Al-Shabaab watano wajisalimisha Somalia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Wizara ya habari ya Somalia imetangaza kuwa, wapiganaji watano wa kundi la al-Shabab akiwemo mtaalam mwandamizi wa mabomu wamejisalimisha kwa serikali ya Somalia wiki hii.

Wizara hiyo imesema Bw. Yusuf Ahmed Adow ambaye ni mtaalam wa mabomu wa kundi la al-Shabab amejisalimisha kwa Jeshi la taifa la Somalia SNA kwenye eneo la Gedo, kusini mwa nchi hiyo, na kufanya idadi ya watu waliosaliti kundi hilo kuongezeka hadi watano.

Maofisa wa mikoa ya nchi hiyo wamesema watu hao watakabidhiwa kwenye mamlaka ya Mogadishu.

Tukio hilo limetokea wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la al-Shabab linalojaribu kupinga serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.


Swahili.cri.cn
 
... hawa magaidi wanapoteza muda tu. Huwezi kushindana na serikali halali tena bila support ya umma huku ukiwauwa wananchi kila uchao ukashinda! Haijwahi kutokea duniani.
 
... hawa magaidi wanapoteza muda tu. Huwezi kushindana na serikali halali tena bila support ya umma huku ukiwauwa wananchi kila uchao ukashinda! Haijwahi kutokea duniani.
na serikali ya Somalia ndio inayo 'back/fund' Al Shabaab, niulize kwanini
 
Wawe nao makini maana siku wanajilipua hawataamini inaweza ikawa ndo mbinu yao au kuna kitu wamefuata
 
Kwa style hii wale wenye ndoto ya kuja kuitawala hii dunia, basi wajue ndoto yao itabaki ndoto tu siku zote. Ushenzi hauwezi kuwa juu ya Ustaarabu. Never.
 
Walishamaliza mission yao. Wajinga wataamini ni kweli wamejisalimisha
 
Tandika shaba wote wakafilie mbali halafu iwe siri, huenda wanapeleleza tu wakuda hao
 
Back
Top Bottom