Al-Shabab yaua polisi Kenya

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
al-shababu-pic-data.jpg


Wapiganaji wa kundi la kigaidi Al-Shabab wameshambulia gari la polisi mashariki mwa Kenya na kuwaua maofisa wawili na raia mmoja wakidai kuishinikiza Kenya kuondoa vikosi vyake kutoka kwa ujumbe wa kulinda amani wa AU nchini Somalia.

Kwa mujibu wa kituo cha habari ‘Aljazeera’ wameeleza gari hilo aina ya lori lilikuwa likisafiri kutoka kambi ya Hayley Lapsset kuelekea mji wa Garissa, kilomita 120 kutoka mpaka wa Somalia, wakati lilipogonga kifaa cha kulipuka, hii ni kulingana na taarifa ya polisi.

Wanaeleza wapiganaji hao walirusha guruneti la kurushwa kwa roketi kwenye gari hilo na kujihusisha na mapigano makali ya moto, polisi walisema.

Redio Andalus ya Al-Shabab ilisema katika matangazo yake, watu waliokuwa na silaha waliwaua wanajeshi wawili wa kikosi cha usalama cha Kenya na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulio lililo tokea mpakani mwa Somalia.

Kundi hilo liliua watu 166 katika Chuo Kikuu cha Garissa mwaka wa 2015, na 67 katika maduka makubwa jijini Nairobi mwaka 2013, lakini mara kwa mara na ukali wa mashambulizi ya al-Shabab nchini Kenya umepungua katika miaka ya hivi karibuni.

Kundi hilo lenye mafungamano na al-Qaeda linaendelea kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka kuishinikiza Kenya kuondoa majeshi yake kutoka kwa kikosi cha kulinda amani kilichopewa mamlaka na Umoja wa Afrika nchini Somalia.

Al-Shabab imekuwa chini ya shinikizo nchini Somalia tangu Agosti wakati Rais Hassan Sheikh Mohamud alipoanza mashambulizi dhidi yao, akiungwa mkono na Marekani, kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) na wanamgambo washirika wa eneo hilo.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom