Akina Mwanyika mbona mpo kimya sana ela zetu za EPA?

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Wakati JK alipounda timu chini ya AG Mwanyika kuwachunguza waliochota mabilioni ya EPA, moja ya adidu za rejea za kamati hiyo ilikuwa ni kutoa taarifa mara kwa mara kupitia vyombo vya habari.
Ni wiki kadhaa sasa zimepita, si mwanyika wala wajumbe wenzake ambao wamejitokeza hadharani kueleza kinachoendelea. Juzi juzi alisema katibu Mkuu Kiongozi kuwa bil 50 zimerejeshwa lakini yeye si mjumbe wa kamati hiyo kwa hiyo hivyo hatuwezi kuichukulia kauli yake kama kauli rasmi ya kamati.
Kwanza yeye alisema ili kuwapendezesha wale mawana wakubwa waliokuwa wanamtembelea bosi wake siku ile.
Mbona mwanyika na wenzako hamtaki kutueleza maendeleo ya uchunguzi wa wizi wa mabilioni yetu wakati tuliahidiwa habari mara kwa mara kutoka kwenu?
msituyeyushe
 
CHADEMA baada ya kuanguka kule Kiteto naona wamepunguza mashambulizi ili wajipange tena upya!

Mnyika dogo upo wapi? Watu wanawaulizia over EPA!
 
Back
Top Bottom