Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,065
22,758
Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda. Hapa yabidi tujiulize kwa nini mpaka dakika hii mteuzi wake hajachukua hatua yoyote kutunusuru raia na kadhia hii?

Najua pia kumetokea si mara moja ama mbili tu Makonda, ameamrisha Jeshi letu la Polisi, kutii amri zake zisizo na uhalali wowote. Bila shaka haya yote yemewezekana kwa sababu Makonda akitamka, mungu katamka. Hii imewajengea wengi taswira kwamba kila anachofanya Makonda kina baraka za aliyemteua ambaye pia ndiye Jemadari Mkuu wa Taifa kikatiba. Sasa kama Makonda ni mungu, Rais Magufuli pia ni moja katika waumini wake?

=======
 
Jamaa ana akili za ajabu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
 
Watu wengine bwaana sasa na ww kwa akili yako umeichukulia cliac kabisa mpaka umeanza kumtangaza jaribuni kuwaza nje ya box acheni kutafacli kwa mtazamo hasi ujui kuwa ww ndio unaemtangaza kuwa ni mungu
 
Hata mitume na manabii hawakuwahi kutamka maneno hata. Heko watu wa Dar es salaam kwa kuwa na Mungu karibu yenu kupitia Makonda.
Mashehe, mapadre na wachungaji katafuteni kazi nyingine Dar sasa wakitaka toba au msaada wa Mungu watapitishia kwa Makonda kwani ndio njia rahisi maana alipo simama yeye hapo hapo ndipo alipo. Hili jambo litangazwe duniani na hakika ulimwengu utafurika hapa kuja kwa Makonda na nchi itanufaika kwa chanzo hicho kipya cha mapato
 
Watu wengine bwaana sasa na ww kwa akili yako umeichukulia cliac kabisa mpaka umeanza kumtangaza jaribuni kuwaza nje ya box acheni kutafacli kwa mtazamo hasi ujui kuwa ww ndio unaemtangaza kuwa ni mungu
Aina yako ya uandishi inaonyesha kiwango cha ukomavu wako kiumri na kiakili.
Hili ni jukwaa lenye watu wazima wengi usiandike hayo mambo yenu ya "cliac"= serious; "kutafacli" kutafakari n.k
Haya tueleze wewe uliyaza nje ya box umepambanua nini huko?
 
Aina yako ya uandishi inaonyesha kiwango cha ukomavu wako kiumri na kiakili.
Hili ni jukwaa lenye watu wazima wengi usiandike hayo mambo yenu ya "cliac"= serious; "kutafacli" kutafakari n.k
Haya tueleze wewe uliyaza nje ya box umepambanua nini huko?
Tusifundishane kuandika maana ukunilipia ada yote kwa yote kama unaamini ndio Mungu basi
 
Subirini tu kanusho. Atasema siyo yeye, na kama ni yeye hajayatamka hayo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…