Al-Shabab wakata vichwa watu saba Msumbiji

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
9,610
Reaction score
20,436
Maputo, Msumbiji. Washambuliaji kadhaa Jumanne waliua watu saba kwa kukata vichwa vyao kwa mapanga na kuchoma nyumba zaidi ya 10 Kaskazini mwa nchi, eneo ambalo lilikumbwa na shambulizi kama hilo hivi karibuni.

pic+msumbiji.jpg

Jimbo la Cabo Delgado, ambalo linatarajiwa kugeuka kuwa makao makuu ya uzalishaji gesi asilia baada ya ugunduzi wa hivi karibuni kuonyesha matumaini, limekuwa likishuhudia mashambulizi ya mauaji dhidi ya vikosi vya usalama na raia tangu Oktoba mwaka jana.

"Wahalifu walitumia mapanga kuua watu saba. Tunafikiri kikundi hiki ni sehemu ya kile kilichoua watu 10 kwa kukata vichwa Mei 27," msemaji wa polisi Inacio Dina aliliambia shirika la AFP akirejea shambulizi la mwezi uliopita katika jimbo hilo.

"Washambuliaji, Jumanne alfajiri, walichoma moto nyumba 164 na waliharibu magari manne walipofanya shambulizi katika kijiji cha Naude wilaya ya Macomia," alisema.
Washambuliaji ambao wenyeji na maofisa wanadai kuwa ni "al-Shabab", hawana uhusiano wowote na wale wa Somalia wanaotumia silaha na jina hilo hilo.

Baada ya tukio la awali polisi waliongezwa katika eneo hilo kuimarisha usalama.
Dina alidokeza kuwa kikundi hicho kinaweza kuwa na uhusiano na “waasi” tisa waliouawa na vikosi vya usalama mwishoni mwa wiki waliogundulika kuwa na bunduki za kivita na nyaraka zilizoandikwa kwa Kiarabu.
"Kundi hili limegawanyika sana katika vikundi vidogo ambavyo vinajaribu kukabiliana na vishindo vya mashambulizi ya polisi,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Serikali ya Msumbiji idhibiti hao magaidi haraka sana. Usipoziba ufa utajenga ukuta. Wajifunze kutokana na yale yaliyotokea Nigeria. Wasicheke na hao "Makafiri".
 
Kuna jamaa alisema jwtz waliwamaliza hao watu Malawi.. Sina uhakika kama nmemquote vizuri.
 
Aiseee..."" Wanasemaga dunia sio mbaya ......................!!!?
 
Tuzidi kuishukuru serikali ya tanzania kukomesha tabia chafu zilizotaka kujitokeza kanda ya kusini mashariki.
 
Kama kweli hao ni Al-shabab basi ni hatari maana naona bokoharam Nigeria kama wameshanyoosha mikono Juu..

Alshabab,bokoharam,Seleka dawa yao ndogo tu Anti balaka ndio mwisho wa matatizo,muarobaini wa hawa viumbe ni anti Balaka.

Anti balaka wakikamata kiumbe wanakatakata/chalaza mapanga kisha wanatafuna nyama yake ikiwa mbichi,hebu imagine watu wanakutafuna ukiwa hai Seleka nadhani walipata fundisho vyema kutoka kwa antibalaka.

Unyama unyama aliyeua auwawe!!!!
 
Maputo, Msumbiji. Washambuliaji kadhaa Jumanne waliua watu saba kwa kukata vichwa vyao kwa mapanga na kuchoma nyumba zaidi ya 10 Kaskazini mwa nchi, eneo ambalo lilikumbwa na shambulizi kama hilo hivi karibuni.

pic+msumbiji.jpg

Jimbo la Cabo Delgado, ambalo linatarajiwa kugeuka kuwa makao makuu ya uzalishaji gesi asilia baada ya ugunduzi wa hivi karibuni kuonyesha matumaini, limekuwa likishuhudia mashambulizi ya mauaji dhidi ya vikosi vya usalama na raia tangu Oktoba mwaka jana.

"Wahalifu walitumia mapanga kuua watu saba. Tunafikiri kikundi hiki ni sehemu ya kile kilichoua watu 10 kwa kukata vichwa Mei 27," msemaji wa polisi Inacio Dina aliliambia shirika la AFP akirejea shambulizi la mwezi uliopita katika jimbo hilo.

"Washambuliaji, Jumanne alfajiri, walichoma moto nyumba 164 na waliharibu magari manne walipofanya shambulizi katika kijiji cha Naude wilaya ya Macomia," alisema.
Washambuliaji ambao wenyeji na maofisa wanadai kuwa ni "al-Shabab", hawana uhusiano wowote na wale wa Somalia wanaotumia silaha na jina hilo hilo.

Baada ya tukio la awali polisi waliongezwa katika eneo hilo kuimarisha usalama.
Dina alidokeza kuwa kikundi hicho kinaweza kuwa na uhusiano na “waasi” tisa waliouawa na vikosi vya usalama mwishoni mwa wiki waliogundulika kuwa na bunduki za kivita na nyaraka zilizoandikwa kwa Kiarabu.
"Kundi hili limegawanyika sana katika vikundi vidogo ambavyo vinajaribu kukabiliana na vishindo vya mashambulizi ya polisi,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Vipi hawawezi kusogea na hapo ' Ntwara ' Mkuu kwa Ndugu zangu kabisa Wamakonde, Wamakuwa, Wayao na Wamwera?
 
Itakua wale masalia wa Rufiji wameenda kumalizia Machungu huko baada ya JW kuwageuza asusa wenzao. Manina zao kupona
 
Tatizo cabo Delgado kuna hiyo gas asilia pia Luna rubi,hao wajanja Fulani wanaotaka kuiba madini na nishati kwahiyo wanaamua kuitengeneza hiyo hofu ili wajipigie pesa
Nalog off
 
Kama kweli hao ni Al-shabab basi ni hatari maana naona bokoharam Nigeria kama wameshanyoosha mikono Juu..

Alshabab,bokoharam,Seleka dawa yao ndogo tu Anti balaka ndio mwisho wa matatizo,muarobaini wa hawa viumbe ni anti Balaka.

Anti balaka wakikamata kiumbe wanakatakata/chalaza mapanga kisha wanatafuna nyama yake ikiwa mbichi,hebu imagine watu wanakutafuna ukiwa hai Seleka nadhani walipata fundisho vyema kutoka kwa antibalaka.

Unyama unyama aliyeua auwawe!!!!
Umeisoma thread lakini au umekurupuka? Hao jamaa hawana uhusiano wowote na All shabaab wamejiita kwa kulipenda jina tu. Yaani kama wewe uamue kujiita Messi wa kwa mtogole kwa kumpenda messi japokuwa hufanani naye kwa vyovyote.
 
Hapana, kama umesoma bandiko langu vizuri nimetanguliza na "kama kweli"

Hivyo hata mimi nilitambua mapema hakuna uthibitisho kamili ya kuwa ni Alshabab.
 
Back
Top Bottom