Akutwa amekufa chooni msikiti Kariakoo

Akutwa amekufa chooni msikiti Kariakoo

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamisi Said (49) amekutwa amekufa katika choo cha msikiti wa Idrisa, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, mwili huo umeokotwa katika choo namba 12 cha Msikiti huo uliopo katika mtaa wa Tandamti, wilayani Ilala.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tano usiku na kwamba uchunguzi wa awali haukuonesha kama marehemu alikuwa na majeraha yoyote huku ikisemekana kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.

Hata hivyo, marehemu alikutwa akiwa na vyeti mbalimbali vya hospitali alizokuwa akitibiwa enzi za uhai wake.

Maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana, Ilala wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea kufanywa.

Katika tukio jingine, moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba ya Dickson Gama (48), mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na kusababisha hasara na mamilioni ya fedha.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea juzi saa mbili usiku eneo la Mbezi Beach kwenye ghorofa za BOT, Flat K katika Wilaya ya Kinondoni.

Alisema kuwa moto huo uliteketeza nyumba nzima yenye jumla ya vyumba vitatu viliyopo ghorofa ya pili pamoja na mali zote zilizokuwepo ndani yake.

Alisema kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa uliokuwa unawaka ndani ambao uliunguza godoro na hatimaye kuenea nyumba yote, thamani ya vitu vilivyoungua bado haijajulikana na polisi wanaendelea na uchunguzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom