Al-Shabab washambulia kambi ya Jeshi la Somalia

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab nchini Somalia wamesema wameshambulia na kuteka kambi ya wanajeshi wa Somalia karibu na mji wa Mogadishu.

Kundi hilo linasema lilifanikiwa kudhibiti kambi ya mafunzo ya wanajeshi ya Lanta-Buro, kilomita 40 magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu baada ya mapigano ya karibu dakika 40.

Wanasema waliwaua wanajeshi 73 na pia kuteka magari 10 wakati wa shambulio hilo.

Wakazi wamethibitisha kwamba walisikia milio ya risasi kwa saa kadha usiku wa kuamkia leo.

Kambi hiyo imekuwa ikitumiwa na majeshi ya Taifa ya Somalia.

Serikali ya Somalia kufikia sasa haijatoa taarifa yoyote ramsi kuhusu shambulio hilo.

Kamanda mmoja wa jeshi hilo amesema kwamba wapiganaji hao walikabiliwa na kuzidiwa nguvu. Amesema wapiganaji waliotoroka wanaandamwa.

Wapiganaji wa al-Shabaab waliondoka eneo la Lanta-Buro mwaka 2012 bila mapigano, baada ya kukabiliwa maeneo mengine na wanajeshi wa Somalia na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

Eneo hilo linapatikana kilomita 10 pekee kutoka mji wa Afgoye, jimbo la Lower Shabelle.


Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom