Kama mtakumbuka hotuba moja ya Mwl akiongelea muungano alisema '' kutenda dhambi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza kula utaendelea kula tu'
Hili la Makonda si geni labda ugeni wake ni namna linavyokaliwa kimya na wahusika
Ugeni wake ni jinsi anavyoungwa mkono 100% hata pale anapopotoka
Turudi katika historia kidogo sana
Makonda akiwa mwenyekiti Chipukizi alijitokeza wazi na kumsema sana Lowassa
Shambulio kama kada halikuwa na tatizo! tatizo ni lugha yake isiyovumilika kirahisi
Makonda akaenda Ubungo Plaza akiwa na kundi la 'wahuni' .
Tunajua kilichotokea kwa Mzee Warioba, Butiku na wengine.
Likaonekana jambo la kawaida kwasababu alisimama na chama
Makonda akatoa kauli ya Polisi wapige tu yeye atajibu. Bila kujali sheria za nchi na leo tunajua ni kwasababu ya ukaribu na mungu, hakuna,ikaonekana kawaida
Makonda majuzi kamshambulia kwa maneno kamanda wa kanda na wenzake wa chini
Hakuna aliyestushwa na ukiukwaji wa juu wa team work na collective responsibility
Hakuna aliyeona ufa alioutia akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa
Makonda kapita Kinondoni kutoa kauli ya 'ukaribu' na mwenyezi mungu ingawa hakuna vitabu vitakatifu vinavyoonyesha mungu akitoa matusi hata alipoudhiwa na wanadamu
Haya ni kwa uchache sana lakini yanalingana na kauli za Mwl ya kula nyama ya mtu
Katika hili kumlaumu Makonda pia ni kosa, hakuna anayemsaidia na hakuna anayeshtushwa. Makonda ni kijana mdogo kiumri na kisiasa, anahitaji malezi
Kwa haya, walezi wake kisiasa wanaomwacha atende atakalo, atukane watumishi, aamuru watu wafanyiziwe atajibu yeye n.k. ndio wanaobeba dhamana.
Wale waliompa fursa hii adhimu ya kutumikia umma na si kuudhihaki ndio wenye dhama ya ima kumweka kitako kama wanadhani anafaa au wamuondoe ili akajifunze kwanza
Nadhani Makonda hana makosa sana, ni yeye kama yeye, wapo wanaopaswa kutusaidia na hao ndio tunwashangaa hadi leo bado hawaoni tatizo