woga; “Nimefanya nini Baba mdogo. Mchawi alijibu kwa upole nae; “Usiogope kitu, nitii mimi. Chini ya jiwe hili kuna hazina ambayo ni ya kwako, na hakuna yeyote awezaye kuigusa, hivyo lazima ufaye kama ninavyokuambia”.

Baada ya kusikia neno ‘hazina’, woga ulimuondoka Aladdin, aliishika kwa nguvu pete kama alivyoambiwa, huku akitaja majina ya Baba na Babu yake. Jiwe lilikuja juu na kufunguka, ngazi zilionekana. Mchawi alimwambia Aladdin; “Nenda, chini kabisa ya hizo ngazi utaona mlango upo wazi ambazo utakupeleka kwenye kumbi kubwa tatu. Kunja kanzu yako na upite bila kugusa kitu chochote au utakufa. Hizo kumbi zinaongoza kwenye bustani ya miti ya matunda matamu. Endelea kwenda mpaka ufike kwenye pembe ya varanda ambapo kuna taa ya chemli inayowaka. Mwaga mafura yake na uniletee”.

Mchawi alivua pete yake na kumpa Aladdin, na kumtakia kila la kheri. Aladdin alikutakila kitu kipo kama mchawi alivyosema, alichuma baadhi ya matunda na kuchuka ile taa, alirudi na kufika kwenye mlango wa pango. Mchawi alimpigia kelele kuwa aharakishe; “Fanya haraka unipe taa hiyo”. Aladdin alikataa kumpa ile taa, akitaka mpaka atoke nje ya pango lile.

Mchawi alishikwa zaidi na hasira, akamwaga unga mwingine kwenye moto na kutamka maneno yake ya kichawi, lile jiwe lilirudi na kujifunga kama mwanzo. Mchawi aliondoka kutoka Fursi daima, jambo lile lilimuonyesha Aladdin kuwa yule hakuwa Baba yake mdogo, ila ni mchawi tu ambaye alisoma kwenye vitabu kuhusu taa ya ajabu, ambayo ingemfanya yeye kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani.

Ingawa ni yeye (mchawi) tu ndiye aliyejua taa ilipo, lakini ilikuwa ni lazima aipokee kutoka kwenye mikono ya mtu mwingine. Alimchagua mpumbavu Aladdin kwa jambo hili, akiazimia kupata taa na kumuua Aladdin baada ya hapo.

Kwa muda wa siku mbili, Aladdin aliendelea kubaki gizani, akilia na kujuta. Mwisho alikuwa akisugua mikono kwa maombi, katika kufanya aliisugua ile pete, ambayo mchawi aliisahau kuichukua kutoka kwake. Kwa haraka alitokea Jini mkubwa anayetisha sana, akasema; “Unataka nini kwangu? Mimi ni mtumwa wa pete na nitakutii na kufanya chochote utakacho”.

Bila woga Aladdin alijibu; “Nitoe kwenye hii sehemu!”. Ardhi ikajifungua, na Aladdin alijikuta yupo nje. Baada ya kukaa sawa, alianza kurudi nyumbani kwao. Alipofika, alimwambia Mama yake kilichotokea, alimuonyesha taa na matunda, ambayo kumbe yalikuwa ni madini kuhalisia (sio matunda).

Aladdin aliomba chakula kwa Mama yake. Mama alijibu; “Aah!! Mwanangu, hamna kitu leo. Lakini nimechuma pamba kidogo, nitakwenda kuuza na kununua chakula”. Aladdin alimwambia Mama yake ahifadhi pamba yake, badala yake atakwenda yeye (Aladdin) kuuza ile taa. Kwa kuwa ilikuwa chafu sana,Mama yake alianza kuisugua ili iwe safi na aiuze walau kwa bei ya kuridhisha kidogo.

Wakati akiendelea kuisugua ile taa, ghafla alitokea Jini na kuuliza kitu gani anataka. Mama alizimia, lakini Aladdin aliwahi na kusema; “Niletee chakula”, Jini alileta bakuli, sahani kumi na mbili zilizojaa nyama nzuri, vikombe viwili na chupa mbili za mvinyo, vyombo vyote vilikuwa vya fedha.

Mama alipozinduka alisema; “Vyakula hivi vizuri vimeletwa na nani?”. Aladdin alijibu; “Mama usiulize, wewe kula tu”. Walikula, mpaka ilipofika mchana, Aladdin alimwambia Mama yake kuhusiana na taa. Mama alimuomba Aladdin auze ile taa na asijishughulishe na Majini. Aladdin alisema; “Hapana, lazima tuitumie hii taa na hii pete vilevile, ambayo itakuwa kidoleni kwangu kila siku”.

Walipomaliza kula vyakula vyote vilivyoletwa na Jini, Aladdin aliuza moja ya sahani zake za fedha na nyingine mpaka zikaisha zote. Kisha aliendelea kumuita Jini, ambaye alimpatia sahani nyingine, walikula chakula na sahani kuuza. Waliendelea kuishi vile kwa miaka mingi.

Siku moja Aladdin alisikia amri kutoka kwa Sultani, ikisema kwamba kila mmoja anatakiwa asitoke nyumbani kwake na afunge milango na madirisha wakati Bintisultani akienda na kurudi kutoka kuoga. Aladdin alishikwa na tamaa haswa ya kuuona uso wa Bintisultani, kitu ambacho kilikuwa ni kigumu, kwasababu muda wote aliufunika uso wake kwa nikabu.

Aladdin alikwenda kujificha nyuma ya mlango wa bafu, na alikuwa akichungulia kupitia kitobo kidogo. Bintisaltani alipandisha nikabu yake alipokuwa akiingia, alikuwa ni mrembo sana kiasi kwamba Aladdin alijikuta akimpenda na kuzama palepale. Aladdin alirudi nyumbani kwao akiwa amebadilika sana mpaka Mama yake akaogopa labda huenda mwanae kapata tatizo.

Aladdin alimwambia Mama yake kwamba amempenda Bintisultani sana kiasi kwamba hatoweza kuishi bila yeye na anahitaji kumuowa. Mama yake aliposikia hili, aliangua kicheko kikubwa, lakini Aladdin alimuomba Mama yake aende kwa Sultani akafikishe ombi lake. Mama alichukua kitambaa na kuweka ndani yake yale matunda ya kichawi kutoka bustani ya kichawi, ambayo yaling’aa kama vito vizuri vya rhamani. Mama alibeba vitu vile ili walau amfurahishe Sultani.

Mama alitoka na kuelekea Ikulu, Mshauri mkuu na Wakuu wengine wa serikali waliingia kwenye ukumbi wa mkutano. Wakati huo Mama yake Aladdin naye aliingia ukimbini pale na kusimama sehemu ya mbele akiangalia kiti cha enzi cha Sultani. Hatahivyo, Sultani hakumzingatia (hakumtilia maanani).

Mama aliendelea kwenda pale kila siku kwa muda wa wiki nzima. Pindi mkutano ulipoisha kwenye siku ya sita, Sultani alimuuliza Mshauri wake; “Huwa ninamuona mwanamke fulani kwenye chumba cha mikutano kila siku akiwa amebeba kitu kwenye kitambaa. Nataka umuite, ili nijue anahitaji kitu gani”.

Siku iliyofuata, kwa ishara ya Mshauri mkuu, Mama yake Aladdin alikwenda kwenye kiti cha enzi na kubaki akiwa amepiga magoti huku macho ameinamisha chini mpaka Sultani alipomwambia; “Inuka ewe mwanamke mwema na uniambie unataka nini”. Mama alisita kidogo, hivyo Sultani aliondoa watu wote isipokuwa Mshauri wake, na kumuomba azungumze kwa uhuru, huku akimuahidi kutochukizwa na kusamehe kwa chochote atakachozungumza.

Mama alimueleza Sultani kuhusu suala la mwanawe (Aladdin) kumpenda sana Bintisultani. “Nilimuomba sana amsahau” alisema Mama, “Lakini ilishindikana, alitishia kufanya kitu kibaya kama ningekataa kuja kukuambia kuhusu yeye kutaka kumposa Binti yako. Sultani naomba unisamehe mimi na mwanangu”.

Sultani kwa upole alimuuliza yule Mama kitu gani amebeba kwenye kitambaa, Mama alifungua kitambaa chake na kumuonyesha Sultani vile vito vya thamani kubwa alivyobeba. Sultani alipigwa na butwaa, akamgeukia Mshauri wake na kumwambia; “Ulisema nini? Hivi sihitajiki kumuoza Binti yangu kwa mtu ambaye anamthamini kwa gharama kama hii?”.

Mshauri, ambaye alikuwa akitaka Bintisultani aolewe na mwanaye, alimuomba Sultani aendelee kusubiri kwa miezi mitatu, huku akiwa na tumaini kwamba mwanaye atamletea Sultani zawadi za gharama kubwa kuliko zile. Sultani alikubaliana na jambo lile, na kumwambia Mama Aladdin kwamba ingawa yeye amekubali na jambo la ndoa, lakini Mama Aladdin hatakiwi kuja tena kwa Sultani mpaka ipite miezi mitatu.

Aladdin aliendelea kusubiri kwa karibu miezi mitatu, lakini baada ya miezi miwili kupita, Mama Aladdin alikwenda mjini kununua mafuta, alimkuta kila mtu akifurahi, aliuliza ni kitu gani kinaendelea. “Hujui!! Mtoto wa Mshauri mkuu anamuoa Bintisultani usiku wa leo?” hilo ndio lilikuwa jibu.

Mama Aladdin akiwa kaishiwa pumzi, alirudi nyumbani haraka na kumwambia Aladdin habari zile, alipatwa na mshtuko mkubwa, lakini alitulia na baadae kidogo aliikumbuka taa yake. Aliisugua na Jini alitokea na kusema; “Unataka nini?”. Aladdin alijibu; “Sultani kama unavyomjua, amevunja ahadi yake kwangu, na amamuoza Binti yake kwa mtoto wa Mshauri. Amri yangu ni kwamba, usiku wa leo uwalete hapa bwana na bibiharusi”. “Ninatii, Bwana wangu” alisema Jini.

Aladdin alikwenda chumbani kwake,ambapo usiku ule, Jini alileta kitanda kilichowabeba Bintimfalme na mumewe. Aladdin alimwambia Jini; “Mchukue huyu bwanaharusi mpya umpeleke nje kwenye baridi, kisha urudi asubuhi”. Jini alimchukua mtoto wa Mshauri mkuu na kumpeleka nje huku kitandani akibaki Aladdin na Bintisultani. Aladdin alimwambia Bintisultani; “Usiogope kitu, wewe ni mke wangu, niliyeahidiwa na Baba yako asiyetenda haki, na hautadhurika na chochote”. Bintisultani aliogopa sana na usiku ule ulikuwa ndio usiku mgumu kwenye maisha yake, wakati akiwa amelala pembeni yake tena akikoroma sana.

Muda ulipofika, Jini alirudi akamchukua bwanaharusi kutoka kwenye baridi na kumlaza kitandani, kisha alikirudisha kile kitanda ikulu. Sultani alikwenda kumsalimia Binti yake, mtoto wa Mshauri alijificha, wakati Bintisultani hakuweza kusema neno lolote na alikuwa ni mwenye huzuni sana.

Sultani alipoona hali ile, alimtuma mkewe akazungumze na mwanawe; “Vipi mwanangu hauzungumzi na Baba yako? Nini kimetokea?”. Bintisultani alishusha pumzi nzito na kumwambia Mama yake, wakati wa usiku, kitanda chao kilipelekwa kwenye nyumba ngeni, na kilichotokea huko. Mama yake hakumuamini, lakini alimuomba aichukulie ile kama ni ndoto mbaya tu.

Usiku uliofuata, kitu kile kile kilitokea tena, na asubuhi iliyofuata kwa kitendo cha Bintisultani kukataa kuongea na Sultani, Sutani alitishia kumkata kichwa. Bintisultani kwa kuogopea maisha yake, alisema yaliyotokea yote kwa Sultani, na kumwambia kama ataona ni uongo basi amuulize mtoto wa Mshauri mkuu (ambaye ndiye mume wa Bintisultani).

Sultani alimwambia Mshauri wake amuulize mtoto wake, ambaye alisema ukweli wote, na kuongeza kwamba, ingawa alimpenda sana Bintimfalme, lakini yupo ni bora kwake kufa kuliko kupitisha usiku mwingine wa kutisha na kuomba aachanishwe na Bintimsultani. Ombi la mtoto wa Mshauri mkuu lilikubali na hivyo kuachana na Bintisultani.

Pindi miezi mitatu ilipoisha, Aladdin alimtuma Mama yake kwenda kumkumbusha Sultani kuhusu ahadi yake. Sultani alipoona Mama yake ni masikini sana, alijihisi uzito kutekeleza ahadi yake, alitaka ushauri kutoka kwa Mshauri wake, alimshauri Sultani kuweka mahari kubwa sana ambayo hakuna mtu yeyote atakayeweza kuimudu.

Sultani alimgeukia Mama Aladdin na kumwambia; “Mwanamke mwema, Sultani lazima akumbuke ahadi yake, na mimi nitaikumbuka ya kwangu, lakini mtoto lazima aniletee mabakuli arobaini ya dhahabu yaliyojaa vito vya thamani, yakiwa yamebebwa na watumwa arobaini weusi, wakiwa wamevaa mavazi ya thamani. Mwambie mwanao nasubiri jibu lake”.

Mama Aladdin alirudi nyumbani akihisi tayari wameshindwa. Alifikisha ujumbe kwa Aladdin na kumwambia; “Ametoa muda mrefu wa kusubiri jibu kutoka kwako”. “Sio muda mrefu Mama, kama unavyofikiria” alijibu Aladdin, “Nitafanya jambo kubwa zaidi ya hilo kwa ajili ya Bintimfalme”.

Aladdin alimuita Jini, na ndani ya muda mfupi walifika watumwa themanini na kujaa nyumba nzima mpaka kwenye bustani. Aladdin aliwataka waelekee ikulu, wawili kwa wawili, wakiongozwa na Mama yake. Walikuwa na wamevaa ya gharama sana, wakiwa na vito vya thamani kwenye mikanda yao, huku wakiwa mabakuli ya dhahabu vichwani mwao, watu walikusanyika kwa wingi kuwaangalia.

Waliingia ikulu, na baada ya kupiga magoti mbele ya Sultani, walisimama nusu mduara kuzunguka kiti cha enzi, wakati huo Mama yake Aladdin aliwatambulisha kwa Sultani. Sultani hakusita tena, ila alisema; “Mwanamke mwema, rudi na umwambie mwanao kwamba ninamsubiri kwa mikono mikunjufu kabisa”.

Mama hakupoteza muda kwenda kumwambia Aladdin na kumtaka afanye haraka. Lakini Aladdin kwanza alimuita Jini na kumwambia; “Nahitaji kuoga maji yanayonukia, farasi mzuri kuliko wa Sultani, watumwa ishirini. Pia nahitaji watumwa sita wakiwa na mavazi ya gharama wakumsindikiza Mama yangu, na mwisho nahitaji vipande elfu kumi vya dhahabu vikiwa ndani mikoba kumi”. Vitu vyote hivyo vikatokea palepale.

Aladdin alipanda farasi wake na kupita mitaani, watumwa wake walikuwa wakirusha dhahabu huhu na huko wakati wanakwenda. Wale waliocheza naye utotoni, hawakumjua kabisa, alikuwa amependezac sana. Sultani alipomuona Aladdin akija, alishuka kwenye kiti chake cha enzi ili kumlaki, na kumuongoza mpaka kwenye ukumbi ambako kuliandaliwa sherehe kubwa, huku Sultani akiwa ameazimia kumuoza Binti yake kwa Aladdin siku ileile.

Lakini Aladdin alikataa kuoa siku ile na kusema; “Lazima nijenge Kasri linaloendana na Bintisultani”. Baada ya kusema vile Aladdin aliondoka. Alipofika nyumbani alimwambia Jini; “Nijengee Kasri kubwa lenye kunakshiwa kwa marumaru na mawe mengine ya thamani. Katikati ya Kasri kujengwe kuba, kuta nne za dhahabu na fedha, kila upande liwe na madirisha sita, isipokuwa moja, liachwe likiwa halijamaliziwa matengenezo yake, hayo madirisha yapambwe kwa almasi na yakuti. Lazima kuwe na farasi, wachungaji wake na watumwa”.

Siku iliyofuata, kazi ya kujenga Kasri ilikuwa imeisha na Jini alimchukua Aladdin na kumpeleka kumuonyesha, na kulitandikwa kapeti kutoka kwenye Kasri ya Aladdin mpaka kwa Sultani. Mama Aladdin alivaa vizuri, na kuanza safari ya kuelekea ikulu akiwa na watumwa wake, huku Aladdin akimfuata Mama yake kwa nyuma akiwa juu ya farasi.

Sultani alipeleka wanamuziki wakiwa na matarumbeta na ngoma kwenda kuwapokea. Mama Aladdin alipelekwa kwa Bintisultani, ambaye alimsalimia kwa heshima kubwa sana. Usiku Bintisultani alimuaga baba yake, na kuanza safari kuelekea kwenye Kasri ya Aladdin akiwa na Mama yake huku akifuatwa na watumwa mia. Bintisultani alifarishwa alifurahishwa na muonekano wa Aladdin, ambaye aliwahi kumpokea.

“Bintisultani, ulaumu uzuri wako kwa vitendo vyangu kama nitakuwa nimekuudhi” alisema Aladdin. Bintisultani alimwambia kwamba, kwa kule kumuona tu, basi amekubaliana na baba yake kwa moyo wote juu ya jambo lile la ndoa.
Mkuu, kwa heshima na taadhima tafadhali sana naomba uni-PM pdf ya hii kitu aisee.
 
Alfu lela u lela. Usiku wa siku elfu moja na moja.
 
Duu kitabu hiki tulikuwa tumasomewa na Mwl darasa la nne badala ya kucheza cheza Mwl anakuja kutusomea hadithi, R.I.P Mwl Nswima.
Asante kwa kutukumbusha ya kale dhahabu.
 
Mwl Nswima!
Ilikua ni shule gani mkuu, kama hautajali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom