MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,297
Hatuna budi kupongeza jitihada zinazofanywa na serikali sikivu ya CCM pamoja na wadau wengine kuchimba visima vya maji ili wananchi wapate maji safi husuan sehemu za vijijini. Lakini huwa najisikia kutapika kila nikiona watawala na wapambe wao wa kiume na wa kike wakionesha furaha kubwa sana kuwatwisha ndoo za maji akina mama kama sehemu ya uzinduzi wa visima hivyo. Hii ni ishara kwamba hata katika muongo wa pili wa karne ya 21 watawala wetu na sisi sote bado tumegubikwa na fikira mgando kwamba mama aendelee kubeba ndoo ya maji kichwani. Hakuna ishara wala dalili za fikira mbadala kwamba badala ya kubeba kichwani angaa tumuhimize huyu kiumbe atumie mkokoteni wa kusukuma wenye uwezo wa kubeba ndoo mbili au tatu - njia mbadala kama hii inao ufanisi mkubwa kuliko kuendelea na njia ya enzi za mawe. Kwanza itaboresha afya ya mama (na hapa tukumbuke hawa wamama huanza kubeba wakiwa bado wasichana wa miaka 10) na itaokoa muda wake kwa kufanya safari moja badala ya mbili au tatu. Mandhari kama hii ya Mhe Kikwete kumtwisha mama ndoo ya maji imekuwa ni mojawapo ya nderemo na vigelegele vipambavyo zinduzi mbalimbali za visima. Nilifikiri kijana kama Riz1 angekuja na fikira mbadala. Lakini na yeye (kama mwakilishi wa vijana wetu wanaosema huu ndio wakati wao) bado anafanya yale yale ya JK na JKN! Tafakari!

Source: Picha kutoka mjengwablog (Agosti 11, 2014)

Source: Picha kutoka mjengwablog (Agosti 11, 2014)