Akili za Lusinde na Matokeo ya Ubunge Arumeru Mashariki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akili za Lusinde na Matokeo ya Ubunge Arumeru Mashariki!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by PERECY, Apr 2, 2012.

 1. PERECY

  PERECY Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Nawashukuru mliorekodi thread yenye kuonyesha Ndugu Lusinde akikisaidia chama chake katika kampeni Arumeru Mashariki. Nimesikiliza kwa makini, iwapo kila wakati nilijikuta natabasamu, tabasamu lenye maswali mengi ndani yake. Kubwa, nilijiuliza, nasikiliza sauti ya Mbunge Lusinde au naota?

  Kwa kuwa ndani ya JF hakuna mambo yanayoingia bila ushahidi wa kutosha, naridhika kuamini kwamba sikuwa naota, nimesikia matusi toka kwa kiongozi ambaye eti huwa anapewa heshima kama mbunge, mwakilishi wa wananchi wenzetu; maskini wanohitaji kuongozwa na mtu mwenye maono.

  Namwandikia Lusinde: Lusinde kama hutatumia hadhara, na vyombo vya habari kuomba radhi jamii nzima ya waTz - siongelei CHADEMA hapa; namaanisha waTz wote, mpaka watoto wadogo kabisa ambao bado wengine hawajazaliwa - nakutabiria utapata mrejesho mbaya sana katika maisha yako ya uongozi, kutokana na matusi ambayo kinywa chako kimeyaumba na kuyatamka mbele ya jamii, kwa uwazi na bila aibu. Hatutumii uchawi hapa - tunatumia hekima na maono! Narudia kusema, maisha yako ya uongozi hata baada ya uongozi, kama hutatubu na kuomba radhi jamii ya waTz, kwa matusi haya ambayo umeyatamka kwa kudhamiria kabisa ukiwa na akili timamu, kwa ajili tu ya siasa - hakika safari yako itakuwa ngumu!

  Najua wengi hatuna hekima ya kutubu na kuomba samahani kutokana na matendo yetu, tukiamini kufanya hivyo ni kukiri udhaifu. Najua hutaomba samahani Bwana Lusinde. Itakugharimu!

  WanaCCM, kama kweli hamtasikia hili; na kwa kuwa mpo katika hatua ngumu sana, najua hamtataka kulisikia hili; binafsi nina mashaka sana na aina ya viongozi katika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama chenu na hatma yenu.

  Kiongozi wa umma anashabikia kutukana! Kiongozi wa umma anatukana hadharani! Anatukana akifurahi na kutabasamu kama vile anakula chakula kizuri; AJABU HII! Eti hii ni kampeni kukisaidia chama chake kupata ushindi; ajabu hii!

  DHAMBI HII ITAWATAFUNA, HAKIKA!
   
 2. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kama nilisikia alisema kuwa yeye ni kichaa wa kuzaliwa! Mpaka nikasikia mch. Mtikira anataka kumfungulia kesi maana vichaa hawakubaliki bungeni!
  Kwa mtu aliye mzima, mwenye maadili tena anayeamini Mungu hawezi kutamka aliyotamka Lusinde(sipendi kumwita mheshimiwa) hata akiwa peke yake au kimoyo moyo. Ni maneno machafu sana.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa kiasi kikubwa matusi ya huyu bwana ni moja ya chachu ya sababu za ushindi kwa CHADEMA. Wananchi sasa wamewaelewa vizuri MAGAMBA na Sera zao na sasa wanataka tumaini jipya. Japo next week CDM lazima wakuchukulie hatua kwa lugha yako chafu, binafsi nasema asante sana!
   
 4. g

  glojos88 Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana na wewe. Ila mimi naona Chama kinatakiwa kuchukua collective responsibility kutamka hadharani kuwa hakikumtuma na kimeaikitushwa na hayo. Vinginevyo tuna haki ya kuamini kuwa huo ni msimamo wa Chama.
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Elimu yake ni darasa la 5 then akaenda kuwinda ndege kabla ya kuibukia CUF.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  I second this!...Huyu mtu atumie media kuomba msamaha kwa jamii ya Kitanzania, maana obviously hawezi kuiomba msamaha cdm!...Naamini kabisa ushindi wa cdm umechagizwa na kauli zake maana watu hata ambao walikuwa wakimwamini wamekatishwa tamaa na uwezo wake wa kufikiri na kupambanua mambo!
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa ni mbinu ya Nape group kumchafulia Lowassa baada ya kumkata Millya kugombea ubunge wa E.A.!! Wao wanaiita DOUBLE TRAGEDY STRATEGY!! Wake up call kwa Lowassa kuwa huyo ambae hawakukutana barabarani amedhamilia kumtosa! Mark my words.
   
 8. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Sio siri amekitia aibu chama chake na watanzania kwa ujumla especialy wananchi wa jimbo lake! Wanapaswa kumuadabisha!
   
 9. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama mtanzania tena wakawaida sana ningependa kuweka wazi kuwa nina mashaka na aina ya watunga sheria tulionao. Wakati umefika sasa tufanye maboresho ktk vigezo sifa vya mtu kuwa mbunge. Hii itasaidia bunge kuepuka wabunge wadizain ya kina Lusinde a.k.a Lusinde type kutopata upenyo mjengoni kwani ni aibu then ni tishio kwa maendeleo ya taifa!
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Makundi yao yanawaponza!
   
 11. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  CCM fitna zitawamaliza James Milya amefitiniwa na George Nangale the outgoing EALA member kwa kumtanguliza Kijana wake Mrisho Gambo kwani wangalipita vijana wawili Milya angeleta ushindani mkubwa kwake!
   
 12. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Katika uchaguzi huu Lusinde kaibuka na hadhi nyingine kabisa ya kuvuliwa uheshimiwa na kuitwa MSHENZI LUSINDE kwa kuanzia nitamwandikia barua ataikuta kwenye pigeon hall yake bungeni rasmi kumjulisha wadifa huu mpya.
   
 13. b

  betty marandu JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 710
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 80
  Ccm have got new name CHAMA CHA MATUSi
   
 14. w

  wakuwaza JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Sikumsikia kiongozi hata mmoja wa CCM katika kampeni za Arumeru Mashariki akizungumza la maana. Lakini wananchi wa Arumeru wameonyesha kwa vitendo kuwa hawawataki watu hawa. Huwezi kudanganya watu wenye akili zao na wakakukabali. CCM irudi Lumumba ijisahihishe, vinginevyo huu ndio mwanzo wa mwisho wake.
   
Loading...