Akili za watanzania zinapokuwa likizo

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Nimewasikiliza nakuwasoma kwenye maandiko yao baadhi ya wenzetu na kusikitishwa kuwa mtu makini kweli anaweza kuja na agenda rahisi na nyepesi kuwa sifa ya rais ajae awe ni Kijana. Niwaulize wenzangu mniambie kweli kama si agenda ya siri nyuma ya pazia ni nini hiki. Nyerere hakuwahi kuwa Rais wa nchi hii kwa sifa ya Ujana bali kipawa chake kilijitokeza wakati angali kijana na wananchi wakamsalimia kuwa anatosha. Vivyo hivyo kwa wengine. Imetokea katika mataifa mengine dunia kuchagua vijana kuwa viongozi wa nchi zao si kwa sifa ya Ujana bali wamechomoza na vipaji vyao katika siasa na wakachaguliwa kuwa viongozi. Ukiona mtu anasimama jukwaani anawambia Watanzania safari hii ni lazima tumchague kijana huyo amefirisika kisiasa na asipewe fursa hata kidogo ya kusikilizwa kwani analo lake jambo.

Sifa kubwa ya Ujana ni kuwa anaweza kuchacharika na kufanya masaa mengi bila kuchoka lakini udhaifu mkubwa wa vijana ni kukosa busara ya subira wakati wa kufanya maamuzi kwa sababu ya kukosa uzoefu. Experience is the best teacher and mother of informed decisions matokeo ya haya yote ni busara kwa kiongozi. Kiongozi wa nchi hawezi kuchaguliwa kwa vigezo vya kijinsia wala umri ila vyote hivi vinaweza kuwa sifa ya ziada kama wagombea wametoshana katika sifa za msingi za urais.

Kama hatuwalengi watu fulani na kuzima nyota zao kwa kigezo hiki mufilisi basi tuwaache wanaoutamani uraisi waje na agenda zao wataifanyia nini nchi hii na tuwachague kwa hoja zao. Warioba Watu wamemuwekea maneo mdomoni kwa ufafanuzi wao na siamini Zito anaweza kuja na hoja hii nyepesi.
 

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,775
3,136
Sio wtz wote , ila ni wale wenye ubinafsi , wanafikiri kuwa WATAENDELEA kuwa vijana milele, sijui wakiwa hai miaka michache ijayo hoja yao itakuwa ni ipi hasa maana ujana utakuwa sio hoja yao tena .
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom